Saturday, 28 October 2017

Wilaya ya mjini yazindua mashindano ya vijana ,Chura awataka makocha kuacha tabia za uzalilishaji kwa vijana.

Mashindano ya vijana Central league wilaya ya mjini Unguja yamezinduliwa rasmini asubuhi ya leo katika kiwanja cha Amani mjini Unguja kwa mchezo kati ya timu ya Aman Academy na timu ya Mpira Pesa.
Rais wa Raska zone Ali Mkanga akisalimiana na muamuzi wa mchezo kati ya timu ya Amani Academy na Mpira Pesa Abubakary Khatibu mchezo ambao umemalizika kwa sare yakufungana goli 1-1.


Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani kwa pande zote timu hizo zimetoka sare yakufungana goli 1-1.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya mjini Unguja Hassan Haji Hamza amemewataka walimu wanaofundisha soka la vijana kuachana na vitendo vya unyanyanyasaji watoto sambamba na kuwaingilia kinyume na maumbile.
Viongozi wa kamati ya mashindano ya vijana wilaya ya mjini wakiwa katika picha ya pamoja  na mgeni rasmini katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo Ali Mkanga.

Amesema kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi kwa baadhi ya makocha kushiriki katika vitendo hivyo jambo ambalo linahitajika kupingwa kwa nguvu zote.

Amesema endapo chama chao kitapata uhakika wa tuhuma hizo hatua kali watamchukulia muhusika huku akilitaka jeshi la polisi visiwani kufuatilia kwa umakini mkubwa tuhuma hizi ili kama zipo ziwezekupatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake rais wa Raska zone Ali Mkanga amewataka vijana kujituma katika michezo kwani michezo ni ajira.

No comments:

Post a Comment