Katika kuhakikisha
wanakiimarisha kikosi chao kwa ajli ya msimu ujao wa ligi timu ya Ruvu shuting ipo
visiwani Zanzibar kusaka nyota wataowasajili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo.
Akizungumza na mtandao
huu akiwa kisiwani Unguja msemaji wa timu hiyo Masau Bwire amesema amekuja
kuangalia vipaji vya wachezaji wa Zanzibar na kusema tayari wapo katika
mazungumzo na baadhi ya wachezaji na endapo watakubaliana anatarajia kuondoka
na nyota hao.
Amongeza kuwa tayari
uongozi wa timu hiyo wapo katika mazungumzo na nyota wawili kutoka Unguja na
endapo watafikia makubaliano nyota hao watasaini mkataba wakujiunga na kikosi
chao hicho.
Amefafanua kuwa
wanahitaji vijana wenye umri mdogo kwani wanataka kukijenga kikosi chao hicho
kwa miaka minne ijayo.
Aidha amesema kuwa ni
mapema sana kuwataja ni kina nani hao ila watakapofikiana makubakilano wataweka
bayana ni akina nani hao ambao wataitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.
No comments:
Post a Comment