Mwamuzi mtanzania Frank John Komba ni miongoni mwa waamuzi walioorodheshwa kuchezesha michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17 Africa Cup of Nations) michuano ambayo imepangwa kufanyika Gabon.
Komba yupo kwenye orodha ya waamuzi wasaidi (Assistant Referees au washika kibendera) na ni mwamuzi pekee kutoka Tanzania aliyepata fursa hiyo kutoka Tanzania. Komba anaungana na waamuzi wengine wawili kutoka ukanda wa Afrika Mashariki Pacifique Ndabihawenimana (mwamuzi wa kati kutoka Burundi na Davies Ogenche Omweno (mwamuzi wa kati kutoka Kenya).
![]() |
Orodha ya waamuzi watakaochezesha mashindano ya vijana nchini Gabon mapema mwezi ujao |
No comments:
Post a Comment