Saturday, 13 May 2017

JKU,ZIMAMOTO KATIKA PICHA.

Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto Yussuf Ramadhani akimpita beki wa Timu ya JKU Edward Peter 
Mshambuliaji  wa Timu ya Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika (mwenye jezi ya njano) akimiliki mpira mbele ya mlinzi wa timu ya JKU Issa Haidar  katika mchezo wa mwanzo wa hatua ya nane bora ligi kuu soka ya Zanzibar  mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika akimpita beki wa Timu ya JKU Mwinyijuma Mwinyi, wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Zanzibar Nane Bora uliofanyika uwanja wa amaan


Kocha Mkuu wa Timu ya JKU  Mohamed Seif King akifuatilia mchezo kati ya timu yake na timu ya Zimamoto mchezo ambao JKU wamekubali kipigo cha goli 1-0. 


Baadhi ya washabiki waliohudhuria katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kati ya JKU na Zimamoto
Mshambuliaji wa timu ya JKU Suweid Juma mwenye mpira akijiandaa kumpita beki wa timu ya Zimamoto Suleiman Said.

Kocha wa timu ya Zimamoto Seif Bausi alievaa fulana nyeupe akisalimiana na kocha wa timu ya JKU Mohamed Seif King kabla yakuanza kwa mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya nane bora kati JKU na Zimamoto mchezo ambao Zimamoto imeibuka na ushindi wa gol 1-0.

No comments:

Post a Comment