Sunday, 29 October 2017

NYOTA REAL KIDS FC,WAPIMWA AFYA ZAO ,TAYARI KWA MICHEZO YA VIJANA YALIYOFUNGULIWA JUMAMOS OCTOBER 28.

Katika kuhakikisha wanaepusha matatizo ya kiafya kwa wachezaji wao wawapo uwanjani uongozi wa timu ya  Realkdis Fc inayoshiriki ligi madaraja ya vijana nadani ya wilaya ya ya mjini Unguja imewafanyia vipimo vya afya nyota wao ilikujua matatizo yanayowakabili nyota hao.

Akizungumza nasi katibu wa timu hiyo Nassor Abdaallah amesema lengo kuu lakufanya hivyo nikujua afya za nyota wa sambamba na kuepusha matatizo ambayo yanaweza kujitokeza kwa wachezaji ambao kwa mujibu wa afya zao hawastahiki kucheza mpira.

Aidha ameishukuru timu ya maktari ambayo imefanya kazi hiyo kwa kushirikia na uongozi wa timu hiyo nakusema zoezi hilo la upimaji afya kwa wachezaji wao litakuwa likifanya kila muda ilikulinda afya za wachezaji wao nakuwataka wachezaji wa timu hiyo kufuata ushauri waliopewa na madaktar baada yakupima afya.


"Tunawashukuru timu ya madaktari kwa kushirikiana na uongozi kuhakikisha kuwa zoezi hili la upimaji wa afya limekwenda vizuri na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kugundua baadhi ya matatizo yanayowakabili vijana wetu sambamba na kuwapa elimu ya afya jinsi ya kulinda afya ya miili yao haswa misuli kwa kufanya mazoez kwa bidii na njia iliyo sahihi ili iwasaidie kufanya vizuri katika mechi zao za kila siku” alisema.


Vipimo ambavyo walifanyiwa nyota hao ni pamoja na vipimo vya damu kama vile blood group, blood glucose, blood pressure,Afya ya masikio, uoni wa macho, misuli pamoja na joints.

Saturday, 28 October 2017

Wilaya ya mjini yazindua mashindano ya vijana ,Chura awataka makocha kuacha tabia za uzalilishaji kwa vijana.

Mashindano ya vijana Central league wilaya ya mjini Unguja yamezinduliwa rasmini asubuhi ya leo katika kiwanja cha Amani mjini Unguja kwa mchezo kati ya timu ya Aman Academy na timu ya Mpira Pesa.
Rais wa Raska zone Ali Mkanga akisalimiana na muamuzi wa mchezo kati ya timu ya Amani Academy na Mpira Pesa Abubakary Khatibu mchezo ambao umemalizika kwa sare yakufungana goli 1-1.


Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani kwa pande zote timu hizo zimetoka sare yakufungana goli 1-1.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya mjini Unguja Hassan Haji Hamza amemewataka walimu wanaofundisha soka la vijana kuachana na vitendo vya unyanyanyasaji watoto sambamba na kuwaingilia kinyume na maumbile.
Viongozi wa kamati ya mashindano ya vijana wilaya ya mjini wakiwa katika picha ya pamoja  na mgeni rasmini katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo Ali Mkanga.

Amesema kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi kwa baadhi ya makocha kushiriki katika vitendo hivyo jambo ambalo linahitajika kupingwa kwa nguvu zote.

Amesema endapo chama chao kitapata uhakika wa tuhuma hizo hatua kali watamchukulia muhusika huku akilitaka jeshi la polisi visiwani kufuatilia kwa umakini mkubwa tuhuma hizi ili kama zipo ziwezekupatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake rais wa Raska zone Ali Mkanga amewataka vijana kujituma katika michezo kwani michezo ni ajira.

Thursday, 26 October 2017

ZFA yaridhishwa na maendeleo ya soka la wanawake visiwani.

Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kimeelezea kuridhishwa kwake na hamasa  uliojitokeza kwa timu za wanawake zinazoshiriki ligi dogo ya kinamama inayoendelea katika kiwanja cha Amani mjini Unguja ambapo lengo nikutafuta wachezaji 20 watakaounda timu ya taifa ya wanawake itakayoshiriki katika mashindano ya kina mama kule nchini Rwanda.

Akizungumza na mtandao huu katibu wa chama cha mpira wa miguu Zanzibar Muhamed Ali Hilal Tedy amesema michezo hiyo inayoendelea visiwani hapa tayari makocha waliopewa jukumu lakutafuta wachezaji wanaendelea kufanya kazi hiyo.

Ameongeza kuwa katika michezo iliyochezwa vijana kadhaa wameonesha viwango vya hali ya juu na kinachosubiriwa kwa sasa ni makocha waliopewa jukumu kumaliza kazi yao nakutangazwa watakaobahatika kuitwa katika timu ya taifa ya wanawake.


Ameongeza kuwa tayari chama chao kimepokea majina ya wachezaji watano kutoka Pemba ambao wataungana na 15 kutoka Unguja kutangazwa kikosi kamili.


Ameongeza kuwa mara baada yakutangazwa kwa kikosi hicho kocha aliepewa dhama yakukinoa kikosi hicho ataanza majukumu yakukiandaa kikosi kabla yakuondoka kuelekea katika mashindano ya Afrika mashariki na kati kwa upande wa kina mama yanayotarajiwa kufanyika Rwanda mapema mwezi ujao.

Wednesday, 25 October 2017

Simba yazidi kuitafutia kasi Yanga na mvua yao.

Wekundu wa msimbazi Simba wanaendelea kujinoa visiwani Zanzibar kwa ajili yakujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya mahasimu wao Yanga mchezo ambao utavurumishwa Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.


Simba ambao wapo visiwani wanafanya mazoezi yakujiandaa na mchezo huo katika kiwanja cha Amani kwa wakati wa asubuhi na katika dimba la jeshini jioni kwa baadhi ya siku.

Ikiwa simba ikiendelea na mzoezi yakujiandaa na mahasimu wao Yanga mshambuliji wachezaji wao waliokuwa majeruhi mshambuliaji John Bocco na kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim wameonekana wakifanya mazoezi ya nyota wenzao kuashirikia kuwa tayari kuikabilia Yanga.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa habari wa timu hiyo wekundu hao wa msimbazi wanatarajiwakuondoka visiwani hapa Jumamosi asubuhi kuelekea Tanzania bara kwa mchezo huo.

Mzunguko wa nne ligi kuu soka Zanzibar kituo cha Unguja kuanza kesho,Miembeni City kuwakaribisha Chuoni FC.

Baada yakuenda mapumzikoni kwa takribani siku mbili ligi kuu soka ya Zanzibar kituo cha Unguja inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho kwa kuanza michezo ya mzunguko wa nne.

Ambapo hapo kesho mtanange mmoja utavurumishwa katika kiwanja cha Amani mjini Unguja mnamo majira ya saa kumi alasiri ambapo timu ya Chuoni itajitupa katika kiwanja cha Amani kuoneshana kazi na timu ya Miembeni City.

Chuoni inashuka katika kiwanja cha Amani mjini hapa wakiwa na alama 4 huku Miembeni City wenyewe wakijitupa katika mchezo huo wakiwa na rekodi mbaya yakupoteza michezo mitatu mfululizo.

Michezo mengine ya mzunguko huo wa nne ya ligi kuu soka ya Zanzibar inaendelea kesho kutwa Jumamos ambapo mitanange miwili itavurumishwa mnamo majira ya saa nane mchana Taifa ya Jang’ombe itakipiga na JKU  huku mnamo majira ya saa kumi alasiri KVZ inamenyana na Mafunzo.

Ikiwa ligi hiyo inaingia mzunguko wa 4 jioni ya kesho mpaka sasa timu ya KVZ inaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 9 wakifuatiwa na JKU wenye alama tisa tofauti yao ikiwa ni magol yakufungwa nanakufunga.

Ratiba kamili ya michezo ya mzunguko 

IJUMAA
27/10/017
22
MIEMBENI CITY
VS
CHUONI
SAA 10:00 ALS AMAAN
J’MOSI
28/10/017
23
TAIFA YA J/MBE
VS
JKU
SAA 8:00 MCH AMAAN
J’MOSI
28/10/017
24
KVZ
VS
MAFUNZO
SAA 10:00 ALS AMAAN
J’PILI
29/10/017
25
KIPANGA
VS
POLISI
SAA 8:00 MCH AMAAN
J’PILI
29/10/017
26
KMKM
VS
ZIMAMOTO
SAA 10:00 ALS AMAAN
J’TATU
30/10/017
27
BLACK SAILORS
VS
CHARAWE
SAA 8:00 MCH AMAAN
J’TATU
30/10/017
28
JANG’OMBE BOYS
VS
KILIMANI CITY
SAA 10:00 ALS AMAAN

Sunday, 22 October 2017

Jumbi women fighter,New Generation hakuna mbabe.

Timu ya Jumbi women fighter na timu ya New Generation zimetoka suluhu yakutokufungana katika mchezo wa awali wa ligi kuu soka ya wanawake mchezo uliochezwa katika kiwanja cha Amani mjini Unguja asubuhi ya leo.



Katika mchezo huo ambapo ulikuwa na ushindani wa hali ya juu kwa timu zote mbili nakushuhudiwa na washabiki kadhaa uwanjani hapo hadi dakika tisini zinamalizika hakuna timu iliyoona lango la mweziwe.

katika mchezo ulichezwa mnamo majira ya saa nne asubuhi green quen ikakipiga na timu ya Women fighter.


Saturday, 21 October 2017

Imani yangu vijana watafanya kazi nakupata matokeo mazuri mbeleni,kocha Miembeni City.

Licha yakupokea kipigo cha tatu mfululizo kocha mkuu wa timu ya Miembeni City asema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na vijana wake katika mchezo dhidi ya JKU.
 
Kikosi cha Miembeni City kilichoanza katika mchezo wa jana na JKU.
Akizungumza na mtandao huu mara baada ya mchezo wa timu hiyo na JKU kocha wa timu hiyo Muhamed Seif King amesema ameona mabadiliko makubwa katika kikosi chake katika kila mchezo na anamatumaini makubwa yakufanya vyema katika michezo ijayo.

Ameongeza kuwa kikosi chake ni kigeni katika ligi lakini pia kinaunda na vijana ambao ni wanagenzi lakini katika kila mchezo wameonekana wakibalika jambo ambalo yeye kama mwalimu linampa matumaini na anaamini watafanya vyema katika michezo ya mbeleni.

Miembeni City ambayo tayari imeshashuka dimbani mara tatu nakupoteza katika michezo yote mitatu ambapo walifungwa na Polis gol 1-0,kisha mafunzo 1-0 na jana kukubali kipigo cha idadi kama hiyo cha goli 1-0 kutoka kwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo JKU.






Tuesday, 10 October 2017

ZFA YARIZISHWA NA MICHEZO YA MZUNGUKO WA KWANZA LIGI KUU SOKA ,ZANZIBAR.

Michezo ya mzunguko wa kwanza ligi kuu soka ya Zanzibar sambamba na ligi daraja la kwanza taifa Unguja imeenda vizuri huku ushindani ukionekana wa hali juu ka timu shiriki.

Hayo yameelezwa na katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar Muhamed Hilal Tedy wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema kuwa ushindani ulioneshwa na timu husika unaashiria maandalizi mzuri kwa timu hizo.

Ameongeza kuwa chama chao kitasimamia kanuni na sheria zakuenda mashindano hayo ikiwemo lessen kwa walimu wanaofundisha timu shiriki ambapo kanuni inahitaji mwalimu kuanzia lessen B.

Akizungumzia timu ambazo hazijafata kanuni na sheria ya mashindano hayo katibu huyo amesema chama chao kinajipanga kuwapatia adhabu kwa mujibu wa sheria na kanuni.

Kuhusu suala la waamuzi ambao wamechezesha michezo hiyo nakulalamikiwa katibu huyo amesema tayari chama chao kimeshafanya mazungumzo na viongozi wa waamuzi hao kuhusu suala hilo.

Aidha amewataka wadau na wapenda mchezo wa soka kujitoka kwa wengi viwanjani ilikuunga mkono timu zao.


Ligi kuu soka ya Zanzibar inatarajiwa kuendelea October 15 ,ambapo michezo miwili itavurumishwa siku hiyo mnamo majira ya saa 8 mchana JKU itakipiga na timu ya Chuoni huku mnamo majira ya saa kumi alasiri Miembeni City itakipiga na Mafunzo.

Monday, 9 October 2017

KWEREKWE CITY MAUNGANI ,WATAMBIANA.

Ligi daraja la pili taifa Unguja inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake jioni ya leo ambapo michezo minne ya inatarajiwa kuvurumishwa katika viwanja vine tofauti.

Katika kiwanja cha Ngome Fuoni Zantex itakipiga na Bweleo ,huku katika kiwanja cha Tazari New King itaikaribisha New book.

Sungusungu BZL itaoneshana kazi na Mchangani na katika kiwanja cha Maungani Maungani itakipiga na Kwerekwe City.

 Michezo hiyo itavurumishwa mnamo majira ya saa kumi alasiri

Wednesday, 4 October 2017

Nyota Zanzibar heroes ,taifa star afariki dunia.

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar heroes) sambamba na timu ya taifa ya Tanzania Abdumajham amefariki dunia baada yakusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Marehem Abdulmajiham aliekamapata mkongojo enzi za uhai wake.

Nyota huyo ambae ametamba akiwa na timu ya Vikokoni na Cosmos amefariki dunia mnamo majira ya saa moja usiku wa leo.
Nyota huyo anatarajiwa kuzikwa hapo kesho.

Mweneyezi amjalie kauli thabit na amjalia awe miongoni mwa waja wema. Amin.


Endelea kufuatilia mtandao huu ilikujua historia ya nyota .

RATIBA YA LIGI DARAJA LA PILI TAIFA UNGUJA KUNDI A

SIKU
TAREHE
M
 HOME TEAM
VS
AWAY TEAM
VENUE & TIME
1ST ROUND
J’TATU
09/10/017
1
UMEME
VS
SUPER STAR
SAA 10:00 BUNGI
J’TATU
09/10/017
2
SHARP BOYS
VS
MPAPA
SAA 10:00 NEW STAR
J’TATU
09/10/017
3
RASKAZONI
VS
ALUTA
SAA 10:00 WIMBI
J’TATU
09/10/017
4
SHANGANI
VS
MTONI UNITED
SAA 10:00 CHUONI CHUKWANI
2ND ROUND
J’PILI
15/10/017
5
MTONI UNITED
VS
UMEME
SAA 10:00 MWAKAJE
J’PILI
15/10/017
6
ALUTA
VS
SHANGANI
SAA 10:00 MIDIMNI
J’PILI
15/10/017
7
MPAPA
VS
RASKAZONI
SAA 10:00 UZINI
J’PILI
15/10/017
8
UHAMIAJI
VS
SHARP BOYS
SAA 10:00 FUONI
3RD ROUND
J’MOSI
21/10/017
9
UMEME
VS
ALUTA
SAA 10:00 BUNGI
J’MOSI
21/10/017
10
SUPER STAR
VS
MTONI UNITED
SAA 10:00 P/MCHANGANI
J’MOSI
21/10/017
11
RASKAZONI
VS
UHAMIAJI
SAA 10:00 WIMBI
J’MOSI
21/10/017
12
SHANGANI
VS
MPAPA
SAA 10:00 CHUONI CHUKWANI
4TH ROUND
IJUMAA
27/10/017
13
ALUTA
VS
SUPER STAR
SAA 10:00 MIDIMNI
IJUMAA
27/10/017
14
MPAPA
VS
UMEME
SAA 10:00 UZINI
IJUMAA
27/10/017
15
UHAMIAJI
VS
SHANGANI
SAA 10:00 FUONI
IJUMAA
27/10/017
16
SHARP BOYS
VS
RASKAZONI
SAA 10:00 NEW STAR
5TH ROUND
AL’MIS
02/11/017
17
UMEME
VS
UHAMIAJI
SAA 10:00 BUNGI
AL’MIS
02/11/017
18
SUPER STAR
VS
MPAPA
SAA 10:00 P/MCHANGANI
AL’MIS
02/11/017
19
MTONI UNITED
VS
ALUTA
SAA 10:00 MWAKAJE
AL’MIS
02/11/017
20
SHANGANI
VS
SHARP BOYS
SAA 10:00 CHUONI CHUKWANI
6TH ROUND
AL’MIS
09/11/017
21
MPAPA
VS
MTONI UNITED
SAA 10:00 UZINI
AL’MIS
09/11/017
22
UHAMIAJI
VS
SUPER STAR
SAA 10:00 FUONI
AL’MIS
09/11/017
23
SHARP BOYS
VS
UMEME
SAA 10:00 NEW STAR
AL’MIS
09/11/017
24
RASKAZONI
VS
SHANGANI
SAA 10:00 WIMBI
7TH ROUND
J’TANO
15/11/017
25
UMEME
VS
RASKAZONI
SAA 10:00 BUNGI
J’TANO
15/11/017
26
SUPER STAR
VS
SHARP BOYS
SAA 10:00 P/MCHANGANI
J’TANO
15/11/017
27
MTONI UNITED
VS
UHAMIAJI
SAA 10:00 MWAKAJE
J’TANO
15/11/017
28
ALUTA
VS
MPAPA
SAA 10:00 MIDIMNI
8TH ROUND
AL’MIS
23/11/017
29
UHAMIAJI
VS
ALUTA
SAA 10:00 FUONI
AL’MIS
23/11/017
30
SHARP BOYS
VS
MTONI UNITED
SAA 10:00 NEW STAR
AL’MIS
23/11/017
31
RASKAZONI
VS
SUPER STAR
SAA 10:00 WIMBI
AL’MIS
23/11/017
32
SHANGANI
VS
UMEME
SAA 10:00 CHUONI CHUKWANI
9TH ROUND
J’TANO
29/11/017
33
SUPER STAR
VS
SHANGANI
SAA 10:00 P/MCHANGANI
J’TANO
29/11/017
34
MTONI UNITED
VS
RASKAZONI
SAA 10:00 MWAKAJE
J’TANO
29/11/017
35
ALUTA
VS
SHARP BOYS
SAA 10:00 MIDIMNI
J’TANO
29/11/017
36
MPAPA
VS
UHAMIAJI
SAA 10:00 UZINI