Sunday, 4 June 2017

JANG'OMBE BOYS MZIGONI KESHO SPORT PESA SUPER CUP.

Michuano ya sport pesa super cup yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake jioni ya leo kwa michezo miwili  ambapo mchezo wa ufunguzi utazikutanisha timu za  Singada United na FC Leopard huku mchezo wa pili ukiwa kati ya timu ya Tusker FC ya Kenya na Yanga ya Dar es Salam mitanange ambao unavurumishwa katika uwanja wa Uhuru jiji Dar es Saalam.
Wachezaji wa timu ya AFC Leopards ya Kenya wakiwa katika mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa karume jijini Dar es Salaam, janaJuni 4, 2017 kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya 'SportPesa Super Cup' 


Hapo kesho timu peke kutoka Zanzibar ambayo itashiriki katika mashindano hayo ya Sport Pesa Super Cup timu ya Jang’ombe Boys ikitarajiwa kutupa karaka yake ya kwanza hapo kesho kwa kumenyana na Gor Mahia kutoka nchini Kenya.

Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu akiwa Tanzania bara rais wa timu ya Jang’ombe boys Ali Othman Kibichwa amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri huku vijana wakiwa na ari yakufanya vyema katika mashindano.
Wachezaji wa timu ya Tusker ya Kenya wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, jana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya 'SportPesa Super Cup

“Tumealiza mazoezi asubuhi hii katika uwanja wa uhuru kuwapisha wenzatu na wao wafanye mazoezi ari ya wachezaji ipo ya hali ya juu hamasa imeongezeka na wanamsikiliza mwalimu kile anachowafundisha kikubwa wazanzibar watuombee dua maana huku hatujaja kama Jang’ombe boys tumekuja kutafuta heshima ya Zanzibar”alisema kibichwa.

Akizungumzia majeruhi katika kikosi rais huyo amesema kwa mujibu wa ripoti ya daktari wao mchezaji majeruhi ni mmoja ambae ni mlinzi Ali Humud Balii wamemuacha Zanzibar lakini nyota wote waliosafiri nao wapo vizuri.
Kikosi cha Jang'ombe boys


Mchezo mwengnie utakaovurumishwa hapo ambao ndi utakuwa mchezo wa mwanzo kwa kesho wekundu wa msibazi Simba itaoneshana kazi na Nakuru All Star. 

1 comment:

  1. Kila la kheri boys wawakilishi wetu Zanzibar tunwaombea ushindi dhidi ya Gor Mahia na mushinde hizo milioni 60 VIVA Boys.

    ReplyDelete