Sunday, 20 August 2017

Neymar wa Miembeni City kuungana na wenzake wiki hii.

 Mchezaji Ramadhani Khamis Muhamed(Neymar) ambae amesajiliwa na Miembeni City kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Jang’ombe boys anatarajiwa kujiunga katika mazoezi ya timu yake hiyo mpya Agost 24 tayari kujianda na msimu ujao wa ligi kuu soka ya Zanzibar.
 
Ramadhani Khamis Muhamed(Neymar) akiwa na jezi ya timu yake zamani Jang'ombe boys.
Neymar ambae ni miongoni mwa nyota waliong’ara katika msimu wa 2016-2017 ligi kuu soka ya Zanzibar amepewa mapumziko ya wiki moja kabla yakujiunga na wenzake katika mazoezi ya timu hiyo ambayo katika msimu huu wa ligi wanacheza ligi kuu soka ya Zanzibar kwa mara ya kwanza.

Akizungumza na mtandao huu mkuu wa kitengo cha habari wa Miembeni City Ali Khamis amesema mwalimu ameamua kumpa mapumziko hayo kwa sababu nyota huyo hakuapata mapumziko kwa vile alikuwa akiitumikia timu yake katika michezo ya ligi kuu.

“Nikweli tumemsajili Ramadhani Khamis Muhamed (Neymar) kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Jang’ombe boys lakini kwa vile alikuwa akiitumikia timu yake kwenye michezo ya ligi kuu soka ya Zanzibar iliyomalizika wiki iliyopita tumeamua kumpumzisha hadi hapo Agost 24 na hapo ataanza kujiunga na wenzake katika mazoezi.


Nyota huyo ambae alikuwa chachu ya mafanikio kwa timu yake katika msimu uliopita wa ligi kuu soka ya Zanzibar alikuwa miongoni mwa nyota waliounda timu ya combine ya wilaya ya mjini iliyotwaa ubingwa katika mashindano ya Rolling stone mwaka 2016 huko mjini Arusha.

No comments:

Post a Comment