Khamis Mussa rais
ameendeleza rekodi yake yakuwafunga mahasimu wao wa jadi ya Taifa Jang’ombe
baada yakuifungia goli pekee la ushindi katika ushindi wa goli 1-0 mtanange
uliovurumishwa katika dimba la Amani mjini Unguja usiku wakuamkia leo.
Katika mchezo huo
ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na kuhudhuriwa na mashabiki lulkuki
uwanjani hapo hadi timu zinaenda mapumziko hakuna timu iliyoona lango la
mwenziwe.
Kurudi uwanjani
kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko na mabadiliko hayo yaliinufaisha
zaidi boys ambao walijiandikia goli hilo mnamo dakika ya 86 kutokana na kazi
nzuri iliyofanya na Khamis Mussa.
Akizungumzia mchezo
huo kocha msaidizi wa timu ya Jang’ombe boys Issa Amasha amesema mtanange huo
ulikuwa nzuri na ushindani kwa pande zote nakuelezea kufurahishwa na ushindi
huo.
Aidha kocha huyo
amesema kuwa tayari timu yao imetinga katika hatua ya nane bora hivyo
maandalizi yao kwa sasa nikuhakikisha timu inafanya vyema katika hatua hiyo
nakutwaa ubingwa wa Zanzibar kwa msimu huu wa ligi.
Nae mwalimu wa timu ya
taifa ya Jang’ombe Saleh Mussa Maisara amesema mchezo huo ulikuwa na ushindani
kwa pande zote mbili lakini kutolewa kwa mchezaji wake kwa kadi nyekundu ndiko
kulikopelekea kupoteza mchezo huo.
Aidha ameongeza kuwa
wanarudi katika mazoezi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo
huo ilikufanya vizuri katika michezo miwili iliyosalia.
![]() |
Kikosi cha timu ya Jang'ombe boys kilichoanza katika mchezo dhidi ya wapinzani wao wa jadi Taifa ya Jang'ombe |
![]() |