Thursday, 1 June 2017

SOKA LA UFUKWENI ,FURSA KWA VIJANA WA KIZANZIBAR..DULLA SUNDAY


Katibu mkuu wa mashindano ya vijana visiwani Zanzibar Abdallah Thabit (Dulla Sunday) amewataka vijana kuitumia fursa ikiyopo sasa katika kushiriki katika mchezo wa soka la ufukweni.
WACHEZAJI WA SOKA LA UFUKWENI WAKIWA KATIKA MCHEZO HUO.

Ushauri huo ameutoa wakati alipokuwa akizungumza nasi nakusema kuwa endapo vijana watashiriki katika mchezo huo utawasaidia kujitangza kupitia mchezo huo ambao kwa kwa sasa umekuwa ukipewa kipaumbelea na shirikisho la soka barani Afrika sambamba na FIFA.

Ameongeza kuwa ushiriki katika mchezo huo wa soka la ufukweni utasaidia kwa baadhi ya vijana ambao wameshindwa kushiriki kimataifa kupita michezo mengine kuonesha uwzo wao nakushiriki kimataifa.



Aidha katibu huyo amewataka wadau mbalimbali wa soka nchini kuungana na kamati inayosimamia mipira wa ufukweni ilikuimarisha mchezo huo nakutoa nafasi kadhaa kwa vijana wa kizanzibar kuonesha vipaji ambavyo wanavyo.

No comments:

Post a Comment