Kufuatia kutoitwa kwa wanariadha wa
Zanzibar kujumuika na wenzao wa Tanzania bara katika timu ya taifa ya riadha ya
vijana ya Tanzania baadhi ya walimu wa mchezo huo visiwani wameelezea kuumizwa na
kitendo hicho.
Akizungumza na mtandao huo mmoja wa
makocha hao Abdallah Juma Abeid amesema kutokana na kiwango kilichooneshwa na
wanariadha wa Zanzibar katika mashindano ya riadha ya Afrika Mashariki na Kati yaliyomalizika
hivi karibu suala lakutoitwa katika timu ya taifa ya Tanzania kunarejesha nyuma
juhudi zao.
Ameongeza kuwa kutoka na ushindi ambao
wameupata wachezaji hao lazima wachezaji hao walikuwa wajumuishe katika orodha
za wachezaji ambao watashiriki katika mashindano ya riadha ya Afrika sambamba
na Dunia.
“Unajua wachezaji tayari wameitwa na
tayari wanatarajiwa kuenda katika kambi yakujiandaa na mashindano ya Afrika
nchini Kenya lakini hakuna mchezaji hata mmoja wa Zanzibar alieitwa katika timu
hiyo jambo ambalo linarejesha nyuma juhudi zao”alisema Abdallah.
Aidha amesema kuwa mashindano ya riadha
ya Afrika kwa vijana yanatarajiwa kufanya nchini Algeria mwanzoni mwa mwezi wa
sita na yale ya dunia yakitarajiwa kufanyika nchini Kenya mwezi wa saba.
Akiwataja vijana ambao walifanya vyema
katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati ambao wanastahiki kuwepo katika
timu hiyo ni pamoja na Omar Rashid(Burning),Kazija Hassan,Hafidh Abdallah na
Dahala Musilihi Dahala ambao walitwaa medal ya dhahabu katika mashindano hayo
lakini hawajajumuishwa katika timu hiyo ya taifa ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment