Saturday, 11 November 2017

WAZIRI RASHID AWATAKA NYOTA ZANZIBAR HEROES KUJITUMA KWA MOYO WAO WOTE.

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Rashid Ali Juma amewataka wachezaji waliopo katika timu ya taifa ya Zanzibar ( Zanzibar Heroes) kujituma kwa moyo wao wote ilikuviletea heshima visiwa vya Zanzibar.

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo Rashid Ali akizungumza na wachezaji wa Zanzibar Heroes hawapo pichani.


Waziri Rashid ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wachezaji wa timu hiyo wakati alipotembelea katika mazoezi ya timu hiyo.

Amesema endapo vijana hao watajituma kwa moyo mmoja kuanzia sasa timu ikiwa katika maandalizi na wakati wa mashindano timu hiyo itatwaa ubingwa wa mashindano hayo.
Baadhi ya wachezaji wakimsikiliza waziri wa habari.

Ameongeza kuwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo na baraza la michezo watatoa ushirikiano wao wa hali na mali ilikuifanya timu hiyo kuwa na maandalizi yakutosha.

Nae katibu wa chama cha mpira wa miguu visiwani hapa Muhamed Ali Hilal Tedy amesema chama chao kimejipanga kuona wanaindaa timu hiyo katika mazingira yaliyo bora.

Amesema changamoto kuu ambayo kwa sasa wanakabiliana nayo nikukosekana kwa baadhi ya wachezaji ambao wanacheza ligi kuu Tanzania bara sambamba na ukata wa fedha.
Waziri wa habari akiwa na mwenyekiti wa baraza la michezo ,rais wa ZFA ,katibu mkuu wa ZFA na mkurugenzi wa ufunzi wa ZFA wakifuatilia mazozei ya timu ya taifa ya Zanzibar asubuhi ya leo.

Aidha amewataka wadau wa soka kuunga mkono juhudi za chama chao ilikufanya maandalizi yakutosha kwa timu hiyo
Timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) inajiandaa na mashindano ya Afrika mashariki na kati yanayotarajiwa kufanyika nchi Kenya mwishoni mwa mwezi huu nchini Kenya..

Friday, 10 November 2017

BUSHIR KUONGEZA NGUVU CHARAWE.

Kufuatia kucheza michezo mitano nakupoteza katika michezo yote  uongozi wa timu ya Charawe imemteua kocha Ali Bushir kukinoa kikosi chao hicho katika michezo iliyosalia.


Hayo yamethibitishwa na katibu wa timu hiyo Haji Bakar wakati alipokuwa akizungumza nasi nakusema wana imani kubwa kocha huyo anaisadia timu yake ifanye vyema.

Amesema kuwa anamatumaini makubwa timu itafanya vyema kufuatia ujio wa kocha huyo ambae amekuwa na uzoefu katika ligi kuu ya Zanzibar.

Ameongeza kuwa kocha huyo amekubali kufanya kazi katika kikosi hicho nakuahidi kutoa mashirikiano ya hali ya juu katika kikosi chao hicho.


Charawe ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza ligi kuu soka ya Zanzibar tayari imeshacheza michezo mitano nakupoteza katika michezo yote mitano.

Thursday, 9 November 2017

KARIHE AONGEZWA ZANZIBAR HEROES.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman (Morocco) amemuongeza kwenye kikosi Mshambuliaji wa Lipuli ya Iringa Seif Rashid Abdallah (Karihe) ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo itakayokwenda Kenya katika Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017.


Katika uteuzi wa awali wa wachezaji 30 Karihe hakuitwa lakini kocha Morocco amelazimika kumuongeza mshambuliaji huyo na atakuwa mchezaji wa 31 kuitwa katika kikosi cha awali huku Morocco akisema si kosa kwa timu ya Taifa kupunguza au kuongeza mchezaji wakati wowote tu ikiwa bado haijaenda katika Mashindano.

“Hii ni timu ya Taifa wakati wowote unamwita mchezaji au unamtoa kutokana na mahitaji yako, nimelazimika kumuongeza Karihe kwasasa ataungana na wenzake 30 wale wa awali”. Alisema Morocco.


Wakati huo huo kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar kimeendelea na mazoezi yake asubuhi ya leo kuendelea namazoezi nyake kujiandaa na mashindano hayo chini ya mwalimu wake Hemed Suleiman Morroco.
Wachezaji waliyoanza mazoezi ni wale ambao vilabu vyao vya Unguja huku ikiwa bado makundi mawili kutoka Kisiwani Pemba na Tanzania Bara bado hawajajumuika na wenzao ambapo wale kutoka Pemba wakitarajiwa kesho kuungana na wenzao.

Wachezaji waliyoanza mazoezi ni Walinda mlango Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Walinzi Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).


Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad Mshamata (Chuoni) pamoja na washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe)
Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Wednesday, 8 November 2017

UKATA WA FEDHA WAPELEKEA KUOTA MBAWA KWA LIGI KUU YA NET BALL ZANZIBAR.

Hatimae ligi kuu ya netball iliyokuwa ifanyike kisiwani Pemba yaota mbawa kutokana na ukata wa fedha unaovikabili vilabu sambamba na chama cha mchezo huo.


Hayo yameelezwa na katibu wa chama cha mchezo huo Said Ali mansab wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu.

Amesema chama chao kimepokea taarifa kutoka kwa wenzao waliopo Pemba kuwa vilabu vya Pemba havitashiriki katika ligi hiyo nakupelekea viongozi kukutana hapo jana kujadili suala hilo nakutafuta njia ya kufanya ilikupatikana muwakilishi wa Zanzibar katika ligi ya Muungano.


Aidha ameongeza kuwa baada yakukutana chama cha netball Zanzibar kimeamua vlabu vya Unguja kushiriki katika kombe la Muungano sambaba na mashindano ya Afrika mashariki na kati yatakayofanyika mwezi wan ne mwakani.

Akivitaja vilabu vitakavyoshiriki katika ligi hiyo ya Muungano katibu huyo amesema ni pamoja na JKU,Mafunzo,Duma ,KVZ,Zimamoto na Afya.

Amewataka wadu wa mchezo huo kuwaunga mkono ilikuimarisha mchezo huo visiwani hapa.

Ligi kuu ya Muungano kwa mchezo wa Net ball inatarajiwa kufanyika kuanzia November 26 mwaka huu katika kiwanja cha Gymkhana.












Sunday, 5 November 2017

MAPINDUZI CUP 2018 KUJUMUISHA TIMU 10,MLANDEGE,SHABA KUSHIRIKI MICHEZO HIYO

Kamati inayosimamia mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup 2018) inaendelea na matayarisho ya michuano hiyo huku timu 10 zinatarajiwa kushiriki msimu huu.

Hayo yameelezwa na katibu wa kamati ya mashindano hayo Khamis Abdallah Said wakati akizungumza na waandishi wa habari nakusema kuwa licha yakupata maombi kutoka kwa timu mbali kuhitaji kushiriki katika mashindano hayo kamati yao imeamua kuwa na timu kumi kutokana na muda.


Ameomgeza kuwa kuna baadhi ya timu zilikuwa tayari kuharamia kila kitu wao wakihitaji kushiriki tu katika mashindano hayo lakini kamati yao imeona muda wakuendesha mashindano hayo hautotosha.

Akizitaja timu amabzo zitashiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Azam ambao ni mabingwa watetezi, Simba na Yanga zote ikiwa nikutoka Tanzania bara huku kisiwa cha Unguja kikiwakilishwa na JKU, Zimamoto, Taifa ya Jang'ombe na Mlandege na kwa upande wa Pemba kikijumuisha timu ya Shaba na Jamhuri na timu moja kutoka nje ya Tanzania bado haijajulikana lakini itatokea Kenya au Uganda.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi mwishoni mwa mwezi Disemba na fainali itapigwa Januari 13, 2018.

Wajumbe wa Kamati wanaosimamia Mashindano hayo Mwenyekiti ni Sharifa Khamis, huku Makamo Mwenyekiti Gulam Rashid, Katibu Khamis Abdalla Said huku Wajumbe wakiwa Issa Mlingoti Ali, Dk. Ally Saleh Mwinyikai,  Ali Khalil Mirza, Khamis Mzee Ali, Ravia Idarous Faina, Ali Mohammed, Mohammed Ali Hilali (Tedy) na Juma Mmanga.

Morroco ataja kikosi cha awali Zanzibar Heroes.

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes),Hemed Suleiman (Morocco) ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa ma Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 hadi Disemba 9, 2017 nchini Kenya.


WALINDA MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe)
Nassor Mrisho (Okapi)
Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU)

WALINZI
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga)
Mohd Othman Mmanga (Polisi)
Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys)
Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar)
Haji Mwinyi Ngwali (Yanga)
Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege)
Issa Haidar "Mwalala" (JKU)
Abdulla Kheir "Sebo" (Azam)
Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe)

VIUNGO
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City)
Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe)
Mudathir Yahya (Singida United)
Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi)
Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar)
Amour Suleiman "Pwina" (JKU)
Mbarouk Marshed (Super Falcon)
Ali Yahya (Academy Spain)
Hamad Mshamata (Chuoni)
Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji)

WASHAMBULIAJI
Kassim Suleiman (Prisons)
Matteo Anton (Yanga)
Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe)
Feisal Salum (JKU)
Salum Songoro (KVZ)
Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys)
Mwalimu Mohd (Jamhuri)
Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto)