Monday, 9 October 2017

KWEREKWE CITY MAUNGANI ,WATAMBIANA.

Ligi daraja la pili taifa Unguja inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake jioni ya leo ambapo michezo minne ya inatarajiwa kuvurumishwa katika viwanja vine tofauti.

Katika kiwanja cha Ngome Fuoni Zantex itakipiga na Bweleo ,huku katika kiwanja cha Tazari New King itaikaribisha New book.

Sungusungu BZL itaoneshana kazi na Mchangani na katika kiwanja cha Maungani Maungani itakipiga na Kwerekwe City.

 Michezo hiyo itavurumishwa mnamo majira ya saa kumi alasiri

No comments:

Post a Comment