Monday, 31 July 2017

Bushir aeka wazi sababu zilizomfungisha virago Mwadui FC.



Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Mwadui FC Ali Bushir Mahmoud ameelezea sababu iliyopelekea kuondoshwa kukinoa kikosi hicho.
 
Aliyekuwa kocha wa Mwandui FC Ali Bushir Mahmoud.

Akizungumza na mtandao huo kocha huyo amesema amepokea barua yakumjulisha kuondolewa kuitumikia kikosi hicho July 27,mwaka huu iliyoandikwa na katibu mkuu wa timu hiyo.

Amesema kuwa katika barua hiyo imeelezea sababu kuu tatu ambazo zimemfanya afukuzwe kuinoa timu hiyo ambazo nikutokuwa na mashirikiano na wachezaji wa timu hiyo,viongozi pamoja na benchi la ufundi hususani kocha msaidizi wa timu hiyo.

Akielezea sababu nyengine ni timu kutokushinda mchezo hata mmoja wa ugenini tokea kuichukua timu hiyo ambapo ilicheza michezo saba ya ugenini nakupoteza huku michezo saba kati ya nane waliocheza nyumbani wakishinda.

Amesema kuwa sababu nyengine ambayo imepelekea kuondoshwa katika kikosi chake ni migogoro iliyopo kati yake na wachezaji wa timu hiyo.

Ameongeza kuwa sababu ambazo zimeelezwa na uongozi wa timu hiyo haziingii akilini kwa vile kama utaziangalia kwa undani na namna timu ilivyopata matokeo mazuri. 

“ Hizi sababu kusema ukweli haziingii akilini kwa sababu niliichukua timu ikiwa nafasi ya tatu kutoka mkiani sasa kama ingekuwa hakuna mashirikiano kati yangu na wachezaji sambamba na uongozi basi tusingeweza kupata matokeo mazuri nakuibakisha ligi ikiwa ligi kuu”alisema kocha huyo.

Ameogeza kuwa kwa sasa anajiandaa kupokea mafao yake kutoka timu hiyo huku akisema kuna ofa kadhaa ameshazipata kutoka timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya soka ya Tanzania bara.

Katikati ya msimu uliopita Bushir alichukua mikoba ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kujiunga na Mwadui FC ambapo aliikuta timu hiyo ipo nafasi ya tatu kutoka chini na kufanya kazi kubwa mpaka kuisadia kuinusuru kushuka daraja.

Sunday, 30 July 2017

MAAZIMIO YA TIMU YA REAL KIDS FC INAYOSHIRIKI LIGI MADARAJA YA VIJANA BAADA YA ZFA CENTRAL WILAYA YA MJINI KUFANYA VITENDO VYA DHARAU NA KUKIUKA KANUNI NA SHERIA MASHINDANO WALIZOZIWEKA WENYEWE

Ndugu waandishi wa habari…..
Viongozi wa Real Kids wakizungumza na waandishi wa habari.

Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru M/Mungu kwa kutujaalia uzima afya kuweza kukutana hapa leo hii kwa ajili ya kuzungumzia maazimio ya Kamati tendaji ya Timu ya Reak Kids FC kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu.

Uongozi wa Real kids fc ulipokea barua siku ya Jumanne tarehe 25/07/2017 saa 1:00 za usiku yenye Kumbukumbu nambari KMV/CL/WM/VOL-39 naomba kuisoma.

Baada ya kupokea barua hiyo Uongozi wa timu ya Real Kids fc tuliijadili kwa kina na kupinga maamuzi hayo kwa kuandika barua ya kukata rufaa ngazi husika na kumfikia Katibu wa Kamati Central Taifa barua ya tarehe 26/07/2017 yenye kumbukumbu nambari RKFC/26/2017 kabla ya masaa 48 kama inavyoeleza Kanuni kifungu cha 20 ©. “.." naomba kuisoma barua hiyo. Na nakala ya barua hiyo ilimfikia M/Kiti wa ZFA Central Wilaya ya Mjini siku ya Alhamis ya tarehe 27/07/2017 saa 12:06 za jioni.

Kwa vile Timu ya Real Kids fc ilikua imeingia fainali ya ligi ya mtoano tulitegemea kwamba Kamati itasitisha zoezi la utoaji zawadi kwa bingwa ligi ya mtoano daraja la Central mpaka pale rufaa yetu itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Kabla ya kuelezea maazimio yetu naomba kutoa udhaifu wa aliyejipa mamlaka ya kutufuta kwenye mashindano kwa kutumia chuki zisizokua na msingi'

1. M/Kiti wa ZFA Central Wilaya ya Mjini Ndg. Khamis Machano alidiriki kudanganya na kwa kukiuka maamuzi ya kamati yake kwa kuitetea timu ya Mapembeani katika kesi ambayo tayari ilikua imeshatolewa hukumu na kamati yake.

2. Kuwaondosha FC Mwembebeni katika ligi ya mtoano na kuwaachia waendelee kushiriki ligi kwa kuchelewa kwao kulipa ada ya mashindano. ( wakati huo huo Real Kids fc kuondolewa kabisa ligi zote mbili )

3. Kusitisha kuchezwa kwa fainali ligi ya mtooano ambayo ilitakiwa kuchezwa kabla ya mfungo wa mwezi wa ramadhani kwa kusubiria kesi ya Timu ya Mapembeani FC ambayo ilikata rufaa ngazi ya juu kutolewa maamuzi. (Kudharau rufaa ya Real Kids fc)

4. Kufumbia macho mambo ya kishirikina yanayofanywa wazi wazi na baadhi ya timu na kukiuka kifungu cha 26 a(i) na (ii) kinachozungumzia Imani za kishirikina na uchawi.

Baada ya ZFA Central Wilaya ya Mjini kukabidhi zawadi za mshindi wa ligi ya mtoano kwa timu husika, Uongozi wa Real Kids fc ulikaa na kujadili kwa kina kitendo hicho cha ZFA Central Wilaya ya Mjini kwa kuonesha dharau na kukikuka kwa makusudi kanuni na sheria walizozeweka wenyewe. Uongozi umefikia maazimio yafutayo;-

1. Tunalaani vikali hatua ya ZFA Central Wilaya ya Mjini kuendelea kutumia nguvu ya madaraka yake kutoa maamuzi bila kuzingatia sheria na taratibu walizoziweka wenyewe katika kanuni yao ya kuendesha mashindano.

2. Tunaendelea kupinga kile kinachoitwa kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu na kupanga matokeo katika mchezo wetu dhidi ya FC Mwembebeni kama ilivyoelezwa katika barua yao niliyoisoma hapo awali.

3. Tunalaani vikali vyombo vya habari pamoja na magazeti yote yanayoendelea kuchafua jina la timu yetu kupitia kwa kauli za M/Kiti wa ZFA Central Wilaya ya mjini bila ya kuzifatilia, kuzihakiki na kuthibitishwa na pande zote zinazohusika kwa kile wanachodai kua tumefanya kitendo cha utovu wa nidhamu na kupanga matokeo. Kuendelea kutoa habari hizi ni kuenda kinyume na sheria za nchi na Real Kids Fc haitosita kuwafikisha kwa vyombo husika ili kila mwandishi anaendelea kuchafua jina letu kuchukuliwa hatua za kinidhamu kama sheria za nchi zinavyoagiza.

Tunapenda kutoa wito.       

1. Tunawaomba waandishi wa habari pamoja na wahariri wa magazeti kufatilia kwa kina habari zote wanazozikusanya na wasikubali kujaribu kutuma habari kwa kuridhisha upande mmoja bila kujali ukubwa na wadhifa wa mtu husika kwa kufanya hivyo kutaweza kumuweka hatiani kama sheria ya nchi inavyoagiza.

2. Tunaomba Waziri wa wizara husika aliyepewa dhamana ya kusimamia michezo awaangalie vijana kwa jicho la huruma kwani viongozi waliopewa dhamana ya kuwasimamia wanawakandamiza kwa kutumia mwemvuli wa kanuni na kujali maslahi yao binafsi na kusahau dhamna kubwa ya kukuza na kundeleza vipaji vya vijana waliyopewa.

3. Tunamuomba M/Kiti wa Central Wilaya ya Mjini Ndg. Khamis Machano atoke kwenye vyombo vya habari akubali kukiuka kanuni za mashindano kwa kupokea nakala ya rufaa ya timu ya Real Kids fc na kuidharau kwa makusudi na awajibike kisheria kwa kujiuzulu kwa kushindwa kwake kusimamia kanuni na sheria za mashindano walizozipanga wenyewe.

4. Tunaiomba kamati husika inayochagua viongozi wa madaraja ya vijana kuweka sheria ya kuwachagua viongozi wanaotuongoza kwa kuwapigia kura ambayo watashirikishwa viongozi wa vilabu vyote husika kwani kufanya hivyo kunaweza ndio kutaweza kuleta viongozi imara wenye kuwatumikia vijana wetu.

Mwisho napenda nichukue fursa kuwaomba wadau wetu wa real kids fc kutulia na kuendelea kutuunga mkono sambamba na kupuuza kile kinachodaiwa kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu na kupanga matokeo, Ungozi wa Timu ya Real Kids fc upo imara na hauwezi kuyumbishwa na kauli hizo za kuchafuliwa kwa jina letu.

Ahsanteni kwa kunisikiliza….

IMETOLEWA NA
KAMATI TENDAJI
REAL KIDS FC
30/07/2017

Mwenyekiti Cetral wilaya ya mjini aachie ngazi kwa kukeuka kanunu ya mashindano ya vijana,,Real Kids.

Kamati tendaji ya timu ya Real Kids FC inayoshiriki ligi madaraja ya vijana central league wilaya ya mjini imemtaka mwenyekiti wa kamati inayosimamia mashindano ya vijana Khamis Machano kuachia nafasi hiyo baada yakukeua kanuni inayoendesha mashindano hayo.
Viongozi wa  Real Kids FC wakizungumza na waandishi wa habari.

Hayo yameelezwa na msemaji wa timu hiyo Tarik Khamis Ali wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nakusema kuwa kitendo cha ukeukwaji wa kanuni uliofanywa na mwenyekiti huyo akishirikiana na wajumbe wa kamati yake nikurudisha nyuma juhudi za vijana waliojitolea kuimarisha vipaji vya vijana wenzao.

Amesema timu yao ilituma rufaa kwa mujibu wa kanuni inayoendesha mashindano hayo lakini mwenyekiti huyo ameshindwa kusitisha utoaji wa zawadi kwa upande wa ligi ya mtoano  century league ambayo timu ya Real Kids kupisha kusikilizwa kwa rufaa yao.

Amesema kuwa kamati ya century imekaa kutoa maamuzi bila yakuwasikiliza jambo ambalo nikinyume na taratiabu lakini jambo lakusikitisha zaidi kamati hiyo imeshindwa kuheshimu rufaa yao waliyoikata kwa kamati ya mashindano ya vijana taifa na nakala yake kupeleka kwa kamati yake lakini wakashindwa kueheshimu rufaa hiyo jambo amablo linaashirikia kushindwa kuiheshimu kanuni ya mashindano kama ilivyoorodheswa katika kifungu cha 20 C.

Ameelezea kusikitishwa kwake nakuchafuliwa kwa timu yao kwa madai yakupanga matokeo jambo ambalo si sahihi kwani hakuna ushahidi wowote ule unaoashiria vitendo vya upangaji wa matokeo.

 Amewaomba waandishi wa habari kuacha kuichafua timu yao kwa kuchukua taarifa za upande mmoja na badala yake wasikilize maelekezo kwa pande zote mbili ilikutoa taarifa iliyo sahihi.


Saturday, 29 July 2017

Central mjini yamaliza kwa mafanikio.

Mashindano ya vijana ndani ya wilaya ya mjini yamefikia tamati jana ambapo mabingwa katika madaraja mbalimbali walikabidhiwa zawadi zao.

Akizungumza na mtandao huu mara baada yakumalizika kwa mashindano hayo mwenyekiti wa kamati ya amshindabo hayo Khamis Machano amesema mashindabo hayo yamekwenda vyema licha ya changamoto kadhaa mabazo zinawakabili katika kuendesha michezo hiyo.

Akielezea changamoto ambazo wanakabilina nazo katika uendeshaji wa michezo hiyo mwenyekiti huyo amesema uhaba wa fedha imekuwa changamoto kubwa ambayo wanakabiliana nayo katika kuendesha mashindano hayo sambamba na idadi ndogo ya wajumbe wanaosimamia mashindano hayo ukilinganisha na timu ambazo zinashiriki katika michezo hiyo.

Akizungumzia suala zima la zawadi mwenyekiti huyo amesema mashindano ya mwaka huu zawadi ya fedha imepungua ukilinganisha na mwaka jana kutokana na shughuli mbalimbali ambazo kamati yao iliziendesha katika kipindi cha msimu uliomalizika jana.

“Unajua zawadi ya fedha imepungua ukilinganisha na mwaka jana kutoka na shughuli mbali mbali ambazo kamati iliendesha ,msimu huu tuliendesha kozi ya ukocha na kamati ndio iliyogharamia kwa asilimia kubwa kozi hiyo pia kamati ilichangia kwa asilimia kubwa timu ya vijana iliyoenda Manyara katika mashindano ya Rolling stone jambo ambalo limepelekea kamati kupunguza zawadi ya fedha ukilinganisha na mwaka jana”alisema.

Akizungumza vitendo vya upangaji matokeo uliojitokeza katika mashindano ya mwaka huu mwenyekiti huyo ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo hivyo huku akiwaomba wanaosimamia timu za vijana kuachana na vitendo kama hivyo kwani kunarejsha nyuma maendeleo ya soka la vijana.

Mabingwa katika madaraja mbalimbali kwa wilaya ya mjini ni kama ifuatavyo ,Junvinile mabingwa Gold win huku makamo bingwa wakiwa Blacksaloir,Juniour bingwa Tothham makamo bingwa Simba FC,mashindano ya mtoanao Juvinile bingwa Blacksaloir huku makamo bingwa akiwa New academy.


Kwa upande wa mashindano ya mtoano central  bingwa ni Villa coast na kwa upande wa mashindano ya mtoano Juniour bingwa ni Al-noour.

NIDHAMU NI SILAHA PEKEE MICHEZONI,,WAZIRI

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Rshid Ally Juma amewataka wachezaji wa combine ya wialaya ya mjini kuongeza bidii ilikuimarisha vipaji walivyobarikiwa na muumba.
Waziri wa habari utamaduni ,utalii na michezo Rashid Ally Juma akizungmza na wachezaji wa timu ya combine ya wilaya ya mjini.
Waziri Rashid ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo huko ofisini kwake waliponda kupeleka kombe waliotwaa katika mashindano ya Rolling stone yaliyofanyika Mbuu Manyara .
Wachezaji wa combine ya wilaya ya mjini na viongozi wao wakimsikiliza waziri.

Aidha amewapongeza vijana hao kwa ujasiri wa waliouonesha katika mashindano hayo licha ya changamoto kadhaa walizokabiliana nazo wakiwa katika mashindano hayo.
Ameongeza kuwa vijana hao walionesha nidhamu ya hali juu na ndo jambo pekee lililowasaidia kuweza kutwaa Ubingwa huo.
 
Kocha mkuu wa mabingwa wa mashindano ya Rolling stone combine ya wilaya ya mjini Muhamed Seif King,mjumbe wa kamati tetandaji ZFA wilaya ya mjini Kisike wakati kati na kocha msaidizi wa timu hiyo Ramadhani Madundo wakimsikiliza waziri wa habari,utamaduni,utalii na michezo.

Mapema mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wialaya ya mjini Unguja Hassan Haji Hamza ameiomba serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kutoa michango yao ya hali na mali pindi timu itakapokuwa na amshindano nje ya Zanzibar ilikuondoa changamoto ambazo hujitokeza.

Friday, 28 July 2017

KIPA ZANTEX ASAINI MIAKA MIWILI MIEMBENI CITY



Timu ya Miembeni City imekamilisha usajili wa mlinda mlango nambari moja wa timu ya Zantex ,Ally Rajab ambae amesaini kandarasi ya miaka miwili na timu hiyo.
 
Ally Rajab akisaini kandarasi ya miaka miwili na Miembeni City huku akishuhudiwa na aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi wa timu Ali Muhamed.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa habari wa timu hiyo Ali Khamis imesema usajili huo unaifanya timu hiyo iwe na walinda milango watatu ambao ni Aley Ali Suleiman,Abaas Wadi Makame na Ali Rajab alikuja kuongeza nguvu katika eneo hilo. 


Ali Rajab anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Miembeni City katika kipindi hichi cha usajili ambapo wiki iliyopita walimsajili mshambuliji ya Faisal Riam Lucas (Nado) ambae amesaini kandarasi ya miaka mitatu.

PEMBA DABI,JAMHURI ,MWENGE HAPOTOSHI GOMBANI JIONI YA LEO.



Ligi kuu soka ya Zanzibar inaendelea jioni ya leo ambapo michezo miwili inatarajiwa kusukumwa katika viwanja viwili tofauti.
 
KIKOSI CHA TIMU YA JAMHURI.
Katika kiwanja cha Amani mjini Unguja vinara wa ligi hiyo JKU inaoneshana kazi na timu ya Zimamoto, huku katika kiwanja cha Gombani kisiwani Pemba Mwenge itamenyana na Jamhuri.
 
Baadhi ya washabiki wanaofuatilia michezo ya ligi kuu soka ya Zanzibar inayoendelea visiwani hapa.
Kesho ligi hiyo mitamaliza mzunguko wake wa tisa kwa michezo miwili katika dimba la Amani kutakuwa na dabi ya Jang’ombe pale Jang’ombe boys itakapomenyana na taifa ya Jang’ombe huku katika kiwanja cha Gombani kisiwani Pemba Okapi itakipiga na Kizimbani.
Wachezaji wa Zimamoto wakipongezana katika moja ya michezo ya ligi kuu soka ya  Zanzibar.

Wednesday, 26 July 2017

NYOTA GULION FC ASAINI MIAKA MIWILI STAND UNITED.

Mlinzi wa kati wa timu ya Gulion FC Ali Hamad Ali inayoshiriki ligi daraja la pili wilaya ya mjini Unguja amesajili miaka mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu ya Stand United ya Tanzania bara.
Ali Hamad Ali akizungumza na waandishi wa habari.

Akizungumza na mtandao huu nyota huyo ameelezea kufurahishwa kwake nakusajiliwa na timu hiyo huku akisema kuwa hiyo itakuwa safari yake yakuanzia kucheza soka lakulipwa.

Amesema kuwa atahakikisha anajituma kwa hali na mali kuhakikisha anakiimarisha kiwango chake ulikufanikisha malengo yake.


Ali Hamad Ali ameanza soka lake katika timu ya Vikokotoni tokea madaraja ya vijana kabla yakujiunga timu ya Gulion akiwa nahodha wa timu hiyo.

Tuesday, 25 July 2017

Fii akosa penalt ,boys yalala kwa fire.

Timu ya Zimamoto imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jang’ombe Boys katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora uliosukumwa jioni ya leo katika uwanja wa Amaan.
Mchezaji wa Jang'ombe Boys Fii akijiandaa kupiga Penalt.

Goli la Zimamoto lilifungwa na Idrissa Simai Pandu dakika ya 84.
Katika mchezo huo mlinzi wa kati wa Jang'ombe boys Ali Humud Badri (Balii) alitolewa nje kwa kadi njekundu baada yakuunawa kwa makusudi mpira uliokuwa ukimpita.
Wachezaji wa timu ya Zimamoto wakilalamikia maamuzi ya muamuzi Haule.

Mchezo mwengine umepigwa katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba timu ya Jamhuri ikaenda sare ya 1-1 dhidi ya Okapi.
Kocha wa timu ya Jang'ombe boys Muhamed akisalimiana na Fii.

Bao la Okapi limefungwa na Bakar Hamad dakika ya 5 wakati bao la Jamhuri limefungwa na Ahmed Ali Omar dakika ya 20.

PICHA TOFAUTI JANG'OMBE BOYS VS FIRE