Wednesday, 10 May 2017

UTAWALA WA TIMU YA VIKOSI LIGI KUU UNAELEKEA MWISHO WAKE ,NYOTA MIEMBENI CITY , CHARAWE WASEMA WAO HAWATORUDI KAMA CHWAKA.



Ushindi katika michezo mitatu katika hatua  ya nne bora ligi daraja la kwanza taifa Unguja imeifanya timu ya Miembeni City kuibuka vinara wa ligi hiyo na kujikatia tiketi yakushiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018.

Miembeni City ambao walianza kuwafunga Charawe magol mawili 2-0,wakawafunga tena magol 2-0 Sebelen nakumaliza kwa kuwafunga Ngome idadi hiyo hiyo ya magol katika mchezo wa jana ambao magol yakifungwa na mshambuliaji Yahya Haji Salim (Karoa) na nahodha msaidizi kiungo Haroun Abdallah Jabir ( Boban).

Wakizungumza mara baada ya mchezo huo wachezaji wa Miembeni City wameelezea kufurahishwa kwa na ushindi huo huku wakiahidi kujakupambana katika hatua ambao wamefika kwa sasa.

"Unajua kwa misimu mitatu sasa timu yetu inamaliza nafasi ya kwanza katika kila hatua hivyo hata huku tulipofika tutapambana kuendeleza rekodi yetu hiyo" walisema.

Aidha nyota hao wamesema kuwa wameona kila mwaka ligi kuu ya Zanzibar ushindi huenda katika timu ya vikosi hivyo wao watahahkikisha wafanya mapinduzi kwa kutwaa ubingwa huo.

"Hatujajua kutakuwa na mfumo gani lakini sisi pop[ote pale tutakaposhiriki tutahakikisha tunakuwa wa kwanza nakuondoa ile tabia yakuwa timu za vikosi ndizo zinazokaa juu katika msimu wa ligi ,tutahakikisha kile kinachofanya Jang'ombe boys kwa sasa ndicho tutakachokifanya na sisi" waliongeza.
Wachezaji wa Miembeni City baada ya ushindi wa magol 2-0 dhidi ya Ngome


Timu nyengine iliyoungana na Miembeni City kutinga ligi kuu timu ya Charawe ambao walitinga katika hatua hiyo kwa kujinyakulia alama 6 baada yakuwafungwa Ngome 4-2 nakuwafunga Seblem jumla ya magol 3-0.


Mara baada ya mchezo huo kati ya Charawe na Seblen wachezaji wa timu ya Charawe wamesema wanakuja kupambana na wala hawatakuja nakurudi kama walivyofanya majirani zao Chwaka.

Wameelezea kufurahishwa kwao na hatua ambayo timu yao imefika huku wakiahidi kufanya vyema katika hatua inayofuta .


Wachezaji wa Charawe wakisalimiwa na mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayoub Mahmoud

No comments:

Post a Comment