Chama cha
mpira wa miguu visiwani Zanzibar kimeelezea kuridhishwa kwake na hamasa uliojitokeza kwa timu za wanawake
zinazoshiriki ligi dogo ya kinamama inayoendelea katika kiwanja cha Amani mjini
Unguja ambapo lengo nikutafuta wachezaji 20 watakaounda timu ya taifa ya
wanawake itakayoshiriki katika mashindano ya kina mama kule nchini Rwanda.
Akizungumza na
mtandao huu katibu wa chama cha mpira wa miguu Zanzibar Muhamed Ali Hilal Tedy
amesema michezo hiyo inayoendelea visiwani hapa tayari makocha waliopewa jukumu
lakutafuta wachezaji wanaendelea kufanya kazi hiyo.
Ameongeza kuwa
katika michezo iliyochezwa vijana kadhaa wameonesha viwango vya hali ya juu na
kinachosubiriwa kwa sasa ni makocha waliopewa jukumu kumaliza kazi yao
nakutangazwa watakaobahatika kuitwa katika timu ya taifa ya wanawake.
Ameongeza kuwa
tayari chama chao kimepokea majina ya wachezaji watano kutoka Pemba ambao
wataungana na 15 kutoka Unguja kutangazwa kikosi kamili.
Ameongeza kuwa
mara baada yakutangazwa kwa kikosi hicho kocha aliepewa dhama yakukinoa kikosi
hicho ataanza majukumu yakukiandaa kikosi kabla yakuondoka kuelekea katika mashindano
ya Afrika mashariki na kati kwa upande wa kina mama yanayotarajiwa kufanyika
Rwanda mapema mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment