Saturday, 10 February 2018

HILIKA AANZA NA GOLI CONGO

KIKOSI CHA TIMU YA FC BUKAVU YA CONGO AMBAYO KWA SASA ANACHEZEA NYOTA WA ZANZIBAR HEROES IBRAHIM AHMADA HILIKA SAMBAMBA NA NYOTA MWENZAKE SULEIMAN KASSIM SELEMBE.
MSHAMBULIAJI MPYA FC BUKAVU IBRAHIM HAMAD HILIKA WAPILI AKIWA KATIKA MAZOEZI NA TIMU YAKE HIYO MPYA.
SULEIMAN KASSIM SELEMBE ALIEVAA JEZI NAMBA 8 AKIWA NA ZANZIBAR MWENZAKE IBRAHIM HAMAD HILIKA ALIEVAA JEZI NAMBA 21 WAKIWA NA TIMU YAO MPYA FC BUKAVU.

Wednesday, 13 December 2017

JKU YAPEWA ZESCO, ZIMAMOTO NA WAHABESH



TIMU ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar itaanza na Zesco United ya Zambia katika Raundi ya Awali ya ligi ya mabingwa Afrika. 


JKU SC wataanzia nyumbani Uwanja wa Amaan, Zanzibar kabla ya kusafiri hadi Ndola kwa mchezo wa marudiano.

Katika droo iliyofanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu 59 zimepangwa katika Ligi ya Mabingwa na 54 zimo katika Kombe la Shirikisho.

Mashirikisho ya nchi nane tu hayajawasilisha wawakilishi ambayo ni ya Cape Verde, Chad, Eritrea, Namibia, Reunion, Sao Tome and Principe, Sierra Leone na Somalia.

Saturday, 11 November 2017

WAZIRI RASHID AWATAKA NYOTA ZANZIBAR HEROES KUJITUMA KWA MOYO WAO WOTE.

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Rashid Ali Juma amewataka wachezaji waliopo katika timu ya taifa ya Zanzibar ( Zanzibar Heroes) kujituma kwa moyo wao wote ilikuviletea heshima visiwa vya Zanzibar.

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo Rashid Ali akizungumza na wachezaji wa Zanzibar Heroes hawapo pichani.


Waziri Rashid ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wachezaji wa timu hiyo wakati alipotembelea katika mazoezi ya timu hiyo.

Amesema endapo vijana hao watajituma kwa moyo mmoja kuanzia sasa timu ikiwa katika maandalizi na wakati wa mashindano timu hiyo itatwaa ubingwa wa mashindano hayo.
Baadhi ya wachezaji wakimsikiliza waziri wa habari.

Ameongeza kuwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo na baraza la michezo watatoa ushirikiano wao wa hali na mali ilikuifanya timu hiyo kuwa na maandalizi yakutosha.

Nae katibu wa chama cha mpira wa miguu visiwani hapa Muhamed Ali Hilal Tedy amesema chama chao kimejipanga kuona wanaindaa timu hiyo katika mazingira yaliyo bora.

Amesema changamoto kuu ambayo kwa sasa wanakabiliana nayo nikukosekana kwa baadhi ya wachezaji ambao wanacheza ligi kuu Tanzania bara sambamba na ukata wa fedha.
Waziri wa habari akiwa na mwenyekiti wa baraza la michezo ,rais wa ZFA ,katibu mkuu wa ZFA na mkurugenzi wa ufunzi wa ZFA wakifuatilia mazozei ya timu ya taifa ya Zanzibar asubuhi ya leo.

Aidha amewataka wadau wa soka kuunga mkono juhudi za chama chao ilikufanya maandalizi yakutosha kwa timu hiyo
Timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) inajiandaa na mashindano ya Afrika mashariki na kati yanayotarajiwa kufanyika nchi Kenya mwishoni mwa mwezi huu nchini Kenya..

Friday, 10 November 2017

BUSHIR KUONGEZA NGUVU CHARAWE.

Kufuatia kucheza michezo mitano nakupoteza katika michezo yote  uongozi wa timu ya Charawe imemteua kocha Ali Bushir kukinoa kikosi chao hicho katika michezo iliyosalia.


Hayo yamethibitishwa na katibu wa timu hiyo Haji Bakar wakati alipokuwa akizungumza nasi nakusema wana imani kubwa kocha huyo anaisadia timu yake ifanye vyema.

Amesema kuwa anamatumaini makubwa timu itafanya vyema kufuatia ujio wa kocha huyo ambae amekuwa na uzoefu katika ligi kuu ya Zanzibar.

Ameongeza kuwa kocha huyo amekubali kufanya kazi katika kikosi hicho nakuahidi kutoa mashirikiano ya hali ya juu katika kikosi chao hicho.


Charawe ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza ligi kuu soka ya Zanzibar tayari imeshacheza michezo mitano nakupoteza katika michezo yote mitano.

Thursday, 9 November 2017

KARIHE AONGEZWA ZANZIBAR HEROES.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman (Morocco) amemuongeza kwenye kikosi Mshambuliaji wa Lipuli ya Iringa Seif Rashid Abdallah (Karihe) ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo itakayokwenda Kenya katika Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017.


Katika uteuzi wa awali wa wachezaji 30 Karihe hakuitwa lakini kocha Morocco amelazimika kumuongeza mshambuliaji huyo na atakuwa mchezaji wa 31 kuitwa katika kikosi cha awali huku Morocco akisema si kosa kwa timu ya Taifa kupunguza au kuongeza mchezaji wakati wowote tu ikiwa bado haijaenda katika Mashindano.

“Hii ni timu ya Taifa wakati wowote unamwita mchezaji au unamtoa kutokana na mahitaji yako, nimelazimika kumuongeza Karihe kwasasa ataungana na wenzake 30 wale wa awali”. Alisema Morocco.


Wakati huo huo kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar kimeendelea na mazoezi yake asubuhi ya leo kuendelea namazoezi nyake kujiandaa na mashindano hayo chini ya mwalimu wake Hemed Suleiman Morroco.
Wachezaji waliyoanza mazoezi ni wale ambao vilabu vyao vya Unguja huku ikiwa bado makundi mawili kutoka Kisiwani Pemba na Tanzania Bara bado hawajajumuika na wenzao ambapo wale kutoka Pemba wakitarajiwa kesho kuungana na wenzao.

Wachezaji waliyoanza mazoezi ni Walinda mlango Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Walinzi Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).


Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad Mshamata (Chuoni) pamoja na washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe)
Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Wednesday, 8 November 2017

UKATA WA FEDHA WAPELEKEA KUOTA MBAWA KWA LIGI KUU YA NET BALL ZANZIBAR.

Hatimae ligi kuu ya netball iliyokuwa ifanyike kisiwani Pemba yaota mbawa kutokana na ukata wa fedha unaovikabili vilabu sambamba na chama cha mchezo huo.


Hayo yameelezwa na katibu wa chama cha mchezo huo Said Ali mansab wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu.

Amesema chama chao kimepokea taarifa kutoka kwa wenzao waliopo Pemba kuwa vilabu vya Pemba havitashiriki katika ligi hiyo nakupelekea viongozi kukutana hapo jana kujadili suala hilo nakutafuta njia ya kufanya ilikupatikana muwakilishi wa Zanzibar katika ligi ya Muungano.


Aidha ameongeza kuwa baada yakukutana chama cha netball Zanzibar kimeamua vlabu vya Unguja kushiriki katika kombe la Muungano sambaba na mashindano ya Afrika mashariki na kati yatakayofanyika mwezi wan ne mwakani.

Akivitaja vilabu vitakavyoshiriki katika ligi hiyo ya Muungano katibu huyo amesema ni pamoja na JKU,Mafunzo,Duma ,KVZ,Zimamoto na Afya.

Amewataka wadu wa mchezo huo kuwaunga mkono ilikuimarisha mchezo huo visiwani hapa.

Ligi kuu ya Muungano kwa mchezo wa Net ball inatarajiwa kufanyika kuanzia November 26 mwaka huu katika kiwanja cha Gymkhana.












Sunday, 5 November 2017

MAPINDUZI CUP 2018 KUJUMUISHA TIMU 10,MLANDEGE,SHABA KUSHIRIKI MICHEZO HIYO

Kamati inayosimamia mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup 2018) inaendelea na matayarisho ya michuano hiyo huku timu 10 zinatarajiwa kushiriki msimu huu.

Hayo yameelezwa na katibu wa kamati ya mashindano hayo Khamis Abdallah Said wakati akizungumza na waandishi wa habari nakusema kuwa licha yakupata maombi kutoka kwa timu mbali kuhitaji kushiriki katika mashindano hayo kamati yao imeamua kuwa na timu kumi kutokana na muda.


Ameomgeza kuwa kuna baadhi ya timu zilikuwa tayari kuharamia kila kitu wao wakihitaji kushiriki tu katika mashindano hayo lakini kamati yao imeona muda wakuendesha mashindano hayo hautotosha.

Akizitaja timu amabzo zitashiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Azam ambao ni mabingwa watetezi, Simba na Yanga zote ikiwa nikutoka Tanzania bara huku kisiwa cha Unguja kikiwakilishwa na JKU, Zimamoto, Taifa ya Jang'ombe na Mlandege na kwa upande wa Pemba kikijumuisha timu ya Shaba na Jamhuri na timu moja kutoka nje ya Tanzania bado haijajulikana lakini itatokea Kenya au Uganda.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi mwishoni mwa mwezi Disemba na fainali itapigwa Januari 13, 2018.

Wajumbe wa Kamati wanaosimamia Mashindano hayo Mwenyekiti ni Sharifa Khamis, huku Makamo Mwenyekiti Gulam Rashid, Katibu Khamis Abdalla Said huku Wajumbe wakiwa Issa Mlingoti Ali, Dk. Ally Saleh Mwinyikai,  Ali Khalil Mirza, Khamis Mzee Ali, Ravia Idarous Faina, Ali Mohammed, Mohammed Ali Hilali (Tedy) na Juma Mmanga.

Morroco ataja kikosi cha awali Zanzibar Heroes.

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes),Hemed Suleiman (Morocco) ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa ma Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 hadi Disemba 9, 2017 nchini Kenya.


WALINDA MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe)
Nassor Mrisho (Okapi)
Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU)

WALINZI
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga)
Mohd Othman Mmanga (Polisi)
Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys)
Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar)
Haji Mwinyi Ngwali (Yanga)
Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege)
Issa Haidar "Mwalala" (JKU)
Abdulla Kheir "Sebo" (Azam)
Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe)

VIUNGO
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City)
Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe)
Mudathir Yahya (Singida United)
Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi)
Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar)
Amour Suleiman "Pwina" (JKU)
Mbarouk Marshed (Super Falcon)
Ali Yahya (Academy Spain)
Hamad Mshamata (Chuoni)
Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji)

WASHAMBULIAJI
Kassim Suleiman (Prisons)
Matteo Anton (Yanga)
Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe)
Feisal Salum (JKU)
Salum Songoro (KVZ)
Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys)
Mwalimu Mohd (Jamhuri)
Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto)

Sunday, 29 October 2017

NYOTA REAL KIDS FC,WAPIMWA AFYA ZAO ,TAYARI KWA MICHEZO YA VIJANA YALIYOFUNGULIWA JUMAMOS OCTOBER 28.

Katika kuhakikisha wanaepusha matatizo ya kiafya kwa wachezaji wao wawapo uwanjani uongozi wa timu ya  Realkdis Fc inayoshiriki ligi madaraja ya vijana nadani ya wilaya ya ya mjini Unguja imewafanyia vipimo vya afya nyota wao ilikujua matatizo yanayowakabili nyota hao.

Akizungumza nasi katibu wa timu hiyo Nassor Abdaallah amesema lengo kuu lakufanya hivyo nikujua afya za nyota wa sambamba na kuepusha matatizo ambayo yanaweza kujitokeza kwa wachezaji ambao kwa mujibu wa afya zao hawastahiki kucheza mpira.

Aidha ameishukuru timu ya maktari ambayo imefanya kazi hiyo kwa kushirikia na uongozi wa timu hiyo nakusema zoezi hilo la upimaji afya kwa wachezaji wao litakuwa likifanya kila muda ilikulinda afya za wachezaji wao nakuwataka wachezaji wa timu hiyo kufuata ushauri waliopewa na madaktar baada yakupima afya.


"Tunawashukuru timu ya madaktari kwa kushirikiana na uongozi kuhakikisha kuwa zoezi hili la upimaji wa afya limekwenda vizuri na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kugundua baadhi ya matatizo yanayowakabili vijana wetu sambamba na kuwapa elimu ya afya jinsi ya kulinda afya ya miili yao haswa misuli kwa kufanya mazoez kwa bidii na njia iliyo sahihi ili iwasaidie kufanya vizuri katika mechi zao za kila siku” alisema.


Vipimo ambavyo walifanyiwa nyota hao ni pamoja na vipimo vya damu kama vile blood group, blood glucose, blood pressure,Afya ya masikio, uoni wa macho, misuli pamoja na joints.

Saturday, 28 October 2017

Wilaya ya mjini yazindua mashindano ya vijana ,Chura awataka makocha kuacha tabia za uzalilishaji kwa vijana.

Mashindano ya vijana Central league wilaya ya mjini Unguja yamezinduliwa rasmini asubuhi ya leo katika kiwanja cha Amani mjini Unguja kwa mchezo kati ya timu ya Aman Academy na timu ya Mpira Pesa.
Rais wa Raska zone Ali Mkanga akisalimiana na muamuzi wa mchezo kati ya timu ya Amani Academy na Mpira Pesa Abubakary Khatibu mchezo ambao umemalizika kwa sare yakufungana goli 1-1.


Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani kwa pande zote timu hizo zimetoka sare yakufungana goli 1-1.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya mjini Unguja Hassan Haji Hamza amemewataka walimu wanaofundisha soka la vijana kuachana na vitendo vya unyanyanyasaji watoto sambamba na kuwaingilia kinyume na maumbile.
Viongozi wa kamati ya mashindano ya vijana wilaya ya mjini wakiwa katika picha ya pamoja  na mgeni rasmini katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo Ali Mkanga.

Amesema kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi kwa baadhi ya makocha kushiriki katika vitendo hivyo jambo ambalo linahitajika kupingwa kwa nguvu zote.

Amesema endapo chama chao kitapata uhakika wa tuhuma hizo hatua kali watamchukulia muhusika huku akilitaka jeshi la polisi visiwani kufuatilia kwa umakini mkubwa tuhuma hizi ili kama zipo ziwezekupatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake rais wa Raska zone Ali Mkanga amewataka vijana kujituma katika michezo kwani michezo ni ajira.

Thursday, 26 October 2017

ZFA yaridhishwa na maendeleo ya soka la wanawake visiwani.

Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kimeelezea kuridhishwa kwake na hamasa  uliojitokeza kwa timu za wanawake zinazoshiriki ligi dogo ya kinamama inayoendelea katika kiwanja cha Amani mjini Unguja ambapo lengo nikutafuta wachezaji 20 watakaounda timu ya taifa ya wanawake itakayoshiriki katika mashindano ya kina mama kule nchini Rwanda.

Akizungumza na mtandao huu katibu wa chama cha mpira wa miguu Zanzibar Muhamed Ali Hilal Tedy amesema michezo hiyo inayoendelea visiwani hapa tayari makocha waliopewa jukumu lakutafuta wachezaji wanaendelea kufanya kazi hiyo.

Ameongeza kuwa katika michezo iliyochezwa vijana kadhaa wameonesha viwango vya hali ya juu na kinachosubiriwa kwa sasa ni makocha waliopewa jukumu kumaliza kazi yao nakutangazwa watakaobahatika kuitwa katika timu ya taifa ya wanawake.


Ameongeza kuwa tayari chama chao kimepokea majina ya wachezaji watano kutoka Pemba ambao wataungana na 15 kutoka Unguja kutangazwa kikosi kamili.


Ameongeza kuwa mara baada yakutangazwa kwa kikosi hicho kocha aliepewa dhama yakukinoa kikosi hicho ataanza majukumu yakukiandaa kikosi kabla yakuondoka kuelekea katika mashindano ya Afrika mashariki na kati kwa upande wa kina mama yanayotarajiwa kufanyika Rwanda mapema mwezi ujao.

Wednesday, 25 October 2017

Simba yazidi kuitafutia kasi Yanga na mvua yao.

Wekundu wa msimbazi Simba wanaendelea kujinoa visiwani Zanzibar kwa ajili yakujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya mahasimu wao Yanga mchezo ambao utavurumishwa Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.


Simba ambao wapo visiwani wanafanya mazoezi yakujiandaa na mchezo huo katika kiwanja cha Amani kwa wakati wa asubuhi na katika dimba la jeshini jioni kwa baadhi ya siku.

Ikiwa simba ikiendelea na mzoezi yakujiandaa na mahasimu wao Yanga mshambuliji wachezaji wao waliokuwa majeruhi mshambuliaji John Bocco na kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim wameonekana wakifanya mazoezi ya nyota wenzao kuashirikia kuwa tayari kuikabilia Yanga.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa habari wa timu hiyo wekundu hao wa msimbazi wanatarajiwakuondoka visiwani hapa Jumamosi asubuhi kuelekea Tanzania bara kwa mchezo huo.

Mzunguko wa nne ligi kuu soka Zanzibar kituo cha Unguja kuanza kesho,Miembeni City kuwakaribisha Chuoni FC.

Baada yakuenda mapumzikoni kwa takribani siku mbili ligi kuu soka ya Zanzibar kituo cha Unguja inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho kwa kuanza michezo ya mzunguko wa nne.

Ambapo hapo kesho mtanange mmoja utavurumishwa katika kiwanja cha Amani mjini Unguja mnamo majira ya saa kumi alasiri ambapo timu ya Chuoni itajitupa katika kiwanja cha Amani kuoneshana kazi na timu ya Miembeni City.

Chuoni inashuka katika kiwanja cha Amani mjini hapa wakiwa na alama 4 huku Miembeni City wenyewe wakijitupa katika mchezo huo wakiwa na rekodi mbaya yakupoteza michezo mitatu mfululizo.

Michezo mengine ya mzunguko huo wa nne ya ligi kuu soka ya Zanzibar inaendelea kesho kutwa Jumamos ambapo mitanange miwili itavurumishwa mnamo majira ya saa nane mchana Taifa ya Jang’ombe itakipiga na JKU  huku mnamo majira ya saa kumi alasiri KVZ inamenyana na Mafunzo.

Ikiwa ligi hiyo inaingia mzunguko wa 4 jioni ya kesho mpaka sasa timu ya KVZ inaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 9 wakifuatiwa na JKU wenye alama tisa tofauti yao ikiwa ni magol yakufungwa nanakufunga.

Ratiba kamili ya michezo ya mzunguko 

IJUMAA
27/10/017
22
MIEMBENI CITY
VS
CHUONI
SAA 10:00 ALS AMAAN
J’MOSI
28/10/017
23
TAIFA YA J/MBE
VS
JKU
SAA 8:00 MCH AMAAN
J’MOSI
28/10/017
24
KVZ
VS
MAFUNZO
SAA 10:00 ALS AMAAN
J’PILI
29/10/017
25
KIPANGA
VS
POLISI
SAA 8:00 MCH AMAAN
J’PILI
29/10/017
26
KMKM
VS
ZIMAMOTO
SAA 10:00 ALS AMAAN
J’TATU
30/10/017
27
BLACK SAILORS
VS
CHARAWE
SAA 8:00 MCH AMAAN
J’TATU
30/10/017
28
JANG’OMBE BOYS
VS
KILIMANI CITY
SAA 10:00 ALS AMAAN