Tuesday, 25 April 2017

KIZIMKAZI YAMALIZA LIGI KWA USHINDI

TIMU ya Kizimbani imekamilisha michezo 32 katika ligi kuu ya Zanzibar,
baada ya kuitandika Younger Islander na kufikisha alama 61.

Kizimbani kwa sasa inaongoza ligi hiyo kwa muda, ikiwa mbele kwa alama
moja nyuma ya Jamhuri yenye alama 60 ikiwa na michezo 31 mkononi.
Mcheoz huo uliopigwa katika uwanja wa FFU Finya, huku ukishuhudiwa na
mashabiki wachache kiwanjani hapo, kutokana na timu hizo kumaliza
michezo yake.

Ushindi huo kwa Kizimbani umekuwa mchungu kwa Timu ya Younger Islandrambayo imeshuka hadi nafasi ya 13 katika ligi hiyo na kujihakikishia kushuka daraja.

Magoli ya Kizimbani yamefungwa na Ali Mkadam dakika 21, Mohamed Salim dakika 53 na Rajab Hafidh dakika 60, Younger Islander imefikisha alama 33 baada yakucheza michezo 32.

Kwa upande wa Ligi daraja la kwanza Taifa Pemba, Timu ya Cossovo
imetandika Nuru Boys goli 2-0, magoli ya washindi yamefungwa na Ali
Kheri dakika 21 na Abass Sultan dakika 58.


Timu ya Mkoroshoni na Muungano Ukombozi zimegawana alama 1-1, Uwanjani hapo.

1 comment: