Wanamichezo visiwani Zanzibar wametakiwa kuvitumia vipaji vyao
ipasavyo katika kuitangaza Zanzibar kimataifa sambambana kujikwamua kimaisha.
![]() |
WANAMICHEZO WA ZANZIBAR WAKIMSIKILIZA NAIBU WAZIRI WA HABARI ,UTALII,UTAMADUNI NA MICHEZO CHUMU KOMBO HAYUPO PICHANI. |
Ushauri huo umetolewa na naibu waziri wizara ya habari
utamaduni,utalii na michezo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Chumu Kombo
wakati alipokuwa akizungumza na wanamichezo wa Zanzibar wanatarajiwa kushiriki
katika mashindano ya Umiseta.
Amesema kuwa kwa sasa Zanzibar imepatiwa uanachama wa shirikisho
la soka barani Afrika hivyo umefika wakati sasa kwa vijana kuitumia fursa hiyo
ipasavyo ilikuweza kujikwamua na umasikini kupitia vipaji vyao.
Nae naibu waziri wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar
Mmanga Mjengo amewataka wanamichezo hao kuzingatia suala zima la nidhamu
watakapokuwa katika michezo hiyo.
Jumla ya wanamichezo 135 kutoka Unguja na Pemba wameondoka Unguja mchana wa leo
kuelekea Tanzania bara kushiriki katika mashindano ya michezo na sanaa
skuli za secondary Tanzania Umiseta.
No comments:
Post a Comment