Thursday, 29 June 2017

IDADI YA MAKOCHA WENYE LESSEN A ,YAONGEZEKA ZANZIBAR.



Idadi ya makocha wenye lessen A imeongezeka visiwani Zanzibar baada ya makocha  saba kutoka Zanzibar  kuwa miongoni mwa makocha 19 waliohitimu kozi ya Daraja ‘A’ ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) iliyofanyika Makao Makuu ya Shirikisho la Kabumbu Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.

Kocha Abdul Mutik Haji wa timu ya Jamhuri ni miongoni mwa makocha waliohitimu kozi ya Lessen A ya ukocha.

Makocha hao walimaliza gwe ya pili ya siku 19, katika kozi hiyo ambayo mbali ya kuwa na wakufunzi wengine, wakufunzi wakuu wa CAF walikuwa ni Athumani Lubowa na Sunday Kayuni.

Kayuni ambaye ni Mkurugenzi wa zamani wa TFF katika kozi hii amehudumu kama mkufunzi mkuu wa CAF na aliyekuja kuwasimamia (Accessor) ni Mkurugenzi wa sasa wa Shirikisho la Soka Uganda, Athumani Lubowa.
Malale Hamsini Keya.

Makocha hao (7)kutoka Zanzibar waliohitimu katika kozi hiyo ya ukocha kwa ngazi ya lessen A  ni Abdul mutik Haji “Kiduu” (Jamhuri), Hababuu Ali Omar (JMK Youth Park), Abdallah Mohammed Juma “Bares” (Prisons), Malale Hamsini Keya (Ruvu Shooting), Ali Vuai Shein (Kijichi),  Salum Juma Makame (Tanga) pamoja na kocha Salum Ali Haji (Chwaka Stars).


Makocha wengine waliohitimu katika kozi hiyo ni pamoja na Kidao Wilfred Mzigama, Wane Nelson Mkisi, Meck Maxime Kianga, Emmanuel Raymond Massawe, Mohammed Alawdin Tajdin, Fikiri Elias Mahiza, Juma Ramadhani Mgunda na Dismas Gordon Haonga, Abdul Hassan Banyai, Maka Andrew Mwalwisi, Dennis Mrisho Kitambi na Sebastian Leonard Nkoma.

Saturday, 24 June 2017

ZFA IBADILIKE ILIKUIMARISHA SOKA LETU,KOCHA BUSHIR.

Kocha mkuu wa timu ya Mwadui ya Shinyanga Ali Bushir Mahmoud amewataka viongozi wa chama cha mpira wa miguu visiwani kubadilika kiutendaji ilikuimarisha soka katika visiwa vya Zanzibar.
 
Kocha Ali Bushir Mahmoud.
Bushir ametoa ushauri huo wakati alipokuwa akizungumza na zenjsport on line nakusema kuwa baada ya Zanzibar kupata uanachama wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF)  lazima viongozi wa chama cha soka kubadilika kiutendaji nakuacha kufanya kazi kimazoea ilikukuza soka la Zanzibar.

“Lazima tujieke sawa katika uongozi,tuache ubabaisha katika kuongoza soka hapa ndani lazima tujirekebishe tufanye soka la nyumbani liwe la ushindani na tuwe na nizamu sambamba na kuwa na watu wa mpira kweli ambao watafata kanuni na sheria zinazoongoza soka”Alisema Bushir.
 
Makamo wa rais wa ZFA Ali Muhammed.
Amesema kuwa umefika wakati sasa kwa Zanzibar kutengeneza katiba ambayo itakuwa imara na yenye kuangalia masilahi ya soka la Zanzibar nakuwataka viongozi wa vilabu kuwa na viongozi wanaongoza vilabu vyao wenye uweledi wakuendesha shughuli za mchezo wa soka ilikuendesha timu zao katika misingi iliyoimara.


Akizungumzia soka la vijana kocha huyo amewataka viongozi wa ZFA kuandaa mfumo nzuri ambao utasaidia kukuza soka la Zanzibar nakupelekea kuwa na timu za taifa imara katika miaka mitano ijayo.

NINAENDA YANGA KUPAMBANA ,NINJA.


Mlinzi mpya wa timu ya Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja" amesema mara baada yakufanikiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na timu ya Yanga ya Dar es salam kwa sasa anajipanga kuona anapata namba ya uhakika katika kikosi hicho chenye maskani yake katika mtaa wa Jangwani.

Ninja ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na zenjsport -on line nakusema anajua atakabiliana na changamoto katika kikosi hicho lakini atahakikisha anajituma ili awe chaguo namba moja la kocha wa kikosi chake hicho kipya.
 
Abdallah Haji Shaibu "Ninja"
Amesema moja ya ndoto zake nikucheza katika timu kubwa lakini kufika kwake yanga ni miongoni mwa njia zakufikia kule alikojipangia.
 “Yanga ni kama njia kwangu yakusonga mbele zaidi lengo langu nikucheza soka nje ya Tanzania naamini kujituma kwangu ndiko kutakakosaidia kufikia malengo yangu “Alisema Ninja.

Aidha nyota huyo amewaomba mashabiki wa soka visiwani na wapenzi wake kumuombea dua ilikufanikisha malengo yake aliyojiekea nakusema kuwa atahakikisha anapambana ipasavyo ilikufikia malengo yake.


Ninja ndie mchezaji wa kwanza msimu huu wa mwaka 2017-2018 kusajiliwa Yanga akitokea Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar ambapo amefunga mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

SURE BOY ANG’ARA ,MLANDEGE IKIIFUNGA TAIFA.

Mchezaji wa timu ya Azam FC Abuabakary Sure boy ametokea nyota wa mchezo(man of the match) katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Coconut FM Ndondo cup mtanange uliovurumishwa katika dimba la Amani mjini Unguja usiku wakuamkia leo.
Kikosi cha Mlandege 

Mtanange huo ambao ulikuwa na ushindani na mvuto kwa washabiki waliofika uwanjani hapo huku ukishuhudiwa na mlinzi  wa Liverpol ya England Mamadou Sakho ulikuwa na ushindani wa hali ya juu.

Katika mchezo huo ambao umeshuhudiwa na mashabiki kadhaa magol ya Mlande yalifungwa na Abdallah Edi Mundo dakika ya 60 na Razak Halfan dakika ya 78.

Huku goli pekee la Taifa limekifungwa na Ali Badru dakika ya 30.


Mashindano ya Coconut Ndondo Cup yanatarajiwa kuendelea baada yakumalizika sherehe za Idd.

Thursday, 22 June 2017

FEREJI SALUM AREJEA UWANJANI.

Kiungo wa timu ya Jang’ombe boys Ferej Salum(Ozil) amerejea uwanjani baada yakukaa nje kwa takribani miezi mitatu kuuguza majeraha ya goti.
Kiungo Ferej Salum wakati alipokuwa Villa United

Fereji ambae amesajiliwa Jang’ombe boys katika kipindi cha dirisha dogo akitokea Villa United nakushindwa kuitumikia timu yake hiyo mpya katika michezo ya ligi kuu kutokana na majeraha hayo aliyoyapata katika michezo yakujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu soka ya Zanzibar.

Kiungo huyo ambae alikuwa majeruhi ameanza kurudi uwanjani katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya combine ya Rolling Stone na timu yake mchezo ambao umefanyika usiku wakumkia leo na kuonesha kiwango cha hali ya juu.

Akizungumza na mtandao huu kiungo huyo ameeleza kuwa anafurahishwa na hali ya afya yake nakuwaomba wadau na wapenzi wa soka wazidi kumuombea ili hali yake iwe vizuri zaidi.
Ferej Salum akiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha Azam B.

Ameongeza kuwa baada yakukaa juu kwa takribani miezi mitatu kwa sasa anatahakikisha anafanya mazoezi ya nguvu ilikurudisha kiwango chake nakuisadia timu yake kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka ya Zanzibar.


Nyota huyo ambae pia alipitia katika kituo cha soka cha Azam amesema kwa sasa akili yake yote anaielekeza katika kurejesha kiwango chake nakuachana na kila aina ya anasa ilikufikia malengo ambayo amejiekea.

JKU YAHAHA KUTAKA HUDUMA YA BOBAN.

Timu ya JKU inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar imepania kuona wanapata huduma ya kiungo mshambuliji wa Miembeni City HarounAbdallah Jabir(Boban).
 
Kiungo anefukuziwa na timu ya JKU Haroun Abdallah Jabir(Boban)
Boban ambae alikuwa chachu ya mafanikio ya timu yake katika msimu uliomalizika wa ligi timu ikiwa inashiriki ligi daraja la kwanza taifa  nakufanikiwa kuipandisha ligi kuu amekuwa akifuatiliwa na timu hiyo kwa kipindi kirefu sasa.

Akizungumza na mtandao huu katibu wa JKU Saad Ujudi amesema mwalimu amependekeza jina la nyota huyo tokea msimu uliopita lakini jitihada zakunasa saini ya nyota huyo ikashindikana lakini bado wanahitaji huduma ya nyota huyo.
 
Kiungo wa miembeni City ,Haroun Abdallah Jabir(Boban) 
Ameongeza kuwa bench la ufundi la timu yake wamependekeza tena jina la nyota huyo kujumuishwa katika usajili wa msimu ujao wa ligi na tayari wameshatumwa watu kufuatilia suala hilo kwa hatua ya awali.

“Tulimuhitaji nyota huyu tokea msimu uliopita lakini ilishindikana kutokana na kuhitajika na timu yake,na msimu huu pia mwalimu aliyopo amependekeza jina lake na sisi kama uongozi tushaanza taratibu za awali zakufuatilia uwezokano wa nyota huyo kujiunga na kikosi chetu”Alisema katibu huyo.

Mtandao huu umemtafuta mkurugenzi wa ufundi wa timu ya Miembeni City, Ali Muhammad kujua kuwa tayari kuna ofa yoyote ile kutoka kwa JKU nakusema mpaka sasa hakuna ofa yoyote ile iliyokuja kutoka kwa timu hiyo.
 
Bobani akiwa na jezi ya timu ya Zanzibar ya shule za msingi.
Amefafanua kuwa JKU waliwafata katika msimu ulimalizika kutaka kumchukua nyota huyo lakini hawakufikia makubaliano kutokana na timu kumuhitaji nyota huyo.

Aidha ameweka bayana kuwa timu yao inakaribisha mazungumzo na timu yoyote ile na endapo watafikia makubaliano wapo tayari kumuachia nyota wao yoyote kuenda timu yoyote ile inayomtaka.






BABY,PRINCE ,TIOTE,MKOKO,WASHINDWA KUISAIDIA COMBINE YA ROLLING STONE,YALAZIMISHWA SARE NA BOYS.

Wakiwa katika kujiandaa kwa ajili ya mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kufanyika July 9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara mabingwa watetezi wa mashindano hayo Combine ya wilaya ya mjini usiku wa jana wamejitupa katika dimba la Amani kukipiga mchezo wa kirafiki na timu ya Jang’ombe.
Nyota wa combine ya wilaya ya mjini baada yakumalizika kwa mchezo kati ya timu ya Jang'ombe boys na timu hiyo.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wakuvutiwa mabingwa hao wamelazimishwa sare yakutokufanga.

Akizungumzia mchezo huo kocha masaidizi wa timu hiyo Ramadhani Madundo amesema mchezo ulikuwa nzuri na waushindani huku akifurahishwa na kiwango kilichoonesha na vijana.
Wachezaji wa combine ya wilaya ya mjini.


Kocha huyo ameongeza kuwa kwa sasa walimu wa timu hiyo hawaangalii ushindi bali wanachoangalia ni namna gani  vijana wao wanayafanyia kazi yale wanayowaelekeza katika mazoezi.

Amewataka wadau na wapenzi wa soka visiwani kutoka michango yao ya hali na mali ilikufanikisha safari yao hiyo huku wakiamini kuwa vijana hao watakuja na ushindi.
Gulion FC.


Mjini watacheza mchezo mwengine wa kirafiki leo Alhamis kuanzia saa 10:15 za jioni dhidi ya timu ya Gulioni ambayo inashiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.

Wednesday, 21 June 2017

TUKIWEKEZA KWA VIJANA TUTAPIGA HATUA KIMICHEZO,MKOKO.

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya habari utamaduni utalii na michezo,baraza la michezo ,wizara ya elimu na mafunzo ya amali kwa kushirikiana na chama cha mpira wa miguu visiwani ZFA vimeshauriwa kuelekeza nguvu zao  katika kusaidia na kuendeleza michezo kwa vijana ilikutengeza taifa lililobora kimichezo.
Mshambuliaji wa Serengeti boys Ibrahim Abdallah Mkoko akiwa katika majukumu ya taifa .

Ushauri huo umetolewa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania ya chini ya miaka 17 Serengeti boys Ibrahim Abdallah(Mkoko) wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema kuwa endapo serikali na wadau wakuu wa michezo wataekeza kuanzia chini Zanzibar itatajika kwa michezo kimataifa.

Amesema nchi zote ulimwenguni ambazo zimepiga hatua kimichezo wameekeza kwa vijana jambo ambalo limeweza kuzisaidia nchi hizo kiuchumi.
Baadhi ya vijana wakizanzibar wakionesha uwezo wao wakusakata kabumbu.

Ameongeza kuwa Zanzibar imebahatika kuwa na vijana wengi wenye vipaji katika michezo mbali mbali lakini kutokuwepo kwa sera nzuri yakukuza,kuendeleza na kuimarisha vipaji vya vijana hao ndiko kunakopelekea kudumaa kwa vipaji vya vijana hao.

Amepongeza mpango wa wizara ya elimu wakuwa na mfumo wa mashindano ya elimu bila malipo ambayo husirikisha wanamichezo kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari nakutoa nafasi kwa vijana kuonesha uwezo wao,nakushauri vijana ambao wataonesha vipaji katika michezo hiyo kuendeleza zaidi ilikuepusha kudumaa kwa vipaji walivyo navyo.

“ Huu utaratibu unaofanya na wizara ya elimu wakuandaa haya mashindano ya elimu bila ya malipo ni nzuri lakini uwepo mpango wakukusanywa wale wote wenye uwezo ilikuendelezwa vipaji walivyonavyo ili visije kupotea”Alisema Mkoko.

Kuhusu Zanzibar kupatiwa uwanachama wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Mkoko amesema ni jambo jema na litasaidia kutoa fursa kwa vijana wakizanzibar kujitangaza huku akikiomba chama cha mpira wa miguu visiwani kuanza maandalizi ya mapema kwa timu zake ambazo huenda zikaanza kushiriki katika mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na shirikisho hilo.

“Nimefarijika sana Zanzibar kupata uanachama wa shirikisho la soka barani Afrika huu ni wakati wa vijana wa kizanzibar kutangaza vipaji vyao kimataifa jambo la msingi na la umuhimu nikwa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kuanza maandalizi ya timu zake mapema ilikuona wanafanya vyema katika mashindano wakati utakapowadia”Alisema.

Akizungumza malengo yake katika soka Mkoko amesema ndoto zake ni kucheza soka lakulipwa lakini kwa sasa atahakikisha anafanya mazoezi kwa bidii kuona anaisadia timu yake anayochezea kwa sasa.

“Unajua lengo nikucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania lakini ili upate nafasi yakufika huko lazima ufanye bidii katika mazoezi,uwe na nidhamu ya hali ya juu nakujituma katika mashindano,kwa sasa naaendelea kujinoa kwa ajili ya haya mashindano ya Rolling Stone lakini nikirudi huko nitaelekeza nguvu zangu katika timu yangu,unajua msimu uliomalizika sijapata kuitumikia sana kilabu yangu kwa vile nilikuwepo katika kambi ya timu ya taifa lakini msimu huu nitahakikisha naisaidia timu yangu kwa nguvu zangu zote”Alimaliza Mkoko.



SINA MPANGO WAKUONDOKA MIEMBENI CITY,PRINCE,

Mshambuliaji nyota wa timu ya Miembeni City,Muhamed Vuai Prince amesema kwa sasa hana mpango wakuhama katika kikosi hicho huku akielekeza nguvu zake kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi.
 
Mshambuliaji wa timu ya Miembeni City ,Muhamed Vuai Prince akiwa katika mizunguko yake katika mitaa ya Vuga mjini Unguja.
Prince ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema kuwa baada yakuisaidia timu hiyo kupanda ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018 kwa sasa anajipanga kuona anaisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ambapo watashiriki kwa mara ya kwanza.

“Tulikuwa na msimu nzuri tumefanikisha kuipandisha timu ligi kuu nashukuru nilikuwa chachu ya ushindi katika timu yangu kwa sasa najipanga kuona nafanya zaidi kile nilichokifanya katika msimu uliopita ilikuisadia timu yangu kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka ya Zanzibar katika msimu wa 2017-2018 ambao timu itashiriki kwa mara ya kwanza”Alisema Prince.
 
Muhamed Vuai Prince akiwajibika katika moja ya michezo ya ligi daraja la kwanza taifa Unguja.
Ameongeza kuwa licha yakuwepo kwa taarifa kadhaa juu ya nyota huyo kuondoka katika kikosi hicho,mshambuliaji huyo amesema yeye binafsi huzisikia taarifa hizo kutoka kwa watu bali hajafanya mazungumzo na timu yoyote huku kwa sasa akili yake akiielekeza katika kuisadia timu yake hiyo kufanya vyema katika msimu ujao wa ligi.

Amefafanu kuwa mkataba wake wa Miembeni City umesalia misimu miwili hivyo haoni haja yakufanya mazungumzo na timu yoyote ile bali lililobakia kwa sasa nikufanya mazoezi kwa bidii kubwa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.

Ameelezea kufurahishwa kwake na mazingira yaliyopo katika kikosi hicho huku akifurahishwa na mashirikiano aliyoyapata katika msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi hicho kutoka kwa wachezaji wenzake sambamba na uongozi wa timu hiyo.

Prince ambae amemaliza msimu wa ligi 2016-2017 akiwa kinara wakufumania nyavu katika kikosi cha Miembeni City kumekuwa na taarifa yakutakiawa na vilabu kadhaa visiwani ikiwemo taifa ya Jang’ombe.




Monday, 19 June 2017

Bushir ,apendekeza nyota 4,Mwadui fc,wawili wakitokea Zanzibar.

Aliyekuwa kocha wa timu ya KMKM inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar Ali Bushir Mahmoud amekishauri chama cha mpira wa miguu visiwani kutumia njia za busara katika kufanikisha kupatikana kwa timu 12 zitakazoshiriki ligi kuu soka kwa msimu ujao wa ligi.
Kocha wa timu ya Mwadui Ali Bushir Mahmoud.

Bushir ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema kuwa busara kwa viongozi wa vilabu sambamba na wale wa ZFA inahitajika katika kufanikisha suala hilo.

Ameongeza kuwa endapo viongozi wa vilabu sambamba na wale wa ZFA wataeka pembeni masilahi binafsi nakuangalia zaidi manufaa ya taifa vilabu 12 vitapatikana bila hata ya malumbano na migogoro.

Kuhusu suala la vilabu vilivyopanda ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018 kocha huyo amesema si busara vilabu hivyo kuviunganisha na vile vilivyopo ligi kuu katika msimu uliopita katika mchako wakutafuta timu hizo bali zijumuishwe kucheza ligi kuu kama kanuni iliyoendesha mashindano inavyosema.

“Mimi nasikia mijadala mingi sana kama kuna ligi ndogo tusubiri tuone kama itakuwepo hiyo ligi ndogo au vilabu na viongozi wa ZFA watakuja na njia nyengine zakupatikana timu 12 mimi binafsi suala lakuchezwa ligi dogo kwangu sioni kama kuna tatizo sana ila hizi timu kama Miembeni City na Charawe sambamba na zile mbili za kule Pemba ambazo zimepanda ligi kuu kwa msimu wa 2017-2018 kwa mujibu wa kanuni sioni sababu yakujumusha hapa ,kama watacheza na wenyewe kwa wenyewe waliopanda kutafuta timu mbili zakupanda badala ya nne nahisi inaweza kuwa njia sahihi lakini kuwacheza na wale waliopo kwenye ligi si jambo sahihi kwa muono wangu”alisema kocha huyo.

Aidha amewaomba viongozi wanaongoza soka la Zanzibar kusimamia sheria zinazoongoza soka nakujaribu kufanya  mazungumzo na baadhi ya makampuni ilikuona haja yakufadhili ligi kuu soka ya  visiwani ilikuongeza mvuto na ushindani katika ligi hiyo.

Akizungumzia ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara akiwa na timu ya Mwaduwi yaShinyanga kocha huyo amesema ligi hiyo inaushindani zaidi ukilinganisha na ile ya nyumbani Zanzibar huku akiongeza kuwa ushindi umeongezekana zaidi kutokana na ufadhili ambao upo katika ligi yao.

Amefafanua kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na nyota wawili wanaokipiga ligi kuu soka ya Zanzibar ambapo ni mlinda mlango sambamba na kiungo mkabaji ambapo bado hajataka kutaja majina ya nyota hao kwa vile mazungumzo kati ya viongozi wa Mwadui na nyota hao bado hayajafanyika.

MACHUPA KUENDESHA KOZI YA MAKOCHA WA MAGOLIKIPA.

Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kinatarajiwa kuandaa kozi ya ukocha wa magolikipa kozi ambayo inatarajiwa kufanyika Juni ,28 mwaka huu.

Mkufunzi wa kozi ya makocha wa makipa Saleh Machupa.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa chama cha mpira wa miguu visiwani Ali Bakar amesema kozi hiyo ya ukocha wa magolikipa inatarajiwa kuendeshwa na mkufunzi anaetambuliwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF, Saleh Machupa.

Ameongeza kuwa kozi hiyo itajumuisha makocha wa magolikipa wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar,ligi daraja la kwanza taifa na la pili taifa.


Aidha amesema kuwa katika msimu ujao wa ligi timu ambayo haitakuwa na kocha wa magolikipa mwenye cheti timu hiyo itaondolewa katika mashindano kulingana na kanuni ambayo itatumika katika mashindano hayo.

Amefafanua kuwa kozi hizo za makocha wa magolikipa itakuwa ikiendeshwa kila kipindi kutokana na mahitaji yananafasi hizo visiwani

VILABU KUKUTANA KUJADILI MFUMO WA LIGI KUU KWA MSIMU 2017-2018.

Viongozi wa vilabu 28 vya soka vinavyoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar vinatarajiwa kukutoka katika ukumbi wa mikutano uwanja wa Gombani kisiwani Pemba kujadili njia ambazo zitatumika kupatikana kwa timu 12 zitakazoshiriki ligi kuu kwa msimu wa 2017-2018.
Makamo wa rais wa ZFA Ali Muhamed.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa chama cha mpira wa miguu Ali Bakar mbele ya wanahabari imesema  viongozi hao wanatarajiwa kukutana July ,8 mwaka huu.

Cheupe amesema kuwa mkutano mkuu wa chama cha mpira wa miguu visiwani uliokutana mwezi mmoja uliopita umebariki msimu ujao wa ligi uwe na timu 12 hivyo kukutana na vilabu husika ndiko kutakapotoa fursa ya njia gani ambayo itapelekea kupatikana kwa vilabu vinavyohitajika katika ligi hiyo.


Ameongeza kuwa maamuzi ambayo yatafikiwa katika mkutano huo wa viongozi wa vilabu ndiyo yatakayopelekwa katika mkutano mkuu wa chama hicho nakupelekea kupatikana kwa timu zitakazoshiriki katika michezo hiyo.

Saturday, 17 June 2017

Uongozi Miembeni City, kutoa mkono wa Idd kwa nyota wake.

Bodi ya wakurugenzi wa timu ya Miembeni City kesho wanatarajiwa kukutana na nyota wanaokipiga katika kikosi hicho kwa lengo lakutoa mkono wa Idd kwa nyota wao hao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na rais wa timu hiyo Seif Kombo imesema kwamba huo ni utaratibu ambao upo katika kikosi chao hicho kila ifikapo mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwakusanya nyota wao hao kwa lengo lakuwapatia fedha ilikujitafutia huduma ambazo zitawasaidia kwa ajili ya Idd.

Ameongeza kuwa baada ya kikao cha bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo kilichokutana asubuhi ya leo kimekubaliana kutoa fedha hizo kwa nyota wao ilikufanya nyota hao kuwa na siku njema ya Idd.

“Huu ni utaratibu ambao tumejiekea kuwapatia fedha nyota wetu kila ifikapo mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ilioneshana upendo kati ya viongozi wa timu na wachezaji wetu waliopo katika kikosi chetu hicho”alisema rais huyo.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chao kuelekea msimu ujao wa ligi rais huyo amesema baada yakumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani wataanza maandalizi ya msimu mpya  wa ligi kulingana na maelekezo ya mwalimu wa kikosi chao hicho.


Kuhusu suala la usajili rais huyo amesema  mwalimu amependekeza nafasi ambazo zinahitaji kufanyiwa marekebisho sambamba na wachezaji ambao waache katika kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Thursday, 15 June 2017

RATIBA YA LIGI YA MABINGWA WA WILAYA UNGUJA 2016/2017




KUNDI A:                                   KUNDI B:                                KUNDI C:                             KUNDI D:
MLANDEGE (MJINI)                    KIANGA INT (MAGH. “A”)            NEW KING (KASK.“A”)           NYANGOBO (MAGH.“B”)
NEWPOWER (KATI)                    AFRICAN BOYS(KASK.”B”)          SUPER TIGER (KATI)           UHURU (KUSINI)          
MAPINDUZI (KUSINI)                  SHINGWI HEROES (KASK.“A”)     FUJONI (KASK.B)                 MFENESINI (MAGH.“A”)
AZIMIO (MAGH. “B”)                    KWEREKWE CITY(MJINI) 
SIKU
TAREHE
M
MCHEZO
GR
MUDA&UWANJA
1ST  ROUND
IJUMAA
07/7/2017
1
AZIMIO        VS MLANDEGE
A
SAA 10:00  JIONI AMAAN
JUMAMOSI
08/7/2017
2
MAPINDUZI VS NEW POWER
A
SAA 10:00  JIONI AMAAN
JUMANNE
11/7/2017
3
KIANGA INT VS SHINGWI HEROES
B
SAA 10:00  JIONI AMAAN
JUMATANO
12/7/2017
4
AFRICAN B       VS KWEREKWE CITY
B
SAA 10:00  JIONI AMAAN
JUMAMOSI
15/7/2017
5
NEW KING        VS SUPER TIGER
C
SAA 10:00  JIONI AMAAN
JUMAPILI
16/7/2017
6
UHURU           VS NYANGOBO
D
SAA 10:00  JIONI AMAAN
2ND ROUND
JUMATANO
19/7/2017
7
NEW POWER     VS   AZIMIO
A
SAA 10:00  JIONI AMAAN
ALHAMIS
20/7/2017
8
MLANDEGE       VS   MAPINDUZI
A
SAA 10:00  JIONI AMAAN
JUMAPILI
23/7/2017
9
AFRICAN B        VS   KIANGA INT
B
SAA 10:00  JIONI AMAAN
JUMATATU
24/7/2017
10
KWEREKWE C   VS  SHINGWI HEROES
B
SAA 10:00  JIONI AMAAN
ALHAMIS
27/7/2017
11
SUPER TIGER     VS  FUJONI
C
SAA 10:00  JIONI AMAAN
IJUMAA
28/7/2017
12
MFENESINI         VS  NYANGOBO
D
SAA 10:00  JIONI AMAAN



3RDROUND
JUMATATU
31/7/2017
13
MAPINDUZI            VS     AZIMIO
A
SAA 8:00   MCHANA AMAAN
JUMATATU
31/7/2017
14
NEWPOWER           VS    MLANDEGE
A
SAA 10:00  JIONI AMAAN
JUMANNE
01/8/2017
15
KWEREKWE C        VS    KIANGA INT
B
SAA 8:00   MCHANA AMAAN
JUMANNE
01/8/2017
16
SHINGWI HEROES VS    AFRICAN BOYS
B
SAA 10:00  JIONI AMAAN
IJUMAA
04/8/2017
17
FUJONI                   VS    NEW KING
C
SAA 10:00  JIONI AMAAN
JUMAMOSI
05/8/2017
18
UHURU                    VS    MFENESINI
D
SAA 10:00  JIONI AMAAN