Timu ya Simba SC ambao
wapo Visiwani Zanzibar kwaajili ya kuweka kambi hadi Agost 22, 2017, kesho
Alhamis watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Mlandege SC mchezo ambao
utasukumwa majira ya saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Mlandege ambao
wamepanda daraja kutoka la pili wilaya ya mjini hadi la pili taifa ambalo
watacheza msimu ujao kwa sasa imekuwa moja kati ya timu zenye kufanya vyema
katika soka la Zanzibar lengo nikurejesha hadhi ya timu hiyo iliyokuwanayo
katika miaka ya 90.
Huu ni mchezo wa
kwanza kwa timu ya Simba kucheza Visiwani hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo
pia itakuwa ni mchezo wake wa tano wa kirafiki kufuatia kucheza michezo minne.
No comments:
Post a Comment