Wednesday, 10 May 2017

SATARI AANIKA KILICHOMREJESHA KATIKA SOKA



Manager wa timu ya Mlandege inayoshiriki ligi daraja la pili wilaya ya mjini Unguja Abdul Satari amesema kitendo cha Zanzibar kupatiwa uanachama wa kudumu na shirikisho la soka barani Afrika CAF ndiko kulikopelekea yeye kurudi katika timu ya Mlandege.

Akizungumza na zenjsport on-line Satari amesema aliamua kuacha kujishughulisha na masuala ya mpira kwa kipindi kirefu lakini baada ya Zanzibar kupata uanacha wa shirikisho la soka barani Afrika ameamua kurudi katika timu yake hiyo ambayo aliongoza kwa mafanikio makubwa katika miaka ya 90.
'' Unajua mimi ni mwanamichezo na niliiongoza Mlandege kwa mafanikio makubwa katika miaka ya 90 lakini nikaamua kukaa pembeni lakini baada ya Zanzibar kupatiwa uanachama wa kudumu na shirikisho la soka barani Afrika nimerudi katika anga za michezo na nipo na timu yangu ya Mlandege ambayo nitatoa michango yangu ya hali na mali kuona timu inafanya vizuri"alisema.

Mchezaji wa Gulioni alievaa fulana nyeupe akitafuta njia zakumtoaka mlinzi wa Mlandege katika mchezo wa hatua ya nne bora ligi daraja la pili wilaya ya mjini ambapo Mlandege imeibuka na ushindi wa magol 3-1 dhidi ya Gulion.

Ameelezea kufurahishwa kwake na kiwango kilichoonesha na timu yake katika michezo miwili waliyocheza huku akiwa na matumaini makubwa yakuna timu hiyo inashiriki ligi daraja la pili taifa Unguja kwa msimu ujao wa ligi.

Amewaomba wadau mbalimbali wa soka kujitokeza kwa wingi viwanjani kuziunga mkono timu mbali mbali ili kuendana na mahitaji ya mchezo wa soka ulimwenguni.



Mwaamuzi Nassir Msomali akimsaidia kunyanyuka mchezaji wa Mlandege.

No comments:

Post a Comment