Katika
kuhakikisha wanaepusha matatizo ya kiafya kwa wachezaji wao wawapo uwanjani
uongozi wa timu ya Realkdis Fc inayoshiriki
ligi madaraja ya vijana nadani ya wilaya ya ya mjini Unguja imewafanyia vipimo
vya afya nyota wao ilikujua matatizo yanayowakabili nyota hao.
Akizungumza nasi
katibu wa timu hiyo Nassor Abdaallah amesema lengo kuu lakufanya hivyo nikujua
afya za nyota wa sambamba na kuepusha matatizo ambayo yanaweza kujitokeza kwa
wachezaji ambao kwa mujibu wa afya zao hawastahiki kucheza mpira.
Aidha ameishukuru
timu ya maktari ambayo imefanya kazi hiyo kwa kushirikia na uongozi wa timu
hiyo nakusema zoezi hilo la upimaji afya kwa wachezaji wao litakuwa likifanya
kila muda ilikulinda afya za wachezaji wao nakuwataka wachezaji wa timu hiyo
kufuata ushauri waliopewa na madaktar baada yakupima afya.
"Tunawashukuru timu ya madaktari kwa
kushirikiana na uongozi kuhakikisha kuwa zoezi hili la upimaji wa afya
limekwenda vizuri na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kugundua baadhi ya matatizo
yanayowakabili vijana wetu sambamba na kuwapa elimu ya afya jinsi ya kulinda
afya ya miili yao haswa misuli kwa kufanya mazoez kwa bidii na njia iliyo
sahihi ili iwasaidie kufanya vizuri katika mechi zao za kila siku” alisema.
Vipimo ambavyo walifanyiwa nyota hao ni pamoja na vipimo vya damu kama vile
blood group, blood glucose, blood pressure,Afya ya masikio, uoni wa macho,
misuli pamoja na joints.
No comments:
Post a Comment