Thursday, 1 June 2017

KAMATI SOKA LA UFUKWENI VISIWANI IMEJIPANGA KUIMARISHA MCHEZO HUO

Kamati inayosimamia mashindano ya soka la ufukweni visiwani Zanzibar imekabidhi mpango kazi wake kwa mwaka 2017-2020 kwa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa habari wa kamati hiyo Suleimani Ussi Mido mpango kazi huo ndio utakafuatwa katika kuendesha shughuli zote za kamati hiyo.

Aidha Mido amesema chama cha mpira wa miguu visiwani kimetoa baraka zote kwa kamati hiyo inayosimamia soka la ufukweni sambamba na mpango kazi wake.

KIWANJA CHA KUCHEZEA BEACH SOCCER


Mpango kazi wa kamati ya mashindano ya vijana ni kama ifuatavyo.

MWEZI –JANUARY .

Mashindano ya kombe la mapinduzi kwa vilabu vya beach soccer Zanzibar .

MWEZI-FEBRUARY .

Mafunzo ya waamuzi wa beach soccer kwa ngazi ya zone ya mpira mashariki kwa waamuzi wa beach soccer wa Zanzibar.

MWZI –MARCH.

 Michezo ya maonesho ya mchezo wa beach soccer mawilayani .pia kushiriki mashindano ya beach soccer kwa nchi za ukanda wa CECAFA

MWEZI- APRIL

Usajili wa vilabu  vyote vya beach soccer kwa mrajisi wa vyama vya michezo na club ambavyo vitashiriki katika mashindano ya amabyo yanayosimamiwa na kamati ya beach soccer chini ya ZFA taifa Zanzibar .

MWEZI –MAY .

Kuanza kwa usajili wa wachezaji katika vilabu na uhamisho .

MWEZI- JUNE .

Viongozi  wa kamati ya beach soccer kutembelea wilaya zote za unguja na pemba kuhamasisha mchezo wa huo kwa kutumia timu ya taifa ya ufukwen ( sand heroes.)

MWEZI –JUNE

Kurejesha fomu za usajili pamoja na kupitia  usajili .

MWEZI-JUNE

Mkutano wa kamati ya becach soccer pamoja na viongozi wa vilabu vyote vitakavyoshiriki ligi ya beach soccer .




MWEZI –JUNE

Mafunzo maalumu  kwa walimu (coaches ) wa vilabu vya beach soccer juu ya kujua kanuni za na sheria za mchezo .

MWEZI –JULY

Kuanza  kwa mashindano ya ligi ya beach soccer .

MWEZI-SPET .

Kushiriki mashindano ya ya becach soccer yanayotayarishwa na shirikisho la  mpira wa miguu Africa CAF.

MWEZI-OCT

Kumalizika kwa ligi ya beach soccer .

MWEZI-NOVEMBER

Mafunzo ya waamuzi na walimu wa beach soccer ngazi ya kitaifa pamoja na walimu waliochaguliwa na wizara ya elimu kupata mafunzo haya kupitia  idara ya michezo na utamaduni ,

MWEZI –DECEMBER .

Mashindano ya vijana ( beach soccer youth tournament ).





No comments:

Post a Comment