Zoezi la usajili na
uhamisho visiwani Zanzibar limemalizika Alkhamis Agost 17 nakuenda vizuri na kinachofata
sasa nikupitiwa kwa fomu hizo nakuhalalishwa kwa wachezaji kucheza timu husika.
Akizungumza na mtandao
huu katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu Zanzibar Muhamed Tedy amesema
kumalizika kwa zoezi hilo chama chao kinajipanga kuzipitia fomu hizo.
“Tutarajia kuzipita
fomu hizo kesho Jumapili mbele ya viongozi wa vilabu na tutaanza na ligi kuu
lengo nikuondoa utata ambao unaweza kujitokeza katika upitishwaji huo wa fomu”
alisema.
Ameongeza katika
kuendesha zoezi hili watahakikisha wanafuata kanuni na sheria na mwaka huu
chama chao kimejipanga kuona wanatekeleza kanuni kwa asilimia zote.
Kuhusu msimu wa
2016-2017 ambao umefikia tamati hapo jana katibu huyo amesema msimu huo
umemalizika kwa mafanikio licha ya changamoto ambazo zimejitokeza katika
kuendesha ligi hiyo.
Akizungumzia vitendo
vya uoangaji wa matokeo ambavyo vilionekana vikijitokeza katika michezo ya ligi
kuu soka ya Zanzibar kwa 2016-2017 katibu huyo amesema chama chao kinajipanga
kukomesha vitendo kama hivyo.
Msimu wa ligi 2016-2017
ligi kuu soka ya Zanzibar umemalizka jioni ya jana ambapo timu ya JKU kwa mara
ya kwanza wametwaa ubingwa wa ligi hiyo huku Zimamoto wakitwaa nafasi ya pili .
No comments:
Post a Comment