Timu ya Jang’ombe
inatarajiwa kuondoka visiwani Zanzibar asubuhi ya kesho kuelekea Tanzania bara
ambapo itashiriki katika mashindano ya Sport Pesa Super Cup.
![]() |
KIKOSI CHA JANG'OMBE BOYS AMBACHO KITAONDOKA KESHO KUELEKEA TANZANIA BARA KATIKA MASHINDANO YA SPORT PESA SUPER CUP. |
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na rais wa timu hiyo Ali Othman wanandinga hao wanatarajiwa kuondoka mnamo
majira ya saa tatu asubuhi kwa boti za Azam Marine.
![]() |
JANG'OMBE BOYS |
Boys ambao wamepangwa
kucheza Jumanne ,June 6, 2017 na Gor
mahia kutoka nchini Kenya wanaenda katika mashindano hayo wakihitaji ushindi.
Akizungumzia hali ya
kikosi chao rais wa timu hiyo amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri huku
wakitarajia kufanya vyema katika mashindano hayo.
Mshindi katika
mashindano hayo anatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Everton
inayoshiriki ligi kuu soka ya Uengereza.
RATIBA YA AWALI YA
MASHINDANO HAYO
Jumatatu 5/6/2017
Singida united Vs FC
leopard
Yanga Vs Tusker fc
Jumanne 6/6/2017
Simba Vs Nakuru All
Star
Jang`ombe boys vs Gor
mahia
No comments:
Post a Comment