Baada ya sare ya tasa dhidi ya timu ya Chuo cha afya
Mbweni timu ya chuo cha waandishi wa habari Zanzibar leo hii inajitupa tena
dimbani kuoneshana kazi na timu ya chuo cha MCC mtanage ambao utavurumishwa
katika dimba la Fuoni mnamo majira ya saa kumi alasiri.
![]() |
KOCHA WA TIMU YA UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR ABUBAKARY HATIBU |
Mtanange huo unatarajiwa kuwa na ushindi kwa pande
zote huku kila timu ya ikijinadi kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Kocha wa timu ya chuo cha waandishi wa habari Zanzibar
Abubakary Hatibu amesema wamejipanga kuona wanafanya vyema katika mchezo huo
huku akitarajia kuwapanga wachezaji ambao wanauwezo wa hali ya juu.
![]() |
WACHEZAJI WA TIMU YA CHUO CHA HABARI WAKIWA NA KOCHA WAO KISANDU |
“Unajua tulitoka sare na afya mchezo ambao ulikuwa
na upinzani huku tukiwa pungufu nimerudi mazoezi na vijana wangu nimeyafanyia
kazi mapungufu naamini vijana watafanya vyema katika mchezo na MCC”Alisema
Kisandu.
![]() |
KISANDU AKIWA MZIGONI |
Akizungumzia vitendo vya utovu wa nidhamu
vilivyofanya na mchezaji wake kocha huyo ameelezea kusikitishwa kwake na kitndo
hicho huku akiongeza kuwa uongozi wao timu yake umemsimamisha mchezaji huyo na
hatamtumia tena katika mchezo wa leo.
No comments:
Post a Comment