Michezo ya mzunguko wa kwanza ligi kuu soka ya
Zanzibar sambamba na ligi daraja la kwanza taifa Unguja imeenda vizuri huku
ushindani ukionekana wa hali juu ka timu shiriki.
Hayo yameelezwa na katibu mkuu wa chama cha mpira wa
miguu visiwani Zanzibar Muhamed Hilal Tedy wakati alipokuwa akizungumza na
mtandao huu nakusema kuwa ushindani ulioneshwa na timu husika unaashiria
maandalizi mzuri kwa timu hizo.
Ameongeza kuwa chama chao kitasimamia kanuni na sheria
zakuenda mashindano hayo ikiwemo lessen kwa walimu wanaofundisha timu shiriki
ambapo kanuni inahitaji mwalimu kuanzia lessen B.
Akizungumzia timu ambazo hazijafata kanuni na sheria
ya mashindano hayo katibu huyo amesema chama chao kinajipanga kuwapatia adhabu
kwa mujibu wa sheria na kanuni.
Kuhusu suala la waamuzi ambao wamechezesha michezo
hiyo nakulalamikiwa katibu huyo amesema tayari chama chao kimeshafanya
mazungumzo na viongozi wa waamuzi hao kuhusu suala hilo.
Aidha amewataka wadau na wapenda mchezo wa soka
kujitoka kwa wengi viwanjani ilikuunga mkono timu zao.
Ligi kuu soka ya Zanzibar inatarajiwa kuendelea
October 15 ,ambapo michezo miwili itavurumishwa siku hiyo mnamo majira ya saa 8
mchana JKU itakipiga na timu ya Chuoni huku mnamo majira ya saa kumi alasiri
Miembeni City itakipiga na Mafunzo.
No comments:
Post a Comment