Wednesday, 10 May 2017

UMEFIKA WAKATI MAKOCHA KUINUA VIPAJI VYA VIJANA WETU ,KIJO.

Aliekuwa kocha mkuu wa timu ya Shangani FC Kijo Nadir Nyoni amesema ameamua kuachana na mpira wa ushindani nabadala yake kwa sasa ameelekeza nguvu zake zote katika kuimarisha soka la vijana.

Akizungumza na zenjsport on –line Kijo ambae kwa sasa anaifundisha katika academy ya vijana ya blacklions football academy ya Muyuni amesema ameamua kufanya hivyo ilikuinua vipaji vya watoto ambao kwa asilimia kubwa huishia njiani kutokana na kukosekana kwa muendelezo wa vijana hao.

“Nimeamua kuekeza huku katika vijana unajua Zanzibar tumejaaliwa vipaji lakini asilimia kubwa ya vipaji hupotea kutokana na kutopatiwa msingi imara wa soka” alisema.
Kocha wa timu ya Black lions football academy Kijo Nadri Nyoni alievaa fulana blue akielezea mikakati ya kituo chake cha black lions football academy

Aidha Nyoni amewataka makocha kuelekeza nguvu zao katika kuimarisha soka la vijana kwani huko ndiko kunakoanzia kuzalisha vipaji vya soka.

“Unajua kumekuwa na tabia kwa walimu kupenda kufundisha ngazi za juu nakuacha timu zetu za vijana jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya soka la vijana wetu ,hivyo ninawashauri walimu wenzangu waangalie na huku katika soka la vijana ili kusogeza mbele maendeleo ya soka la vijana”alisema Nyoni.
Wachezaji wa timu ya Black lions academy wakiwa katika mazoezi yakueka mwili sawa.

Ameongeza kuwa endapo timu za vijana zitafundishwa na walimu wenye taaluma kutapelekea vijana hao kupata msingi nzuri wa soka lao nakupelekea taifa kuwa na ligi bora na timu imara ya taifa.

Akizungumzia kituo chake cha kukuza watoto kisoka cha black lion football academy cha Muyuni kocha huyo amesema vijana waliopo katika kituo hicho wapo vizuri huku akitarajia kuwaendeleza vijana hao ambao ndio nguvu kazi ya taifa la baadae.

Amesema kwa sasa katika kituo cha hicho wapo katika mikakati ya mwisho yakukamilisha ujenzi wa mabanda ya shule ilikutoa nafasi kwa vijana wao waliopo katika kituo hicho kujipatia hudua ya kujipatia elimu katika kituo hicho.
Wachezaji wa Black lions football academy wakimsikiliza mwalimu wao Kijo Nadri Nyoni hayupo pichani baada ya mazoezi ya timu hiyo. 


Black lions football academy ina timu ambazo zinashiriki katika mashindano ya vijana chini ya miaka 20 Central league,chini ya miaka 19 Juvinile na chini ya miaka 15 Juniour.

No comments:

Post a Comment