Makocha wa soka
Visiwani Zanzibar wameshauriwa kuchukua fomu zakujiunga na uanachama wa chama
cha Makocha visiwani Zanzibar ili kuendana na matakwa ya shirikisho la soka
barani Afrika.
![]() |
Mustafa Hassan katibu msaidizi ZAFCA |
Ushauri huo umetolewa
na katibu msaidizi wa chama cha makocha Zanzibar Mustafa Hassan wakati alipokuwa
akizungumza na Mtandao huu nakusema kuwa kujiunga katika chama hicho kutasaidia
kutumia fursa zitakazokuja kwa ufanisi mkubwa.
“Nawaomba makocha
wenzangu waje kujiunga na ZAFCA, mana huko tunakokwenda ni kugumu mno, baada ya
ZFA kuwa mwanachama wa CAF, tumetakiwa makocha wote wajinge na chama chao ili
watambuliwe na ZFA na hapo ndipo utapata fursa ya kusoma kozi mbali mbali za
makocha”. Alisema Mustafa.
Ameongeza kuwa mafunzo yote ya ukocha ambayo yatakuja visiwani yatatoa kipaumbelea kwa wale ambao watakuwa ni wanachama wa chao hicho
No comments:
Post a Comment