Aliyekuwa
kocha mkuu wa timu ya Mwadui FC Ali Bushir Mahmoud ameelezea sababu
iliyopelekea kuondoshwa kukinoa kikosi hicho.
Akizungumza
na mtandao huo kocha huyo amesema amepokea barua yakumjulisha kuondolewa
kuitumikia kikosi hicho July 27,mwaka huu iliyoandikwa na katibu mkuu wa timu
hiyo.
Amesema kuwa
katika barua hiyo imeelezea sababu kuu tatu ambazo zimemfanya afukuzwe kuinoa
timu hiyo ambazo nikutokuwa na mashirikiano na wachezaji wa timu hiyo,viongozi
pamoja na benchi la ufundi hususani kocha msaidizi wa timu hiyo.
Akielezea
sababu nyengine ni timu kutokushinda mchezo hata mmoja wa ugenini tokea
kuichukua timu hiyo ambapo ilicheza michezo saba ya ugenini nakupoteza huku
michezo saba kati ya nane waliocheza nyumbani wakishinda.
Amesema kuwa
sababu nyengine ambayo imepelekea kuondoshwa katika kikosi chake ni migogoro
iliyopo kati yake na wachezaji wa timu hiyo.
Ameongeza
kuwa sababu ambazo zimeelezwa na uongozi wa timu hiyo haziingii akilini kwa vile
kama utaziangalia kwa undani na namna timu ilivyopata matokeo mazuri.
“ Hizi
sababu kusema ukweli haziingii akilini kwa sababu niliichukua timu ikiwa nafasi
ya tatu kutoka mkiani sasa kama ingekuwa hakuna mashirikiano kati yangu na
wachezaji sambamba na uongozi basi tusingeweza kupata matokeo mazuri
nakuibakisha ligi ikiwa ligi kuu”alisema kocha huyo.
Ameogeza
kuwa kwa sasa anajiandaa kupokea mafao yake kutoka timu hiyo huku akisema kuna
ofa kadhaa ameshazipata kutoka timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya soka
ya Tanzania bara.
Katikati ya msimu uliopita Bushir alichukua mikoba ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kujiunga na
Mwadui FC ambapo aliikuta timu hiyo ipo nafasi ya tatu kutoka chini na kufanya
kazi kubwa mpaka kuisadia kuinusuru kushuka daraja.
No comments:
Post a Comment