Kikosi cha Miembeni City kimeanza
rasmini maandalizi ya msimu mpya wa ligi chini ya kocha Muhamed Seif King
katika kiwanja cha Amani mjini hapa.
Mlinzi wa kati wa timu ya Miembeni City Abdullatif Juma Tiago aliesajiliwa msimu huu akitokea Criss. |
Kikosi hicho ambacho kwa mara ya
kwanza kitashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu huu kimeongeza sura mpya
kumi.
Akizungumza na waandishi wa habari
mkuu wa kitengo cha habari wa timu hiyo Ali Khamis Ibny amesema wamefanya
usajili kulingana na matakwa ya mwalimu mkuu wa timu hiyo sambamba na ligi
husika.
Akiwataja nyota hao ambao
wameongezwa katika kikosi hicho ni pamoja na walinda milango Ali Rajab kutoka
Zantex na George Munish ambae ni mchezaji huru.
Pia timu imewasajili walinzi Abdullatif
Juma Tiago kutoka Criss,Halid Bofu kutoka Twalipo academy Dar es salam, Nassoro
Abdallah ,Abdallah Heri wote kutoka United Mtoni,
Nassoro Abdallah mwenye
kusubiri mpira na ,Abdallah Heri ambao ni miongoni mwa nyota wapya wa Miembeni
City waliotokea United Mtoni,
|
Wengine ni Muhamed Jeilani Msuva kutoka
Criss, Ali Bausi kutoka Muembeladu,Feisal Lucas Nado kutoka Chukwani United na Muhamed
Abdallah Banka JKU.
Muhamed Banca nyota mpya wa Miembeni City aliyesajiliwa akitokea JKU. |
Aidha amesema kwa mujibu wa mipango
ya mwalimu kikosi hicho kitacheza michezo minne ya kirafiki yakujieka sawa kwa
ajili ya mfumo mpya wa ligi.
Kocha mkuu wa timu ya Miembeni City Muhamed Seif King akizungumza na wa timu hiyo baada ya amzoezi ya asubuhi. |
Miembeni City ambayo itashiriki ligi
kuu soka ya Zanzibar kwa mara ya kwanza imepania kuona inafanya vyema katika
ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment