Thursday, 31 August 2017

Miembeni City ,mapumzikoni hadi September 4.

Kocha mkuu wa timu ya Miembeni City Muhamed Seif King ametoa mapumziko ya siku tano kwa wachezaji wa timu hiyo ilikutoa nafasi kwa nyota hao kusherehekea skukuu ya ld el hajj ambapo waislam wote ulimwenguni waatarajiwa kusherehekea hapo kesho.
Kocha mkuu wa timu ya Miembeni City Muhamed Seif King akizungumza na nahodha wa timu hiyo Habibu 

King ametoa mapunziko hayo baada ya ushindi wa magol 4-1 dhidi ya Chuoni ikiwa ni miongoni mwa michezo ya kirafiki kwa timu hiyo ambayo ipo katika kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2017-2018 ligi kuu soka ya Zanzibar.

Akizungumza na wachezaji hao kocha huyo amesema wamecheza michezo mitatu ya kirafiki lengo kuu kwake nikuangalia mfumo ngani anaweza kuutumia katika kikosi chao hicho ambacho kimesheni nyota vijana na wenye uwezo wakusakata kabumbu.

Amesema michezo hiyo imemuonesha mapungufu ambayo vijana wake wanayo na atahakikisha anayafanyia kazi  ilikuwa na kikosi kilicho imara na bora.


Miembeni City ambayo itashiriki kwa mara ya kwanza ligi kuu soka ya Zanzibar imecheza michezo mitatu ya kirafiki ambapo waliifungwa Mchangani magol 3-0,wakatoka sare ya goli 1-1 na timu ya New King nakuibuka na ushindi wa magol 4-1 dhidi ya Chuoni wanatarajiwa kurudi mazoezi Jumatatu Sepember 4 kuendelea kujiandaa na msimu ujao wa ligi.

Wednesday, 30 August 2017

MUEMBELADU YANYEMELEA HUDUMA YA BUSHIR

Aliyekuwa kocha wa timu ya Mwadui FC inayoshiriki ligi kuu soka ya Vodacom Tanzania bara Ali Bushir amekuwa akifuatiwa kwa karibu na timu ya Muembeladu inayoshiriki ligi daraja la pili wilaya ya mjini Unguja.
 
Kocha Ali Bushir wa kwanza alieva kapelo akiwa katika moja ya michezo ya Kagame wakati akiifundisha KMKM.
Muembeladu ambayo iliwahi kupata huduma ya mwalimu huyo huko nyuma imepania kuona wanapata huduma ya kocha huyo ilikukinoa kikosi chao hicho. Akizungumza na mtandao huu msemaji wa timu hiyo Said Mussa amesema uongozi wa timu hiyo tayari umeshafanya mazungumzo na mwalimu huyo na mazungumzo yameenda vizuri.

Amesema kuwa lengo la timu yao nikuona inapanda daraja na ilikufikia lengo lao hilo walilojiekea wakaona umuhimu wakutafuta mwalimu ambae anauwezo nakufanikisha lengo lao hilo.

Kwa upande wake kocha Ali Bushir amesema ni kweli amefanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo na anajipanga kufanya kazi na uongozi wa timu hiyo kwa mujibu wa makubaliano yao.


Amesema ataenda kuisaidia timu hiyo kwa vile mipango yake nikufundisha soka Tanzania bara lakini kutokana na mipango yake yakuenda huko haijakaa vizuri ameamua kutumia muda wake aliopo hapa mkuwasaidia vijana hao.

Licha ya Muembeladu kocha huyo amekuwa akihitajiwa na timu kadhaa visiwani hapa lakini ameshinda kufanya nao mazungumzo kutokana na malengo yake nikuenda kufundisha soka Tanzania bara.


Saturday, 26 August 2017

TUTAHAKIKISHA TUNAZIFANYIA KAZI KASORO ZILIZOJITOKEZA MSIMU ULIOPITA,MZIRAI.

Kamati inayosimamia mashindano ya vijana ndani ya wilaya ya mjini Unguja imejipanga kuona wanazifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika mashindano ya msimu uliopita ili zisijirejee tena katika msimu mpya wa mashindano hayo.

Hayo yameelezwa na mshika fedha wa kamati ya mashindano ya vijana ndani ya wilaya hiyo Mussa Habibu Mzirai wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema katika mashindano yaliyomalizika kulikuwa na kasoro kadhaa ambazo zimepelekea kutia dosori mashindano hayo.

Amesema moja ya changamoto ambazo kamati yake imekabiliana nazo katika msimu uliopita ni pamoja na vitendo vya upangaji wa matokeo,mashindano kutokumalizika kwa wakati na uhaba wa viwanja jambo ambalo kamati yao kwa msimu 2017-2018 itahakikisha changamoto hizo hazijitokeze.

Akizungumzia suala la upangaji wa matokeo Mzirai amesema vitendo hivyo vilijitokeza mwishoni mwa mashindano ya Central nakuahidi kutoa adhabu kali kwa yoyote yule atabaaini na vitendo hivyo katika msimu ujao.

Kuhusu zoezi la uhamisho na usajili linaloendelea amesema zoezi hilo linaenda vizuri huku muamko wa vilabu ukionekana kuwa mkubwa.


Amewaomba wadau wa wapenzi wa mchezo wa mpira wa miguu kujitokeza kuunga mkono jitihada za kamati yao ilikuyafanya mashindano hayo yawe na mvuto na ushindani zaidi.

NITAPAMBANA KWA NGUVU ZANGU ZOTE KUIBUKA KINARA WAKUFUMANIA NYAVU LIGI KUU,NADO.

MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Miembeni City Feisal Riyadh Nado, ameahidi kuibuka mfungaji bora wa michuano ya ligi kuu soka ya Zanzibar inayotarajiwa kuanza October mwaka huu.
Feisal akiwa na rais wa Miembeni City.

Feisal aliyesaini mkataba wa miaka mitatu ni miongoni mwa washambuliaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao akitokea Chukwani United alikofunga mabao 22 msimu uliopita..

Akizungumza na mtandao huu Feisal alisema kuwa anafuraha kujiunga na Miembeni City na kudai alikuwa na ndoto ya muda mrefu kujiunga na miamba hiyo ya soka visiwani hapa.

“Kwa kweli nimejipanga kufanya vizuri zaidi kuliko msimu uliopita, natarajia Mwenyezi Mungu atanijalia kila mechi nipate nafasi yakucheza, niweze kufunga na kuwa mfungaji bora wa ligi,” alisema Feisal.

Mshambuliaji huyo ambae atacheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha City , hakusita kuisifia timu hiyo akisema kuwa amefurahishwa na namna inavyojali wachezaji wake.

“Kufika Miembeni City ni njia moja ya mimi kusonga mbele, hivyo nina mpango wa kucheza soka la kulipwa katika timu kubwa zaidi, ila hauwezi kwenda kucheza huko bila kujituma mazoezini pamoja na kwenye mechi, nina imani nitafika huko,” alisema.

Feisal ambaye anavutiwa na staa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno ,Cristiano Ronaldo, amewapa ahadi mashabiki wa Miembeni City kuwa timu hiyo itafanya vizuri msimu ujao huku akiwaoamba waisapoti zaidi timu hiyo.


Hivi sasa straika huyo hatari mwenye spidi na uwezo wa kupachika mabao, ameshacheza mchezo mmoja na Miembeni City nakuifungutia timu yake hiyo mpya goli moja katika ushindi wa magol 3-0 dhidi ya mchangani.

ZFA YAZIPITIA FOMU ZA UHAMISHO NA USAJILI,

Kamati tendaji ya chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar imekutana na vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka kupitia fomu za usajili na uhamisho kwa ajili ya msimu wa 2017-2018.

Akizungumza na waandishi wa habari afisa habari wa chama cha mpira wa miguu visiwani hapa Ali Bakar amesema zoezi hilo limekuja baada yakukamilika kwa zoezi la usajili na uhamisho lililoanza tarehe 17 mwezi wa saba na kukamilika 17 Agosti nakumalizika kwa mafanikio makubwa.

Amesema kuwa zoezi la upitiaji wa fomu hizo limeenda vizuri huku madai kadadha yakasikilizwa kutokana na baadhi ya wachezaji kusajili timu mbili.

Akizungumzia baadhi ya kadhia ambazo zimejadiliwa ni pamoja na suala la mlinzi wa kati wa Miembeni City ambae amesajiliwa na Mlandege Abubakary Ame ambapo kamati tendaji imerizishwa na hoja ya Miembeni City na nyota huyo kuidhinishwa kukipiga katika timu ya Miembeni City.

Sambamba na hayo kamati hiyo pia imesikiliza madai ya Hassan Seif banda ambae pia ameidhinishwa kukipiga katika timu ya Jang’ombe Boys.


Aidha Cheupe amewataka viongozi wa vilabu kufanya maandalizi yaliyo mazuri ilikuifanya ligi kuu kwa mismu wa 2017-2018 iwe ya ushindani na mvuto wa hali ya juu.

Thursday, 24 August 2017

Nitahakikisha najituma kuisaidia Miembeni City kutwaa taji la msimu ujao,Haroun.’

Kiungo hatari wa timu ya Miembeni City , Haroun Abdallah Jabir(Boban)  ameweka wazi kuwa yupo tayari kwa mapambano.
Kiungo wa Miembeni City Haroun Abdallah Boban.
Haroun amedai kuwa moja ya malengo yake ni kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu ujao.
“Kuanza kwa msimu mpya 2017-2018, kwangu mimi nimejipanga kuisaidia timu yangu kuwa mabingwa msimu ujao na mwenyewe kucheza vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kwani ushirikiano wetu ndio utatupa hamasa kama wachezaji ya kufanya vizuri na kuisaidia timu yetu kubeba ndoo (ubingwa),” alisema Haroun wakati akizungumza na mtandao wa huu.

Haroun ni mmoja wa viungo wanaokuja kwa kasi kwa sasa Zanzibar, na amekuwa akiwania na vilabu kadhaa visiwani hapa.

Akizungumzia ujio wa Banka ,Guti na Neymar katika kikosi chao  Haroun amesema ujio wa nyota hao kikosini hapo kutasaidia zaidi timu hiyo kufanya vyema huku akisisitiza kuwa kujituma katika mazoezi sambamba na nakuyafanyia kazi maelekezo ya mwalimu mchezoni ndiko kutakakoisaidia timu yao hiyo kufanya vyema katika ligi hiyo.

Sambamba na hayo Haroun amesema kuwa ligi kuu soka ya Zanzibar ni miongoni mwa ligi ngumu dunia kwa vile inashusha timu nyingi ukilinganisha na idadi ya timu shiriki hivyo inahitajia wachezaji wa timu yao kulijua hilo nakujituma zaidi hasa katika kipindi hiki cha maandalizi.


Miembeni City inaendelea kujinoa kujiandaana msimu ujao wa ligi ambapo kwa mara ya kwanza kikosi hicho kinashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar.

Monday, 21 August 2017

ZFA WAMLILIA DR. KUKU.

Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa daktari wa mwanzi wa timu ya taifa ya Zanzibar Abdallah Said Mohammed al-maaruf ‘Kuku’, aliefariki dunia Agosti 20, 2017 nyumbani kwake Muembetanga mjini Zanzibar.
 
Pichani Jeneza lililobeba mwili wa marehemu likitolewa Msikiti Maiti, Michenzani baada ya kusaliwa. ( picha ndogo kushoto marehemu Abdalla Said enzi za uhai wake) .Picha kwa msaada wa mtandao wa bin zubery.

Akizungumza na mtandao huu makamo wa rais wa ZFA Pemba  Ali Muhamed amesema chama chao kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha daktari huyo huku akiwataka wote walioguswa na msiba huo kuwa na subra katika kipindi hiki cha msiba.

Amesema marehemu katika uhai wake alijitolea kwa hali na mali katika kuwahudumia wachezaji wanapopata matatizo yanayowafanya wasiendelea na mazoezi.

Ameongeza kuwa marehemu alikuwa akifanya kazi kwa ushirikioano bila yakujali kuwa anapata chochote au hapati bali alikuwa akihakikisha anaitumia taaluma yake ipasavyo.

Aidha chama chao kiungana na familia ya marehemu Abdallah Said katika kipindi hiki cha msiba nakuwaomba wanzazibar kumuombea dunia ili Allah ampokea akiwa miongoni mwa waja wema.


Marehemu amezikwa jana mchana kijijini kwao Fujoni Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, ambapo mazishi yake yalihudhuriwa na mamia ya wananchi wa Zanzibar wakiwemo wanamichezo, madaktari na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali alizozifanyia kazi ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) akihudumu katika kiwanja cha kufurahisha watoto Kariakoo kilicho chini ya mfuko huo.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahala pema Peponi. Amin.


Mfenisini kuelekea Dar es salam kwa matayarisho ya ligi.

Timu ya Mfenisini ambayo imepanda ligi daraja la pili taifa Unguja inatarajiwa kuelekea Tanzania bara kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata timu hiyo itakapokuwa Tanzania bara itacheza michezo kadhaa yakirafiki yakujipima nguvu ilikukieka sawa kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Mwalimu msaidizi wa timu hiyo Saha ameuambia mtandao huu kwamba baada yakukamilisha kwa usajili wa nyota wapya wa kikosi hicho kinachofata nikukiandaa kikosi chao hicho kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ambapo timu itashiriki kwa mara ya kwanza.

Amewataka washabiki na wapenzi wa timu yao hiyo kuwaunga mkono ilikufanya vyema katika msimu mpya wa ligi nakuweza kupanda daraja.





Halid Boffu kitasa cha Miembeni City kuungana na wenzake kesho.

Mlinzi wa kati mpya wa timu ya Miembeni City inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar  Khalid Boffu aliesajiliwa akitokea Academy ya Twalipo anatarajiwa kuwasili asubuhi ya kesho akitokea Dar es salam tayari kujiunga na timu yake kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Halid Boffu akijifua katika fukwe  za bahari Boffu atajiunga na wenzake mwishoni mwa wiki hii.

Khalid ambae ni mdogo wa mshambuliaji wa zamani wa timu ya JKU Ruvu Sele Boffu anatarajiwa kuwasili visiwani mnamo majira ya saa tatu asubuhi kwa boti za Azam Marine.

Kwa  mujibu wa taarifa zilizopatika kutoka kwa uongozi wa timu hiyo atakapowasili visiwani hapa nyota huyo atapokelewa na rais wa timu hiyo sambamba na viongozi mbali mbali wa timu na natarajiwa kujiunga katika mazoezi na wenzake kesho kutwa.


Miembeni City tayari imeanza maandalizi kwa ajili yakujindaa na ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu 2017-2018.

Miembeni City waanza kujinoa kwa msimu mpya wa ligi.






Sunday, 20 August 2017

Neymar wa Miembeni City kuungana na wenzake wiki hii.

 Mchezaji Ramadhani Khamis Muhamed(Neymar) ambae amesajiliwa na Miembeni City kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Jang’ombe boys anatarajiwa kujiunga katika mazoezi ya timu yake hiyo mpya Agost 24 tayari kujianda na msimu ujao wa ligi kuu soka ya Zanzibar.
 
Ramadhani Khamis Muhamed(Neymar) akiwa na jezi ya timu yake zamani Jang'ombe boys.
Neymar ambae ni miongoni mwa nyota waliong’ara katika msimu wa 2016-2017 ligi kuu soka ya Zanzibar amepewa mapumziko ya wiki moja kabla yakujiunga na wenzake katika mazoezi ya timu hiyo ambayo katika msimu huu wa ligi wanacheza ligi kuu soka ya Zanzibar kwa mara ya kwanza.

Akizungumza na mtandao huu mkuu wa kitengo cha habari wa Miembeni City Ali Khamis amesema mwalimu ameamua kumpa mapumziko hayo kwa sababu nyota huyo hakuapata mapumziko kwa vile alikuwa akiitumikia timu yake katika michezo ya ligi kuu.

“Nikweli tumemsajili Ramadhani Khamis Muhamed (Neymar) kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Jang’ombe boys lakini kwa vile alikuwa akiitumikia timu yake kwenye michezo ya ligi kuu soka ya Zanzibar iliyomalizika wiki iliyopita tumeamua kumpumzisha hadi hapo Agost 24 na hapo ataanza kujiunga na wenzake katika mazoezi.


Nyota huyo ambae alikuwa chachu ya mafanikio kwa timu yake katika msimu uliopita wa ligi kuu soka ya Zanzibar alikuwa miongoni mwa nyota waliounda timu ya combine ya wilaya ya mjini iliyotwaa ubingwa katika mashindano ya Rolling stone mwaka 2016 huko mjini Arusha.

Saturday, 19 August 2017

Dirisha la usajili na uhamisho lafungwa Zanzibar,ZFA yasema itazisimamia sheria na kanuni msimu ujao.

Zoezi la usajili na uhamisho visiwani Zanzibar limemalizika Alkhamis Agost 17 nakuenda vizuri na kinachofata sasa nikupitiwa kwa fomu hizo nakuhalalishwa kwa wachezaji kucheza timu husika.


Akizungumza na mtandao huu katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu Zanzibar Muhamed Tedy amesema kumalizika kwa zoezi hilo chama chao kinajipanga kuzipitia fomu hizo.

“Tutarajia kuzipita fomu hizo kesho Jumapili mbele ya viongozi wa vilabu na tutaanza na ligi kuu lengo nikuondoa utata ambao unaweza kujitokeza katika upitishwaji huo wa fomu” alisema.

Ameongeza katika kuendesha zoezi hili watahakikisha wanafuata kanuni na sheria na mwaka huu chama chao kimejipanga kuona wanatekeleza kanuni kwa asilimia zote.

Kuhusu msimu wa 2016-2017 ambao umefikia tamati hapo jana katibu huyo amesema msimu huo umemalizika kwa mafanikio licha ya changamoto ambazo zimejitokeza katika kuendesha ligi hiyo.

Akizungumzia vitendo vya uoangaji wa matokeo ambavyo vilionekana vikijitokeza katika michezo ya ligi kuu soka ya Zanzibar kwa 2016-2017 katibu huyo amesema chama chao kinajipanga kukomesha vitendo kama hivyo.

Msimu wa ligi 2016-2017 ligi kuu soka ya Zanzibar umemalizka jioni ya jana ambapo timu ya JKU kwa mara ya kwanza wametwaa ubingwa wa ligi hiyo huku Zimamoto wakitwaa nafasi ya pili .



SIMBA YAIRARUA 5-0 GULIONI FC, MAVUGO AONESHA UFUNDI WAKUPASIA NYAVU.

Wakiwa wanaendelea kujiandaa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya watani wao wa timu ya Simba usiku wakuamkia leo imejitupa katika dimba la Amani mjini Unguja kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Gulion FC inayoshiriki ligi daraja la pili wilaya ya mjini Unguja.
 
Wachezaji wa Simba wakisikiliza maelekezo ya walimu wao.
Katika mchezo huo ambao Simba waliutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa wekundu hao wa msimbazi imeibuka na ushindi wa magol 5-0 magoli yaliyofungwa na mshambuliaji Laudit mavugo katika dk ya 13 na 40, Shiza kichuya dk ya 37,Juma luzio dk ya 41 na Mohd Ibrahim,mo akaimalizia karamu ya bao mnamo dakika ya 67.

Simba ambao wameonekana kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa nakuwazidi wapinzani wao huu utakuwa mchezo wa mwisho wa majaribio kisiwani hapa.
 
Kocha wa Gulion Birhani Msoma.
Akizungumzia mchezo huo kocha msaidizi wa timu ya Simba Jackson Mayanja amesema mchezo huo umesaidia kuona kasoro zilizopo katika kikosi chao nakuyafanyia kazi.


Aidha amesema wamejaribu kubadilisha mfumo kwa kuchezesha washambuliaji wawili ilikutengeneza peya kutokana na kukabiliwa na majeruhi kwa baadhi ya nyota wao akiwemo mshambuliaji Bocco na Okwi.

Kwa upande wake kocha wa timu ya Gulion Burhan Msoma amesema wamepoteza mchezo huo kutokana na wachezaji wake kutokuwa imara kimwili.

Simba wanatarajiwa kuondoka visiwani August 22 kuelekea Tanzania bara tayari kuwakabili wapinzani wao Yanga mtanange ambao utavurumishwa August 23 katika uwanja wa taifa Dar es Salam.


Kikosi cha Gulioni FC kilikuwa; Haji Yussuf, Ibrahim Hamisi, Shaaban Hassan, Mohammed Omar, Nuhu Ally, Ulele Uledi, Hamad Kawamba, Ally Mbaraka, Ally Amour, Ally J Kipanga na Fahim Khalfan.

Simba SC; Aishi Manula/EmManuel Mseja, Erasto Nyoni, Ally Shomary/Mohammed Hussein ‘Thshabalala’, Salim Mbonde, Method Mwanjali/Paul Bundala, James Kotei/Jonas Mkude, Haruna Niyonzima/Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin/Said Ndemla, Laudit Mavugo/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Juma Luizio na Shiza Kichuya/Jamal Mnyate. 

Friday, 18 August 2017

Simba kujipima na Gulion FC usiku wa leo.

Timu ya Simba inatarajiwa kucheza mchezo mwengine wa kirafiki na timu ya Gulion mchezo ambao utavurumishwa usiku wa leo katika kiwanja cha Amani mjini Unguja.

Wachezaji wa Simba.

Simba ambayo imeeka kambi kisiwani Unguja kujiandaa na mchezo wa Ngao ya hisani dhidi ya Yanga sambamba na ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mchezo na Gulion utakuwa mchezo wa pili wa kirafiki kisiwani hapa.

Kikosi cha Simba.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa timu ya Gulion ambae pia aliwahi kuwa kocha wa timu ya Simba Burghani Himid  Msoma amesema mchezo huo wa kirafiki utaisaidia kikosi chao katika  kukianda kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Kocha wa timu ya Gulion FC Burghani Himid  Msoma 

Amesema kuwa amekiona kikosi cha Simba na namna wanavyocheza na anatarajia mchezo wa usiku huu utakuwa na ushindani wa hali ya juu nawakuvutia.



Umaliziaji ndio tatizo kwetu ,Mayanja..Simba yalazimishwa sare na Mlandege.

 Kocha msaidizi wa timu ya Simba Mayanja amesema umaliziaji umekuwa tatizo katika kikosi chao jambo ambalo kwa sasa mwalimu analifanyia kazi kwa nguvu zote.

Kocha huyo ameyasema hayo baada ya sare yakutokufunga na timu ya Mlandege ikiwa ni miongoni mwa michezo ya kirafiki kwa timu hiyo iliyopo kisiwani kujiandaa na mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya Yanga.


Amesema licha yakutengeneza nafasi kadhaa lakini bado safu yake ya usambuliaji inaoneka haipo makini sana hivyo wanazitumia simu hizi zilizosalia kurekebisha matatizo hayo.


Thursday, 17 August 2017

Miembeni City yaanika nyota wake wapya,yaanza kujinoa kwa ajili ya ligi.

Kikosi cha Miembeni City kimeanza rasmini maandalizi ya msimu mpya wa ligi chini ya kocha Muhamed Seif King katika kiwanja cha Amani mjini hapa.
Mlinzi wa kati wa timu ya Miembeni City Abdullatif Juma Tiago aliesajiliwa msimu huu akitokea Criss.

Kikosi hicho ambacho kwa mara ya kwanza kitashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu huu kimeongeza sura mpya kumi.
Ali Bausi mchezaji aliesajiliwa Miembeni City akitokea Muembeladu.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha habari wa timu hiyo Ali Khamis Ibny amesema wamefanya usajili kulingana na matakwa ya mwalimu mkuu wa timu hiyo sambamba na ligi husika.

Akiwataja nyota hao ambao wameongezwa katika kikosi hicho ni pamoja na walinda milango Ali Rajab kutoka Zantex na George Munish ambae ni mchezaji huru.
Ali Rajab mlinda mlango wa Miembeni City aliesajiliwa akitokea Zantex.

Pia timu imewasajili walinzi Abdullatif Juma Tiago kutoka Criss,Halid Bofu kutoka Twalipo academy Dar es salam, Nassoro Abdallah ,Abdallah Heri wote kutoka United Mtoni,
Nassoro Abdallah mwenye kusubiri mpira na ,Abdallah Heri ambao ni miongoni mwa nyota wapya wa Miembeni City waliotokea United Mtoni,
Wengine ni Muhamed Jeilani Msuva kutoka Criss, Ali Bausi kutoka Muembeladu,Feisal Lucas Nado kutoka Chukwani United na Muhamed Abdallah Banka JKU.
Muhamed Banca nyota mpya wa Miembeni City aliyesajiliwa akitokea JKU.

Aidha amesema kwa mujibu wa mipango ya mwalimu kikosi hicho kitacheza michezo minne ya kirafiki yakujieka sawa kwa ajili ya mfumo mpya wa ligi.
Kocha mkuu wa timu ya Miembeni City Muhamed Seif King akizungumza na wa timu hiyo baada ya amzoezi ya asubuhi.

Miembeni City ambayo itashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa mara ya kwanza imepania kuona inafanya vyema katika ligi hiyo.


Wednesday, 16 August 2017

Simba kujipima na Mlandege, kesho.

Timu ya Simba SC ambao wapo Visiwani Zanzibar kwaajili ya kuweka kambi hadi Agost 22, 2017, kesho Alhamis watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Mlandege SC mchezo ambao utasukumwa majira ya saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.


Mlandege ambao wamepanda daraja kutoka la pili wilaya ya mjini hadi la pili taifa ambalo watacheza msimu ujao kwa sasa imekuwa moja kati ya timu zenye kufanya vyema katika soka la Zanzibar lengo nikurejesha hadhi ya timu hiyo iliyokuwanayo katika miaka ya 90.



Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba kucheza Visiwani hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo pia itakuwa ni mchezo wake wa tano wa kirafiki kufuatia kucheza michezo minne.

Tuesday, 15 August 2017

Simba yaanza kujifua Zenj bila Bocco.

Kikosi cha Simba asubuhi ya leo kimeanza mazoezi yake visiwani Zanzibar kujianda na michezo ya ligi kuu soka ya Vodacom sambamba na mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya Yanga unaotarajiwa kufanyika September 23 mwaka huu.

Akizungumza na mtanadao huu mara yakumaliza kwa mazoezi ya asubuhi ya leo kocha msaidi wa timu hiyo Jackson Mayanja amesema hali ya kikosi chao ipo vizuri huku wakitarajia kufanya vyema katika msimu ujao wa ligi sambamba na mchezo wao dhidi ya mahasimu wao wa jadi.


Akizungumzia majeruhi yaliopo katika kikosi chao hicho kocha huyo amesema Shomari Kapombe na John Boko huku wakitarajia Boko kurudi mapema uwanjani kwani tatizo lake sio kubwa sana.










Sunday, 13 August 2017

Yanga waitwanga Mlandege huku Ajib akianza kupasia nyavu.

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Ibrahim Hajib leo amefunga bao lake la kwanza katika timu hiyo ikishinda 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege Uwanja wa Amaan, Zanzibar

Pamoja na kufunga dakika ya 50 akimalizia krosi ya Mzimbabwe Donald Ngoma, Hajib pia leo ametoa pasi ya bao la pili lililofungwa na winga machachari, Emmanuel Mrtin dakika ya 73.

Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika timu hizo zikiwa hazijafungana, kocha Mzambia, George Lwandamina leo alibadilisha wachezaji wote kipindi cha pili, kasoro kipa Ramadhan Awam Kabwili.

Na ni mabadiliko aliyoyafanya ndiyo yaliipa ushindi timu yake katika mchezo huo wa kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Simba Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa timu ya yanga  George Lwandamina amesema ameutumia mchezo kuangalia uimara wa wachezaji wake.

Nae kocha wa timu ya Malandege Jaala Salum amesema mchezo huo wameutumia kukitengeneza kikosi chao kuelekea msimu ujao wa ligi.

Yanga iko Zanzibar ikiendelea na maandalizi ya kujiwinda na pambano lao la ngao ya jamii dhidi ya Simba litakalopigwa agost 23 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo asubuhi ya leo kikosi hicho kitaelekea kisiwani Pemba kwa kambi kabla ya kurejea jijini Dar es salaam siku mbili kabla ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa hali juu.
.