Saturday, 13 May 2017

ZIMAMOTO,OKAPI WAANZA VYEMA KAMPENI ZAKUWANIA UFALME WA SOKA ZANZIBAR

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya Zimamoto imeanza vyema kampeni zake zakuwania ubingwa wa Zanzibar baada yakuifunga timu ya JKU goli 1-0 mchezo wa kwanza hatua ya nane bora ligi kuu soka ya Zanzibar mchezo uliovurumishwa katika dimba la Amani mjini Unguja.

Kikosi cha Zimamoto kilichoanza leo katika mchezo na JKU mchezo ambao wameibuka na ushindi wa gol 1-0.


Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani kwa pande zote Zimamoto walijipatia goli mnamo 35 kupitia kwa mchezaji wake Hassan Haji. 

Nako katika kiwanja cha Gombani kisiwani Pemba timu ya Okapi nayo ikaanza vyema hatua hiyo baada yakuifunga timu ya Kizimbani jumla ya magol 2-1.

Kikosi cha JKU

Ratiba ya michezo ya hatua ya nane bora 




No comments:

Post a Comment