Sunday, 14 May 2017

TAIFA YA JANG'OMBE YAKUBALI UTEJA YALAZWA 3-0 NA MAHASIMU WAO.

Magol Hafidh Barik (Fii) dakika ya 67, Khamis Mussa "Rais" dakika ya 74  na Juma Ali "Mess" dakika ya 89 yameifanya Jang’ombe boys kuondoka kiwanja kidedea baada yakuwafungwa mahasimu wao wa jadi timu ya taifa ya jang’ombe.

Khamis Mussa rais mfungaji wa goli la pili .



Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa hali ya juu kwa pande zote huku ukitawaliwa na ubabae wa hapa na pale jambo ambalo lilipelekea muamuzi wa mchezo huo Mfaume Ali Nassor kuwatoa nje kwa kadi nyekundu mshambuliaji wa Jang’ombe boys Rashid Mohd mnamo Dakika ya 24 na na mshambuliaji  Ali Badru wa Taifa mnao dakika ya 26 kutokana na utovu wa nidhamu.

Mashabiki wa taifa ya Jang'ombe

Matokeo hayo inafanya timu ya jang’ombe boys kukaa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na alama tatu sawa na Okapi,Jamhuri na Zimamoto,boys wakiwazidi wapinzani wao kwa uwiano mzr wa magol yakufungwa ambapo tayari wamshatia kambani magol 3 huu katika nyavu zake ikiwa hawajafungwa goli hata mmoja.
Kikosi cah new king

No comments:

Post a Comment