Wednesday, 31 May 2017

TUIUNGENI MKONO COMBINE YA ROLLING STONE,RAZA LEE.

Mdau wa michezo visiwani Zanzibar Mohamed Ibrahim “Raza Lee”amewataka wadau mchezo wa mpira wa miguu visiwani Zanzibar kuungana kwa hali na mali kuwapatia vifaa sambamba na michango yao timu ya Combine ya wilaya ya mjini inayotarajiwa kushiriki katika mashindano ya Rolling stone yatakayofanyika kuanza June 29, 2017 hadi July 9, 2017 jijini Arusha.
Mdau wa soka Visiwani Zanzibar Mohamed Ibrahim "Raza Lee"akikabidhi mipira kwa viongozi wa combine ya rolling stone wa kat ni katibu wa timu hiyo Ali Othman na kocha Muhamed Seif King.(Picha na Abubakary Hatibu)


Akizungumza na zenjsport-on line mara baada yakukabidhi vifaa hivyo mdau huyo wa michezo visiwani amesema ipo haja yakuwaunga mkono vijana hao ambao wamepania kurudi na ushindi katika mashindano hayo.

Ameongeza kuwa endapo wadau wa soka watatoa michango yao ya hali na mali imani yake vijana hao watafanya vyema katika mashindano hayo.


Timu ya combine ya wilaya ya mjini wanakwenda katika mashindano hayo kutetea taji lao walilotwaa katika mashindano yaliyofanya mwaka jana Arusha Tanzania.

LUGHA ,KIWANGO CHA ELIMU UTATA RASIMU YA KATIBA ZFA.

Na:Abubakry Hatibu

Ikiwa ni siku chache zimepita tokea kamati iliyoundwa kutengeneza katiba ya chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kukabidhi rasimu hiyo kwa katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar baadhi ya viongozi wa ZFA wa mawilaya wameanza kuonesha hofu yao juu ya rasimu hiyo.


Wakizungumza na zenjsport-on line kwa nyakati tofauti baadhi ya Viongozi hao wamesema ni vigumu sana kupita rasimu hiyo kwani ina mapungufu mengi sana huku wakitaja la kiwango cha elimu nakuandikwa kwa lugha ya kigeni.

“Hii Rasimu ina vichekesho sana tulipoiona tulishtuka, sisi viongozi ati tuwe na elimu kuanzia Form IV, kisha imeandikwa kwa Kiengereza wakati sisi ni Waswahili!, si rahisi kupita mazali na sisi ni miongoni mwa wapitishaji, kwasababu uongozi si kusoma bali uongozi ni kipaji na mapenzi ya kitu”.

Akizungumzia hali hiyo katibu wa kamati iliyoteuliwa kuunda katiba hiyo ambae pia ni mwanasheria wa ZFA Saleh Ali Said
Amewatoa wadau hao wa soka kuisoma kwa makini rasimu hiyo sambamba nakutomapungufu yaliyomo katika rasimu hiyo ili ipatikane katiba iliyobora zaidi ambayo inaendana na CAF.


Kamati ya kuandika katiba mpya inaundwa na wajumbe sita (6) ambao ni Afan Othman Juma (Mwenyekiti), Saleh Ali Said (Katibu), Othman Ali Hamad (Msaidizi Katibu), Nassra Juma, Eliud Peter Mvella na Ame Abdallah  Dunia.

HUSSEIN DECO AUNGANA NA MKOKO ROLLING STONE.

Kikosi cha mabingwa  wa mashindano ya vijana ya Rolling Stone kombain ya Mjini Unguja kimezidi kuimarika baada ya kuongezeka kwa kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys na timu ya Kilimani City Assad Juma lengo ikiwa ni kutetea taji walilotwaa katika msimu uliomalizika.
 
KIUNGO WA KILIMANI CITY ASAAD JUMA AKIWA KATIKA MAJUKUMU YA TAIFA GABON
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwalimu wa timu hiyo Muhammed Seif King amesema ameamua kumuongeza kiungo huyo ilikuimarisha zaidi kikosi chake.
DECO AKIWA MZIGONI


Ukiachia Hussein Deco nyota wengine walioitwa kuongeza nguvu katika kikosi hicho ni pamoja na mshambuliaji wa Miembeni City ambae pia alikuwepo katika kikosi cha Serengeti boys kilichokuwepo AFCON Ibrahim Abdallah(Imu Mkoko), mlinda mlango wa Miembeni City Aley Ally,mshambuliaji wa Villa United Juma Ali Yussuf “James” na Muharami Khamis “Terra” wa Black Sailors pamoja na Abdul hamid Salum “Ramos” KVZ.

Kikosi cha Mjini Unguja (Mabingwa watetezi) mpaka sasa kina jumla ya nyota 26 wakiwemo walinda mlango Aley Ali Suleiman “Manula” (Miembeni city), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na Makame Mkadar Koyo (Huru).
KIUNGO WA KILIMANI CITY ASAAD JUMA AKIWA NA MSHAMBULIAJI WA MIEMBENI CITY IBRAHIM ABDALLAH

Wachezaji wa ndani ni Muharami Khamis “Terra” (Black Sailors), Abdul hamid Salum “Ramos” (KVZ), Ali Juma Maarifa “Mabata” (Taifa ya Jan’ombe), Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim Ameir (King Boys), Shaaban Pandu (Villa United), Idrissa Makame (Villa FC), Ramadhan Simba (Calypso), Ali Hassan (Uhamiaji), Fahmi Salum (Mlandege), Salum Omar (Villa United), Yakoub Omar (Jang’ombe Boys) na Mohd Ridhaa (Villa United).

 
MKOKO MZIGONI

Wengine ni Mohd Jailan (Chrisc), Makame Masoud (Schalke 04), Mohd Mussa (Mapembeani), Abrahman Juma (KMKM), Mohd Haji (Jang’ombe Boys), Abdul-hamid Juma (ZAFSA), Ibrahim Chafu (Villa FC) ,Ibrahim Abdallah(Miembeni Cit),Asaad Juma (Kilimani City)na Juma Ali Yussuf “James” (Villa United).
KOCHA WA COMBINE YA WILAYA YA MJINI MUHAMED SEIF KING AKISALIMIANA NA KOCHA WA ZIMAMOTO  SEIF BAUSI ALIEVAA FULANA CHEUPE

Tuesday, 30 May 2017

VIONGOZI WAPYA BAZA KUPATIKA MWEZI WA SITA.


Chama cha mchezo wa kikapu visiwani Zanzibar kipo katika mipango ya mwisho yakufanikisha uchaguzi mkuu wa chama hicho.
KIKOSI CHA TIMU YA KIKAPU YA AFRICAN MAGIC 


Akizungumza na zenjsport-on line  makamo mwenyekiti wa chama cha mchezo wa mpira wa kikapu Zanzibar Rashid Hamza amesema harakati za kufanikisha uchaguzi huo zinaenda vizuri.
Uwanja_wa_mpira_wa_kikapu


Ameongeza kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya katiba ya chama hicho kutakuwa na mapungufu ya baadhi ya nafasi ambapo mwaka huu kutakuwa na nafasi chache sana zakugombania.

 “Unajua tunachosubiri sasa ni kutoka kwa katiba yetu mpya na katika mpya imepunguza idadi ya nafasi za kugombania tofauti na zamani katiba iliyokuwa ikitumika nyuma ilikuwa na nafasi ya makamo mwenyekiti Unguja na Pemba sambamba na naibu katibu Unguja na pemba jambo ambalo katika katiba mpya nafasi hizo hakuna”alisema makamo mwenyekiti huyo.


Aidha amevitaka vilabu kulipia ada ya mwaka kwa baraza la michezo ilikufanikisha kushiriki katika zoezi hilo la uchaguzi.

BOYS WAZIDI KUJIFUA KWA AJILI YA MASHINDANO YA SPORT PESA

Timu ya Jang’ombe boys wanaendelea kujinoa kwa ajili ya mashindano ya Sport pesa super cup yanayotarajiwa kufanyika Tanzania bara mapema mwezi ujao .
KIKOSI CHA TIMU YA JANG'OMBE BOYS KITAKACHOSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SPORT PESA


Akizungumza na zenjsport-on line kocha mkuu wa timu hiyo Mahmoud Abdallah Yussuf amesema vijana wake wapo katika hali nzuri huku akitarajia kufanya vyema zaidi katika mashindano hayo.

Aidha maeongeza kuwa vijana wake wapo katika ari kubwa kuona wanafanya vyema katika michezo hiyo huku akiamini kuwa watafanya vyema katika mashindano hayo.
ABDI KASSIM BABI AKIWA KATIKA MAJUKUMU YA JANG'OMBE BOYS.


Akizungumzia wapinzania wake kocha huyo amesema wanawaheshimu sana wapinzani wao na ni timu nzuri lakini anawaanda wachezaji wake kwa ajili yakupambana.

Kwa upande wake Abdi Kassim Babi amesema mazoezi yanaenda vizuri atatumia uzoefu alionao kuona timu inafanya vizuri katika michezo hiyo.
ABDI KASSIM BABI AKIWAJIBIKA NJE YA TANZANIA 


Amewataka wadau na washabiki wa soka visiwani Zanzibar kuunga mkono juhudi za timu yao ilikufanya vyema nakuijengea heshima Zanzibar kisoka.

Saturday, 27 May 2017

MKOKO ATOA FUNZO KWA VIJANA WA KIZANZIBAR

Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” amewataka vijana wa kizanzibar kujutuma ilikuitumia fursa iliyoipata Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF.

Mkoko ambae amerejea Visiwani Zanzibar akitokea mjini Gentil, Gabon katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania “Serengeti Boys” amesema vijana wa kizanzibar wanatakiwa kuitumikia fursa hiyo ipasavyo ilikujiendeleza zaidi kisoka.
Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” akiwa katika majukumu ya taifa na Serengeti boys.

Akizungumza na zenjsport –on line mshambuliji huyo amesema amefurahishwa mno kwa Zanzibar kupata uwanachama wa shirikisho la soka barani Afrika huku akiamini kuwa vijana wengi wa kizanzibar watapata nafasi yakuonesha kiwango chao.

“Unajua uwanachama wa CAF utatoa nafasi kwa vijana wa kizanzibar kushiriki katika mashindano ya kimataifa binafsi nimefurahishwa mno kufuatia kupatiwa unachama huu na ni muda wa vijana wa nyumbani kuvitangaza vipaji vyetu”alisema mkoko.

Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” akiwa katika mazoezi ya kombain ya wilaya ya mjini Unguja kwenye Uwanja wa Amaan kwa kujiandaa na Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanyika mwezi July mwaka huu jijini Arusha.


Akizungumzia ushiriki wake katika mashindano ya AFCON Imu amesema mashindano hayo yamemsaidia kujenga uimara na uwezo wa kiwango chake huku akihidfi kuyafanyia kazi yale yote ambayo amejifunza katika mashindano hayo.

“Kushiriki katika mashindano ya AFCON nimejisikia vizuri kwa sababu nimejenga confidence,nimejifunza nini professional wanaishi, unajua kunatofauti kubwa kati ya mashindano yetu haya ambayo tumeyazoea kama copa cocacola na mengine nitajua vipi nikae katika timu yangu”aliongeza Mkoko.

Ibarahim Abdallah ambae kwa sasa anakipiga katika kilabu ya Miembeni City ambayo imepanda kushiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018 amepania kufanya vyema zaidi ilikufikisha malengo yake ya soka.

Wednesday, 24 May 2017

JANG'OMBE BOYS KUSHIRIKI SPORT PESA SUPER CUP

KAMPUNI ya SportPesa imeandaa mashindano maalum ya soka yatakayojulikana kama SportPesa Super Cup yatakayoshirikisha timu za Tanzania, Zanzibar na Kenya.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema , bingwa wa michuano hiyo atapata dola za Kimarekani 30,000 na nafasi ya kucheza dhidi ya timu ya England.



Amezitaja timu hizo kuwa Simba SC, Yanga SC na Singida United kwa Tanzania Bara, Jang'ombe Boys ya Zanzibar, Gor Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker FC za Kenya.

Tarimba amesema kwamba michuano hiyo itaanza Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11 na itafanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

“Tunatarajia mashindano haya yatakuwa changamoto nzuri kwa timu zote zitakazoshiriki na pia burudani nzuri kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini, hususan mashabiki wa timu zenyewe,”amesema Tarimba.  



RATIBA YA SPORTPESA SUPER CUP


Juni 5, 2017


Singida United Vs FC Leopard
Yanga SC Vs Tusker FC


Juni 6, 2017
Jang`ombe Boys vs Gor Mahia
Simba Vs Nakuru All Star


NUSU FAINALI


Juni 8, 2017
Singida United/AFC Leopards Vs Yanga SC/Tusker FC
Simba SC/Nakuru All Star Vs Jangombe Boys/Gor Mahia


FAINALI
Juni 11, 2017

Saturday, 20 May 2017

JANG'OMBE BOYS ,JKU HAPOTOSHI AMANI KESHO,MWENGE ,OKAPI GOMBANI

Ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya nane bora inaendelea jioni ya kesho Jumapili 21/5/2017 kwa michezo miwili itakayovurumishwa katika viwanja viwili tofauti.
Katika kiwanja cha Amani mnamo majira ya saa kumi alasiri Jang’ombe Boys itaoneshana kazi na timu ya JKU, huku katika kiwanja cha Gombani kisiwani Pemba  Mwenge watamenyana na OKAPI.







Thursday, 18 May 2017

SERENGETI BOYS, ANGOLA KATIKA PICHA





SERENGETI BOYS MZIGONI TENA

TIMU ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys jioni ya leo inajitupa katika dimba la L’Amitie kumenyana na Angola katika mchezo wake wa pili wa mashindano ya vijana chini ya miaka 17.

Serengeti Boys inashuka dimbani ikihitaji ushindi ili kuweka hai matumaini ya kusonga mbele baada ya kutoka sare katika mchezo wa awali dhidi ya Mali.






Wednesday, 17 May 2017

GUNDU LAMTAWALA KISANDU ZAHLIFE CUP , Z.U WAENDELEZA UBABE

Matumaini ya chuo cha uandishi wa habari kusonga mbele katika mashindano ya vyio vikuu na taasisi ya elimu ya juu Zanzibar yamefifia baada ya jioni ya leo kukubali kipigo cha magol 3-0 kutoka kwa chuo cha Mwenge Community Center (MCC) mchezo uliochezwa katika kiwanja cha Ng'ome Fuoni.

Chuo cha habari kwa sasa wanasubiri mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kati ya timu ya Chuo cha Afya na timu ya MCC huku chuo cha habari huenda kikasonga ambapo MCC wataifunga timu ya Chuo cha Afya jumla ya magol 4-0.
KIKOSI CHA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR
KIKOSI CHA ZANZIBAR UNIVERSTY (Z.U)

ZIMAMOTO ,BOYS HAKUNA MBABE ,KIZIMBANI YAIADHIRI MWENGE

Timu ya Jang'ombe boys imelazimishwa sare ya tasa na timu ya Zimamoto ikiwa ni muendelezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar mchezo uliochezwa katika dimba la Amani mjini Unguja.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani kwa timu zote huku zikiwa na mashambulizi ya zamu hadi kipenga cha muamuzi Mfaume Ally kinapulizwa kuashiria kumalizika kwa mchezo huo hakuna timu iliyoona lango la mweziwe.



Kikosi cha Jang'ombe Boys 

KIKOSI CHA ZIMAMOTO
Katika mchezo uliochezwa katika kiwanja cha Gombani kisiwani Pemba timu ya Kizimbani ikaifungwa timu ya Mwenge magol 2-1.

Ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya nane bora inaendelea kesho ambapo mnamo majira ya saa kumi alasiri katika uwanja wa Amani Taifa ya Jang'ombe itakipiga na timu ya JKU huku katika dimba la Gombani kisiwani Pemba Okapi itakipiga na Jamhuri.

MCC LAZIMA WAFE ,KISANDU .

Baada ya sare ya tasa dhidi ya timu ya Chuo cha afya Mbweni timu ya chuo cha waandishi wa habari Zanzibar leo hii inajitupa tena dimbani kuoneshana kazi na timu ya chuo cha MCC mtanage ambao utavurumishwa katika dimba la Fuoni mnamo majira ya saa kumi alasiri.
KOCHA WA TIMU YA UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR ABUBAKARY HATIBU 

Mtanange huo unatarajiwa kuwa na ushindi kwa pande zote huku kila timu ya ikijinadi kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Kocha wa timu ya chuo cha waandishi wa habari Zanzibar Abubakary Hatibu amesema wamejipanga kuona wanafanya vyema katika mchezo huo huku akitarajia kuwapanga wachezaji ambao wanauwezo wa hali ya juu.
WACHEZAJI WA TIMU YA CHUO CHA HABARI WAKIWA NA KOCHA WAO KISANDU
“Unajua tulitoka sare na afya mchezo ambao ulikuwa na upinzani huku tukiwa pungufu nimerudi mazoezi na vijana wangu nimeyafanyia kazi mapungufu naamini vijana watafanya vyema katika mchezo na MCC”Alisema Kisandu.
KISANDU AKIWA MZIGONI
Akizungumzia vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyofanya na mchezaji wake kocha huyo ameelezea kusikitishwa kwake na kitndo hicho huku akiongeza kuwa uongozi wao timu yake umemsimamisha mchezaji huyo na hatamtumia tena katika mchezo wa leo.

Tuesday, 16 May 2017

KOCHA KING AACHANA NA JKU,AELEKEZA NGUVU ZAKE KATIKA SOKA LA VIJANA.

Aliyekuwa  kocha  mkuu wa timu ya JKU  inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar Muhamed Seif King amesema ameachana na JKU na kwa sasa anaelekeza nguvu zake zote kuimarisha soka la vijana.

Akizungumza na zenjsport on line kocha huyo amesema sababu kuu iliyomfanya kuachana na timu hiyonikutokana na kutoelewana nao na kwa sasa ataelekeza nguvu zake katika kufundisha timu za vijana .

KOCHA MUHAMED SEIF KING ALIEVAA KAPELO AKIWA KATIKA BENCH LA UFUNDI LA JKU KATIKA MOJA YA MICHEZO YA LIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR.

‘’Unajua nimefundisha timu nyingi kwa mafanikio lakini sasa nataka kuelekeza nguvu zangu katika soka la vijana nakuacha soka la ushindani,vijana wengi wanakosoka misingi imara hivyo nataka nitumie muda wangu uliobakia katika kukuza soka la vijana nchini ”Alisema kocha King.

Ameongeza kuwa kujiondoa kwake katika timu ya JKU kutampa nafasi yakuwa na vijana hao kwa muda mrefu jambo ambalo kutamuwezesha yeye katika kuandaa timu za vijana ambazo atakuwa akizifundisha.

Amefafanua kuwa kwa sasa hana mpango hasa wakufundisha timu yoyote ile iliyopo katika ligi za ushindani huku akikanusha uvumi wakuwa yeye anatarajiwa kujiunga na timu ya Mlandege.

"Kwa sasa sitaki timu ya mtu yoyote yule nitaangalia zaidi vijana na lessen yangu ndivyo inavyonielekeza nitatumia muda wote nikiwa na vijana wa wilaya ya mjini na ile timu niliyopewa ilikuifanya iwe imara na ya ushindani"Alisema King.
KOCHA KING AKISALIMIANA NA KOCHA SALUM BAUSI.


Kuhusu makubaliano yake na timu hiyo kocha huyo amesema JKU walimchukua kwa majaribio yakumaliza mechi 12 ambazo tayari zimemalizika na kwa sasa JKU hawamuhitaji kocha huyo.

Kocha King ameongeza kuwa kwa sasa anaendelea na mazoezi na timu ya combine ya wilaya ya mjini ambayo itashiriki katika mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kufanyika Arusha mwishoni mwa mwezi wa sita.

KINA MKOKO WAANZA AFCON KWA SARE

TIMU ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ jana imelazimishwa sare ya tasa dhidi ya Mali ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa AFCON U17 .

Katika mchezo huo ulikuwa na ushindani kwa pande zote mabingwa watetezi, Mali walimiliki mpira kwa muda mrefu jana, lakini wakashindwa kuifunga Tanzania inayocheza mashindano ya ngazi hii kwa mara ya kwanza na mwishowe wakatoka sare ya 0-0.
Matokeo mengine ya kundi B Angola ikalazimishwa sare yakufungana magol 2-2 na Niger .
Mechi za Kundi B zitarudi Alhamisi ya Mei 18, Tanzania wakianza na Angola kabla ya Mali kupepetana na Niger Uwanja wa l’Amitie Sino mjini Libreville.
Hatua ya makundi inatarajiwa kuhitimishwa Mei 20 na 21 mwaka huu, Kundi A Gabon wakimaliza na Cameroon na Guinea na Ghana Uwanja wa Port Gentil kabla ya siku inayofuata, Mali kuanza na Angola na baadaye Tanzania kumalizana na Niger.
Timu mbili za juu katika kila kundi pamoja na kwenda Nusu Fainali, pia zitajihakikishia tiketi ya kucheza Fainali za kombe la Dunia la U-17 Oktoba mwaka huu nchini India


Monday, 15 May 2017

Z.U YAANZA KWA KISHINDO ZAHLFE CUP


Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya juu Zanzibar { ZAHILFE} Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu      {Zanzibar University - ZU} jana ilidhihirisha ubabe wake baada ya kuitandika bila ya huruma Timu ya soka ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere            { MNMA} Magoli 4-0.

Mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 ulifungua pazia la mashindao ya Tamasha la Michezo la Shirikisho hilo uliorindima ndani ya Uwanja wa Michezo wa Amani Mjini Zanzibar ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Mshambuliaji wa mabingwa watetezi wa kombe la ZAHILFE Abdallah Ali Sabebe akisalimiana na makamo wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif  kabla yakunza kwa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya ZAHLFE CUP kati ya ZU dhidi ya Timu ya Soka ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere .

Watetezi hao ZU walionyesha dalili za mapema za ushindi wa mchezo huo licha ya kuwa mpaka wanakwenda mapumziko hakukuwa na timu iliyoona mlango wa mwezake huku washabiki wa Timu zote mbili wakishindwa kukaa kwenye majukwa ya uwanja huo.

Mashabiki wa Timu  ya soka ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu { ZU} wakishangiria kwa kujiamini wakati Timu yao ilipotoa kichapo cha Paka mwizi  cha Goli 4 kwa  Bila dhidi ya Timu ya Soka ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  { MNMA}.

Kipindi cha pili kilianza kwa mikiki mikiki kwa timu zote mbili lakini uzoefu na utaalamu wa Timu ya ZU ukajidhihirisha pale wanandinga hao walipoanza kumimina karamu ya Magoli ndani ya kimia cha MNMA  na hadi mwisho wa mchezo  huo ZU 4 na MNMA 0.

Akiizindua michezo hiyo ya Tamasha la Tano la Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} tokea kuanzishwa kwake Mwaka 2013 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema utunzwaji  wa vipaji vinavyoibuliwa ndani ya mashindao hayo lazima uendelezwe ili kupata wanamichezo bora watakakidhi kiwango cha Kitaifa na Kimataifa.

Balozi Seif  akisalimiana na wachezi wa Timu ya Soka ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  { MNMA} waliopambana na  Mabingwa watetezi wa Kombe la ZAHILFE Timu  ya ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu { ZU}.

Balozi Seif alisema mashindano ya Tamasha la Shirikisho la Zahilfe ni mwanzo wa kuelekea njia sahihi ya kupata vipaji hivyo sambamba na kuchangamsha akili za Wanafunzi katika kukabiliana vyema na masomo yao ya kila siku.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Sera ya Michezo Zanzibar ya Mwaka 2007 imeweka umuhimu wa kuimarisha  Sekta ya Michezo Vyuoni na Maskulini Unguja na Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilifungua Tamasha la Tano la Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar { ZAHILFE} kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

Alisema Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} kupitia Sera hiyo kimeanzisha mafunzo  maalum yalaiyowezesha kutoa Wahitimu 9 wa Stashahada ya Michezo ambao tayari wameanza kusomesha katika maskuli mbali mbali Nchini.

Balozi Seif alihimiza umuhimu wa kuimarishwa michezo Maskulini na Vyuoni kwa vile inasaidia kupatikana kwa matokeo mazuri ya Wanafunzi hasa kwenye mitihani yao pamoja na kuimarika kwa nidhamu miongoni mwa wanafunzi na walimu wao.

Alisema nidhamu  inamuwezesha mtu sio mwanafunzi pekee kufanya kazi zake kwa mipango maalum na akafarajika na utaratibu wa  kuanzishwa kwa mashindano ya Zahilfe yatakayofungua njia sahihi ya kudumisha nidhamu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo na Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar kwa jitihada za watendaji wake kuwaweka pamoja Wanamichezo hapa Nchini.

Mapema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pemba Juma ameipongeza Benki ya Biashara ya NMB kwa moyo wa  kizalendo wa kuamua kwa makusudi kusaidia Sekta ya Elimi Visiwani Zanzibar.

Waziri Riziki alisema Benki ya NMB mbali ya kusaidia Sekta ya Michezo lakini pia juhudi zake za kusaidia Kompyuta 50 pamoja na Vikalio  450 kwa Skuli za Zanzibar ni ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba Uongozi wa Benki hiyo unaendelea kujali umuhimu wa Sekta ya Elimu inayofinyanga wataalamu wa fani zote.

“ Benki ya NMB imekuwa mshirika mkubwa wa Sekta ya Elimu Nchini, mbali ya kusaidia michezo lakini pia kuongeza nguvu zake katika kupunguza uhaba wa Vikavio na vifaa muhimu maskulini kama Kompyuta”. Alisema Waziri wa Elimu Zanzibar.

Akitoa salamu katika uzinduzi huo wa Tamasha la Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} Afisa Mkuu Wateja wadogo wadogo na wa kati pamoja uendeshaji Matawi ya Benki ya NMB Bwana Abdulmajid Nsekela alisema Taasisi hiyo ya kifedha itaendelea kusaidia huduma za Kijamii kadri mapato ya makusanyo yake yanavyoongezeka.

Bwana Nsekela alisema wadau wakuu wa Taasisi hiyo wengi wao ni Wananchi, hivyo hakuna budi wala kigugumizi kwa Uongozi wa Benki hiyo kuzipa kisogo changamoto  zinazowakabili Wananchi hao katika maeneo yao wanayoishi.

Hilo ni Tamasha la Tano la Michezo inayoandaliwa na Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} tokea kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2013.

Sunday, 14 May 2017

TAIFA YA JANG'OMBE YAKUBALI UTEJA YALAZWA 3-0 NA MAHASIMU WAO.

Magol Hafidh Barik (Fii) dakika ya 67, Khamis Mussa "Rais" dakika ya 74  na Juma Ali "Mess" dakika ya 89 yameifanya Jang’ombe boys kuondoka kiwanja kidedea baada yakuwafungwa mahasimu wao wa jadi timu ya taifa ya jang’ombe.

Khamis Mussa rais mfungaji wa goli la pili .



Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa hali ya juu kwa pande zote huku ukitawaliwa na ubabae wa hapa na pale jambo ambalo lilipelekea muamuzi wa mchezo huo Mfaume Ali Nassor kuwatoa nje kwa kadi nyekundu mshambuliaji wa Jang’ombe boys Rashid Mohd mnamo Dakika ya 24 na na mshambuliaji  Ali Badru wa Taifa mnao dakika ya 26 kutokana na utovu wa nidhamu.

Mashabiki wa taifa ya Jang'ombe

Matokeo hayo inafanya timu ya jang’ombe boys kukaa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na alama tatu sawa na Okapi,Jamhuri na Zimamoto,boys wakiwazidi wapinzani wao kwa uwiano mzr wa magol yakufungwa ambapo tayari wamshatia kambani magol 3 huu katika nyavu zake ikiwa hawajafungwa goli hata mmoja.
Kikosi cah new king