Michuano ya sport pesa super cup yanatarajiwa kuanza
kutimua vumbi lake jioni ya leo kwa michezo miwili ambapo mchezo wa ufunguzi utazikutanisha timu za Singada United na FC Leopard huku mchezo wa pili ukiwa kati ya timu ya Tusker FC ya Kenya
na Yanga ya Dar es Salam mitanange ambao unavurumishwa katika uwanja wa Uhuru jiji Dar es Saalam.
![]() |
Wachezaji wa timu ya AFC Leopards ya Kenya wakiwa katika mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa karume jijini Dar es Salaam, janaJuni 4, 2017 kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya 'SportPesa Super Cup' |
Hapo kesho timu peke kutoka Zanzibar ambayo itashiriki katika
mashindano hayo ya Sport Pesa Super Cup timu ya Jang’ombe Boys ikitarajiwa
kutupa karaka yake ya kwanza hapo kesho kwa kumenyana na Gor Mahia kutoka
nchini Kenya.
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu akiwa Tanzania
bara rais wa timu ya Jang’ombe boys Ali Othman Kibichwa amesema kikosi chao
kipo katika hali nzuri huku vijana wakiwa na ari yakufanya vyema katika
mashindano.
“Tumealiza mazoezi asubuhi hii katika uwanja wa uhuru
kuwapisha wenzatu na wao wafanye mazoezi ari ya wachezaji ipo ya hali ya juu
hamasa imeongezeka na wanamsikiliza mwalimu kile anachowafundisha kikubwa
wazanzibar watuombee dua maana huku hatujaja kama Jang’ombe boys tumekuja
kutafuta heshima ya Zanzibar”alisema kibichwa.
Akizungumzia majeruhi katika kikosi rais huyo amesema kwa
mujibu wa ripoti ya daktari wao mchezaji majeruhi ni mmoja ambae ni mlinzi Ali
Humud Balii wamemuacha Zanzibar lakini nyota wote waliosafiri nao wapo vizuri.
![]() |
Kikosi cha Jang'ombe boys |
Mchezo mwengnie utakaovurumishwa hapo ambao ndi utakuwa mchezo wa mwanzo kwa kesho wekundu wa msibazi Simba itaoneshana kazi na Nakuru All Star.
Kila la kheri boys wawakilishi wetu Zanzibar tunwaombea ushindi dhidi ya Gor Mahia na mushinde hizo milioni 60 VIVA Boys.
ReplyDelete