Aliyekuwa kocha
mkuu wa timu ya JKU inayoshiriki
ligi kuu soka ya Zanzibar Muhamed Seif King amesema ameachana na JKU na kwa sasa anaelekeza nguvu
zake zote kuimarisha soka la vijana.
Akizungumza na
zenjsport on line kocha huyo amesema sababu kuu iliyomfanya kuachana na timu hiyonikutokana na kutoelewana nao na kwa sasa ataelekeza nguvu zake
katika kufundisha timu za vijana .
KOCHA MUHAMED SEIF KING ALIEVAA KAPELO AKIWA KATIKA BENCH LA UFUNDI LA JKU KATIKA MOJA YA MICHEZO YA LIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR. |
‘’Unajua
nimefundisha timu nyingi kwa mafanikio lakini sasa nataka kuelekeza nguvu zangu
katika soka la vijana nakuacha soka la ushindani,vijana wengi wanakosoka
misingi imara hivyo nataka nitumie muda wangu uliobakia katika kukuza soka la
vijana nchini ”Alisema kocha King.
Ameongeza
kuwa kujiondoa kwake katika timu ya JKU kutampa nafasi yakuwa na vijana hao kwa muda mrefu jambo ambalo kutamuwezesha yeye katika kuandaa timu za vijana ambazo atakuwa akizifundisha.
Amefafanua kuwa kwa sasa hana mpango hasa wakufundisha timu yoyote ile iliyopo katika ligi za ushindani huku akikanusha uvumi wakuwa yeye anatarajiwa kujiunga na timu ya Mlandege.
"Kwa sasa sitaki timu ya mtu yoyote yule nitaangalia zaidi vijana na lessen yangu ndivyo inavyonielekeza nitatumia muda wote nikiwa na vijana wa wilaya ya mjini na ile timu niliyopewa ilikuifanya iwe imara na ya ushindani"Alisema King.

KOCHA KING AKISALIMIANA NA KOCHA SALUM BAUSI. |
Kuhusu makubaliano
yake na timu hiyo kocha huyo amesema JKU walimchukua kwa majaribio yakumaliza
mechi 12 ambazo tayari zimemalizika na kwa sasa JKU hawamuhitaji kocha huyo.
Ah mizengwe mitupu timu zetu hazijui chema kipi?
ReplyDeleteKila la kheri Kocha King
ReplyDelete