Saturday, 19 August 2017

SIMBA YAIRARUA 5-0 GULIONI FC, MAVUGO AONESHA UFUNDI WAKUPASIA NYAVU.

Wakiwa wanaendelea kujiandaa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya watani wao wa timu ya Simba usiku wakuamkia leo imejitupa katika dimba la Amani mjini Unguja kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Gulion FC inayoshiriki ligi daraja la pili wilaya ya mjini Unguja.
 
Wachezaji wa Simba wakisikiliza maelekezo ya walimu wao.
Katika mchezo huo ambao Simba waliutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa wekundu hao wa msimbazi imeibuka na ushindi wa magol 5-0 magoli yaliyofungwa na mshambuliaji Laudit mavugo katika dk ya 13 na 40, Shiza kichuya dk ya 37,Juma luzio dk ya 41 na Mohd Ibrahim,mo akaimalizia karamu ya bao mnamo dakika ya 67.

Simba ambao wameonekana kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa nakuwazidi wapinzani wao huu utakuwa mchezo wa mwisho wa majaribio kisiwani hapa.
 
Kocha wa Gulion Birhani Msoma.
Akizungumzia mchezo huo kocha msaidizi wa timu ya Simba Jackson Mayanja amesema mchezo huo umesaidia kuona kasoro zilizopo katika kikosi chao nakuyafanyia kazi.


Aidha amesema wamejaribu kubadilisha mfumo kwa kuchezesha washambuliaji wawili ilikutengeneza peya kutokana na kukabiliwa na majeruhi kwa baadhi ya nyota wao akiwemo mshambuliaji Bocco na Okwi.

Kwa upande wake kocha wa timu ya Gulion Burhan Msoma amesema wamepoteza mchezo huo kutokana na wachezaji wake kutokuwa imara kimwili.

Simba wanatarajiwa kuondoka visiwani August 22 kuelekea Tanzania bara tayari kuwakabili wapinzani wao Yanga mtanange ambao utavurumishwa August 23 katika uwanja wa taifa Dar es Salam.


Kikosi cha Gulioni FC kilikuwa; Haji Yussuf, Ibrahim Hamisi, Shaaban Hassan, Mohammed Omar, Nuhu Ally, Ulele Uledi, Hamad Kawamba, Ally Mbaraka, Ally Amour, Ally J Kipanga na Fahim Khalfan.

Simba SC; Aishi Manula/EmManuel Mseja, Erasto Nyoni, Ally Shomary/Mohammed Hussein ‘Thshabalala’, Salim Mbonde, Method Mwanjali/Paul Bundala, James Kotei/Jonas Mkude, Haruna Niyonzima/Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin/Said Ndemla, Laudit Mavugo/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Juma Luizio na Shiza Kichuya/Jamal Mnyate. 

No comments:

Post a Comment