Saturday, 21 October 2017

Imani yangu vijana watafanya kazi nakupata matokeo mazuri mbeleni,kocha Miembeni City.

Licha yakupokea kipigo cha tatu mfululizo kocha mkuu wa timu ya Miembeni City asema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na vijana wake katika mchezo dhidi ya JKU.
 
Kikosi cha Miembeni City kilichoanza katika mchezo wa jana na JKU.
Akizungumza na mtandao huu mara baada ya mchezo wa timu hiyo na JKU kocha wa timu hiyo Muhamed Seif King amesema ameona mabadiliko makubwa katika kikosi chake katika kila mchezo na anamatumaini makubwa yakufanya vyema katika michezo ijayo.

Ameongeza kuwa kikosi chake ni kigeni katika ligi lakini pia kinaunda na vijana ambao ni wanagenzi lakini katika kila mchezo wameonekana wakibalika jambo ambalo yeye kama mwalimu linampa matumaini na anaamini watafanya vyema katika michezo ya mbeleni.

Miembeni City ambayo tayari imeshashuka dimbani mara tatu nakupoteza katika michezo yote mitatu ambapo walifungwa na Polis gol 1-0,kisha mafunzo 1-0 na jana kukubali kipigo cha idadi kama hiyo cha goli 1-0 kutoka kwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo JKU.






No comments:

Post a Comment