Wakiwa katika
mikakati yakukiimarisha kikosi chao baada yakupandisha ligi kuu soka ya
Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018 uongozi wa timu ya Miembeni City wamepania
kufanya usajili wa nguvu ilikuimarisha kikosi chao.
![]() |
MKURUGENZI WA UFUNDI WA TIMU YA MIEMBENI CITY AKIZUNGUMZA NA WASHAMBULIAJI WA TIMU HIYO IBRAHIM ABDALLAH(MKOKO) NA SAID PAMBA |
Kwa mujibu wa taarifa
ambayo mtandao huu umezipata ni kwamba uongozi wa timu hiyo wapo katika
mazungumzo na nyota kadhaa ambao katika msimu uliopita walizitumikia timu
zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Afisa habari wa timu
hiyo Ali Khamis ( Ibny) amesema mara baada yakumalizika kwa ligi daraja la
kwanza taifa na timu yao kumalizakwa mafanikio makubwa mwalimu wa timu hiyo
sambamba na beanch zima la ufundi
lilitoa mapendekezo yake ya nafasi gani zijazwe na tayari uongozi wa timu
unayafanyia kazi mapendekezo hayo.
![]() |
RAIS WA TIMU YA MIEMBENI CITY SEIF KOMBO ALIEVA NGUO NYEUSI AKISHUHUDIA NAHODHA WA TIMU YAKE HABIBU ALI AKIKABIDHIWA KOMBE LA USHINDI WA LIGI DARAJA LA KWANZA TAIFA UNGUJA |
“Unajua tumemaliza
msimu kwa mafanikio nakupandisha timu kinachofanyika kwa sasa nikuona tunafanya
usajili wa maana kulingana na daraja ambalo timu itacheza na mchezaji yoyote
yule ambae timu itakuwa inamuhitaji tutamsajili hata kama atakuwa anacheza Yanga,Simba,Azam na timu nyengine hapa
Tanzania tutamsajili nakuitumikia Miembeni City”Alisema Ibny.
Ameongeza kuwa
wamepania kukiimarisha zaidi kikosi chao ili kiwe bora zaidi nakuleta upinzani
wa hali ya juu huku wakijua kuwa ligi ambayo timu imepanda ni nguvu na yenye ushindani hivyo lazima kukiimarisha kikosi
chao kiweze kupambana.
Kuhusu suala la ligi
ndogo msemaji huyo amesema hilo suala ni la chama cha soka hivyo yeye hawezi
kulizungumzia bali wanachojua wao ni kukiimarisha kikosi chao ili kiwe imara na
kiweze kuwa cha ushindani zaidi.
![]() |
KHAMIS MCHA VIALI |
Miembeni City ambayo
imefanikiwa kutinga ligi kuu soka ya Zanzibar baada yakutwaa ubingwa wa ligi
daraja la kwanza taifa Unguja kwa kushinda katika michezo yake yote ya hatua ya
nne bora.
No comments:
Post a Comment