Baada yakuenda
mapumzikoni kwa takribani siku mbili ligi kuu soka ya Zanzibar kituo cha Unguja
inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho kwa kuanza michezo ya mzunguko wa nne.
Ambapo hapo
kesho mtanange mmoja utavurumishwa katika kiwanja cha Amani mjini Unguja mnamo
majira ya saa kumi alasiri ambapo timu ya Chuoni itajitupa katika kiwanja cha
Amani kuoneshana kazi na timu ya Miembeni City.
Chuoni
inashuka katika kiwanja cha Amani mjini hapa wakiwa na alama 4 huku Miembeni
City wenyewe wakijitupa katika mchezo huo wakiwa na rekodi mbaya yakupoteza
michezo mitatu mfululizo.
Michezo mengine
ya mzunguko huo wa nne ya ligi kuu soka ya Zanzibar inaendelea kesho kutwa
Jumamos ambapo mitanange miwili itavurumishwa mnamo majira ya saa nane mchana
Taifa ya Jang’ombe itakipiga na JKU huku
mnamo majira ya saa kumi alasiri KVZ inamenyana na Mafunzo.
Ikiwa ligi
hiyo inaingia mzunguko wa 4 jioni ya kesho mpaka sasa timu ya KVZ inaongoza
ligi hiyo wakiwa na alama 9 wakifuatiwa na JKU wenye alama tisa tofauti yao
ikiwa ni magol yakufungwa nanakufunga.
Ratiba kamili ya michezo ya mzunguko
IJUMAA
|
27/10/017
|
22
|
MIEMBENI CITY
|
VS
|
CHUONI
|
SAA 10:00 ALS AMAAN
|
J’MOSI
|
28/10/017
|
23
|
TAIFA YA J/MBE
|
VS
|
JKU
|
SAA 8:00 MCH AMAAN
|
J’MOSI
|
28/10/017
|
24
|
KVZ
|
VS
|
MAFUNZO
|
SAA 10:00 ALS AMAAN
|
J’PILI
|
29/10/017
|
25
|
KIPANGA
|
VS
|
POLISI
|
SAA 8:00 MCH AMAAN
|
J’PILI
|
29/10/017
|
26
|
KMKM
|
VS
|
ZIMAMOTO
|
SAA 10:00 ALS AMAAN
|
J’TATU
|
30/10/017
|
27
|
BLACK SAILORS
|
VS
|
CHARAWE
|
SAA 8:00 MCH AMAAN
|
J’TATU
|
30/10/017
|
28
|
JANG’OMBE BOYS
|
VS
|
KILIMANI CITY
|
SAA 10:00 ALS AMAAN
|
No comments:
Post a Comment