Wednesday, 17 May 2017

GUNDU LAMTAWALA KISANDU ZAHLIFE CUP , Z.U WAENDELEZA UBABE

Matumaini ya chuo cha uandishi wa habari kusonga mbele katika mashindano ya vyio vikuu na taasisi ya elimu ya juu Zanzibar yamefifia baada ya jioni ya leo kukubali kipigo cha magol 3-0 kutoka kwa chuo cha Mwenge Community Center (MCC) mchezo uliochezwa katika kiwanja cha Ng'ome Fuoni.

Chuo cha habari kwa sasa wanasubiri mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kati ya timu ya Chuo cha Afya na timu ya MCC huku chuo cha habari huenda kikasonga ambapo MCC wataifunga timu ya Chuo cha Afya jumla ya magol 4-0.
KIKOSI CHA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR
KIKOSI CHA ZANZIBAR UNIVERSTY (Z.U)

No comments:

Post a Comment